Ujumbe kwa Chadema

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,010
2,000
Chama cha demokrasia na maendeleo kimejipambanua kama chama kikuu cha upinzani. Chama hiki kina matarajio makubwa sana kushinda uchaguzi wa 2015 na kushika dola.

Hata hivyo naomba nikitahadharishe kuwa kuna vikwazo vingi na hatari mbele. Ingawa CHADEMA kinaiona CCM kama ndio tatizo kubwa mimi nina maoni tofauti kidogo. Tatizo si CCM hasa bali ni ufisadi au umafia unaoshamirishawa na nguvu ya fedha tana fedha chafu. Ufisadi/umafia ndio hasa ulio na nafasi ya kuiweka serikali uitakayo madarakani. Ikiwa wataona kuwa CCM inaanguka na CDM inashamiri watatafuta namna ya kujipambanua nacho. Na hapo tatizo la nchi litabaki palepale

Hali halisi inaonekana pale ambapo kila mtu analalamika kuhusu ufisadi si ccm si upinzani. Umafia unajali zaidi maslahi yake. Ukiona unashidwa huanza mbinu chafu za kuwatokomeza wanaoupinga bila kujali wanatoka chama gani. Mbinu nyingine ni kuweka mamluki katika vyama na serikali.

Katika hali kama hii ni vena CDM kikatafakari mbinu kabambe za kivita. Hii si kazi ya lele mama na wala si kazi ya kuandamana tu ni mapambano ya kisayansi. Kila anayepinga ufisadi kwa moyo wote asipuuzwe hata kama anotoka chama tofauti.
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,530
2,000
Ndugu yangu, ufisadi na umafia unaozungumzia unadhaminiwa na CCM.
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,010
2,000
umeongea vizuri ......ila ungetupa na maoni yako on wat to do
tangu sasa uongozi wa Chadema ufanye upembuzi/uchambuzi wa kiana na kutoa maelekezo kuanzia ngazi za chini kuhusu mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo ili kuleta ushindi.
Pia kuchukua tahadhari dhidi pandikizi za mamluki ambao ni wawakilishi wa mafisadi/mafia
kuhamasisha kwa nguvu zote wafuasi wake wasifanye fujo maana hilki ni kigezo wanachotumia maadui kujenga sura ya chadema
kwamaba tujue kwamba ingawa tunaona CCM ni adui lakini lakini pembeni kuna adui aliyejificha mabaye huwasaidia baadhi ya watu kutoka vyama kwa ajili ya kulinda maslahi yoa
Ni lazima sasa chama kijengwe kutoka chini kabisa hata kwa kwa gharama.
elimu ni ya demokrasia ni lazima. watu wahamasishwe kukichangia chama kama ilivokuwa wakati wa kugombea uhuru. yapo mengi
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,010
2,000
Ndugu yangu, ufisadi na umafia unaozungumzia unadhaminiwa na CCM.
umezungumza vema lakini kwa kinyume. si kwali kuwa CCM inawadhamini mafisadi bali ni mafisadi wamebaini udhaifu wa ccm na kujipenyeza humo kwa kuwadhamini baadhi yao ili kulinda mfumo wa kifisadi na kimafia. Chama chochote kinaweza kujikuta katika hali kama hii. kwanza wanaanza wachache na kisha taratibu wanaongezeka na ndipo inakuwa vigumu hata kuleta mabadiliko pale chama kinapokuwa kimetekwa kwa sehemu kubwa. Nguvu ya fedha ni tishio sana. ndio maana inakuwa vigumu kwa sasa mtu kupenya ndani ya chama kama ccm akapewa uongozi bila kuwa na fedha
 
mr.kifather

Member
Feb 10, 2012
83
0

ahsante sana arifu hapo "kwenye fujo ndani ya harakati za cdm ni muhimu nadhani kuliko yote kwa sasa''
fujo ni virus anae pandikizwa kuwanyima chadema wafuasi muhimu kama wanawake
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,971
2,000
kumbuka walioshika dola ni ccm na ndio wameingia madarakani kwa pesa chafu kama za EPA zingine! CCM wametajiwa mafisadi kwa majina(Ref. Dr, Slaa "List of Shame") huu mfumo wa kimafia unasimamiwa na viongozi wa ccm mfano majuzi tu tumeona mwindaji haramu akipewa cheo cha utendaji mkuu wa chama, aliyeingiza taifa kwenye mkataba tata wa richmond anataka kuogombea urais! alipokea pesa chafu ya radar ni mwenyekiti wa kamati nyeti ya bunge! sasa chadema wamekuwa sikuzote wakisimama kwenye kusimamia rasilimali za nchi ziwanufaishe wote! wakiingia madarakani kazi ya kazi ni kuvunja uti wa mgongo wa mafisadi na mafia na kurudisha dhana ya uwajibikaji!Hivi tu wakiwa kwenye upinzani wanachachafya serikali hiyohiyo ya mafia hadi rais anavunja baraza la mawaziri bila kupenda sembuse wakabidhiwe dola! mbona wezi, mafisadi, mafia na wazembe watahama nchi??
 
nakuelewa sana arifu
 
angalizo nao jamaa ni virus wanaweza penya hata ndani ya cdm wasipo jipanga kikomando
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,971
2,000
angalizo nao jamaa ni virus wanaweza penya hata ndani ya cdm wasipo jipanga kikomando

Usijali mkuu intelijensia ya chama inafanya very perfect ndio maana kila mbinu chafu zinazopangwa dhidi yetu tunazing'amua kabla ya utekelezaji!
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,010
2,000
kumbuka walioshika dola ni ccm na ndio wameingia madarakani kwa pesa chafu kama za EPA zingine! CCM wametajiwa mafisadi kwa majina(Ref. Dr, Slaa "List of Shame") huu mfumo wa kimafia unasimamiwa na viongozi wa ccm mfano majuzi tu tumeona mwindaji haramu akipewa cheo cha utendaji mkuu wa chama, aliyeingiza taifa kwenye mkataba tata wa richmond anataka kuogombea urais! alipokea pesa chafu ya radar ni mwenyekiti wa kamati nyeti ya bunge! sasa chadema wamekuwa sikuzote wakisimama kwenye kusimamia rasilimali za nchi ziwanufaishe wote! wakiingia madarakani kazi ya kazi ni kuvunja uti wa mgongo wa mafisadi na mafia na kurudisha dhana ya uwajibikaji!Hivi tu wakiwa kwenye upinzani wanachachafya serikali hiyohiyo ya mafia hadi rais anavunja baraza la mawaziri bila kupenda sembuse wakabidhiwe dola! mbona wezi, mafisadi, mafia na wazembe watahama nchi??
hapo umenena mkuu
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,010
2,000
ahsante sana arifu hapo "kwenye fujo ndani ya harakati za cdm ni muhimu nadhani kuliko yote kwa sasa''
fujo ni virus anae pandikizwa kuwanyima chadema wafuasi muhimu kama wanawake
kweli wanawake na wazee wanaogopa sana kukisapoti Cdm pale wanapoambiwa ni chama cha fujo
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
4,480
2,000
Ndugu yangu, ufisadi na umafia unaozungumzia unadhaminiwa na CCM.

Ipo siku utakuja kugundua kwamba adui wa Mtanzania sio CCM, kama vile Waafrika Kusini sasa wanavyoona kuwa adui yao mkubwa hakuwa Mzungu kama walivyokuwa wanaaminishwa siku zote, sasa hivi ukiwauliza watu wa kawaida watakwambia, bora Mzungu aliwabagua lakini mwisho wa siku walipata kazi na kulipwa mshahara, au Wa Egypt kwamba adui mkubwa hakuwa Bw. Mubarak, au Wakenya kwamba adui yao mkubwa hakuwa KANU!

Tatizo ni sisi wenyewe na jamii yetu hapo ndipo tatizo lilipo, kulaumu CCM ni kutafuta ufumbuzi rahisi kwa tatizo kubwa zaidi, hiyo siku itafika, na utarujdi haa tena, kwa nguvu ile ile ila wakati huo jina la adui litakuwa limebadilika halitakuwa CCM tena!

marembo

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
202
170
Wewe unayejiita mzamifu unawaza usawa wa urefu wa pua na huna geni katika thread yako. nani ambaye hajui ufisadi ndio sera ya CCM (Magamba). Unataka kutupeleka darasa lipi wewe katika kuwaza ukaona unapiga bao kwa ***** wako huo. Ufisadi na CCM wanakaa chumba kimoja na hicho chumba ni la zima kisafishwe na kupigwa dawa kali ili kufuta hawa jamaa wawili marafiki wasiwepo na kurudisha heshima na raslimali. Tulishasema JF imekuwa kijiwe cha watu wasikuwa na michango. Yale yale aliyosema Mbunge Wa Iringa Mjini (Mch Msigwa): kuwa matatizo hayawezi kutatuliwa na fikira au mawazo yale yale yaliyosababisha matatizo hayo. Unahitaji fikira za upeo wa juu zaidi. Magamba wamekwama wapishe wana ukombozi (M4C.)
 
tatizo au adui yetu ni nani mkuu tuweke waz
 
KIRUMO

JF-Expert Member
Sep 25, 2012
416
250
umezungumza vema lakini kwa kinyume. si kwali kuwa CCM inawadhamini mafisadi bali ni mafisadi wamebaini udhaifu wa ccm na kujipenyeza humo kwa kuwadhamini baadhi yao ili kulinda mfumo wa kifisadi na kimafia. Chama chochote kinaweza kujikuta katika hali kama hii. kwanza wanaanza wachache na kisha taratibu wanaongezeka na ndipo inakuwa vigumu hata kuleta mabadiliko pale chama kinapokuwa kimetekwa kwa sehemu kubwa. Nguvu ya fedha ni tishio sana. ndio maana inakuwa vigumu kwa sasa mtu kupenya ndani ya chama kama ccm akapewa uongozi bila kuwa na fedha
Ni vema CDM wakafahamu mapema kuwa safari hii watapambana na nguvu ya pese na si nguvu ya ushawishi wa kisiasa. Kwa kuwa CCM inafahamu fika kuwa haimo katika mioyo ya wananchi wa kawaida (japo hawakiri hilo) watataka kutumia kila silaha ili kibaki madarakani ikiwa ni pamoja na pesa. Safari hii huenda ikawa zaidi ya EPA. Dawa ni kujenga chama mapema kuanzia ngazi ya chini na kuhakukusha kuwa elimu ya uraia inatolewa katika ngazi hiyo. CHADEMA time is not your ally. CCM wakishindwa uchaguzi wanaweza hata kutumia Jeshi! Mnakumbuka vitisho vya mnadhimu mkuu mstafu wa JWT- Abdurahaman Shimbo katika kampeni za uchaguzi uliopita?? Kwa CCM, all option are on the table. Ni suala la CDM kuiandaa jamii sasa! penyeni hadi vijijini!!!!
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
6,010
2,000
Wewe unayejiita mzamifu unawaza usawa wa urefu wa pua na huna geni katika thread yako. nani ambaye hajui ufisadi ndio sera ya CCM (Magamba). Unataka kutupeleka darasa lipi wewe katika kuwaza ukaona unapiga bao kwa ***** wako huo. Ufisadi na CCM wanakaa chumba kimoja na hicho chumba ni la zima kisafishwe na kupigwa dawa kali ili kufuta hawa jamaa wawili marafiki wasiwepo na kurudisha heshima na raslimali. Tulishasema JF imekuwa kijiwe cha watu wasikuwa na michango. Yale yale aliyosema Mbunge Wa Iringa Mjini (Mch Msigwa): kuwa matatizo hayawezi kutatuliwa na fikira au mawazo yale yale yaliyosababisha matatizo hayo. Unahitaji fikira za upeo wa juu zaidi. Magamba wamekwama wapishe wana ukombozi (M4C.)
Mkuu wewe unaona kuwa nawaza kama ulivosema. Unathibitisha vipi kuwa hilo ni sahihi. Nadhani umejibu haraka bila kufikiri. Nimesema ndani ya ccm kuna watu wamejikuta wanautumikia mfumo wa kifisadi si kwa kupanga bali kwa udhaifu wao wakajikuta wamegeuka wakala wa mafisadi. Zaidi ni kuwa Mafisadi wamejipenyeza ndani ya CCM kwa kutumia nguvu ya fedha. wanaweza haohao wakajipenyeza ndani ya vyama vingine kama si wakati huu ni wakati mwingine. sasa wewe ulichosema japo ni sahihi lakini namna ulivosema umeashiria kitu fulani ambacho kinaweza kukupunguzia heshima mkuu. angalia mbali zaidi CCM haikuanza naa nguvu ya fedha bali nguvu hiyo imeikuta CCM ipo nayo ikajaribiwa ikasalimu amri kwa hiyo kilichopo nyuma ya CCM ni nguvu ya pesa/ufisadi/umafia sasa watu kama wewe wanaona tu CCM ni sawa na mtu anaona uso umejaa machunusi anaanza kupaka madawa kumbe tatizo lniaanzia katika damu. sasa utapaka madawa adi uso uwe kama wa chatu lakini tatizo liko paleplae
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom