Kuna jambo huwa nafikiria sana. Wengi humu huishia kutangaza biashara zao. Leo naona nizungumzie hawa jamaa wa drip irrigation system. Wengine nitawajia siku nyingine.
Hivi mnaona hiyo 1.8m kwa ekari ni watanzania wangapi wanamudu? fikiria mtu una ekari tano (5). unahitaji milioni ngapi? Sasa, nimeshawishika kuamini kuwa hiyo biashara inawalenga watu ambao kimsingi wanajiweza kiuchumi, na wala siyo kwa ajili ya kuwakomboa watu maskini.
Hivi, haiwezekani mkawa na mfumo ambao unaweza kuwaruhusu kuwafungia watu hiyo mifumo alafu mhusika akawa analipa kwa awamu? Kwa nini msitengeneze mfumo utakaoruhusu mkulima kulipa nusu ya bei wakati mnamfungia, alafu inayobaki akailipa kwa awamu mbili (miezi miwili). Angalau hata ukiweka na riba kidogo juu yake siyo mbaya maana mtakuwa mmemkomboa huyu mkulima.
Pia mnaweza kuangalia assets ambazo huyu mkulima anaweza kuziweka kama dhamana. Amini nawaambieni, mkifanya hivi mtapata wateja wengi sana. Wakulima wengi tatizo lao ni gharama ya kuanza. Kama kweli tunataka kumaliza tatizo la umaskini, nashauri tuwaangalie wakulima wa chini kabisa na tuwainue kupitia huduma hizi.