Ujumbe kutoka kwa Muslim Hassanali

Ujumbe kutoka kwa Muslim Hassanali

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958
Nimepitia na kusoma "comments" za Wadau kwenye(mitandao ya kijamii) Social Media kuhusiana na Mimi kujiunga na CCM Tarehe 9 Januari 2018.

Nawashukuru wale wote waliyechangia mawazo, ushauri, matusi, kejeli na kadhalika na kuyathamini maoni yao. Kwa kuwa wametumia MUDA wao na gharama za Bundle zao za internet. Asanteni wote.

Napenda Tu kusema kwamba, kwa wasiyenijua sio makosa Yao, kwa kuwa muda mwingi wapo "Online" kwenye Facebook,Instagram na wattsapp. Kuna mengi hawajui au kwa maksudi kabisa wanayapinga ili waonekane wanajua kutukana na kukashifu for their own personal benefits.

Nimeona maajabu kusoma pia maandiko ya baadhi ya viongozi wa Chama changu cha zamani eti...wanapinga kuwa Mimi sio "MJUMBE WA BODI YA WADHAMINI". Na baadhi pia kudiriki kusema "NDANI YA CHADEMA WOTE TAKATAKA KASORO TUNDU LISSU"

Sishangai kwa kuwa nimeishi nao muda mrefu na naelewa uwezo wao wa kufikiri na pia naifahamu vizuri matumizi ya midomo yao.

Kuna wengine walikuwa ni walinzi wa viongozi wakuu, Leo wamebahatika kupata vyeo lakini wanashindwa kubadilika na hatimaye uwezo wao wakufikiri unaleta mashaka.

Anyways, sina haja ya Kuthibitisha "Cheo" changu na "Mchango" wangu kwenye chama changu cha zamani.

Naamini, Viongozi wa hicho chama wanalitambua hilo.
Na kuliko kubishana na vijana wasio elewa mamlaka na vyeo, ni mantiki wakawaulize akina Mhe. Freeman Mbowe na Mzee Arcado Ntagazwa ambao nawaheshimu sana, watapata majibu sahihi.

Kwa wale wote ambao hawajabahatika kwenda kufanya kazi za siasa "field" na Mwisho wao ni kwenye comment box za social media. Ili wapate mwanga juu ya mambo wanayo dandia bila kufanya uchunguzi sahihi.

Nimejiunga Chadema kuanzia 2003, na mwaka 2005-2018 hadi najiuzulu nimetumikia nafasi hiyo. Na pia nafasi zingine nyeti ambazo sioni umuhimu kuzitaja kwa kuwa sina tabia ya kumwaga "mtama" penye kuku wengi.

Sitarajii malumbano, sina muda Huo, nipo na harakati za ujenzi wa Taifa kwa maslahi ya Wananchi wote.

Sitaki mutoe "mapovu" hapa. Wenye upeo mpana wanaelewa, na wengine waliopungukiwa endeleeni kutoa "mapovu"

Fanyeni kazi! Jengeni Nchi na Familia zenu.

Hapa Kazi Tu!

CCM MPYA.....

TANZANIA MPYA.....

By: MUSLIM HASSANALI
Mwanachama - CCM
 
Usaliti ni laana mbaya sana .

Ulichosahau hapa ni kuwashukuru wote waliotumia pesa zao kama mimi na muda wao kukuhangaikia usiku na mchana kwenye uchaguzi mkuu 2015 , umesahau kuwashukuru hata waliokutilia mafuta kwenye gari lako .

Mungu hatokuacha utatandikwa laana ya ajabu sana .
 
Huyu hasanali sijui ni very insignifcant figure,
mie mwenyewe hata ndo namjua juzi,

yaani kupewa kazi ya kwenda kudraw hela bank na kuzitawanya kwenye majukumu mbalimbali,tayari ashajiona alikuwa mtu mkubwa sana.

We si ulikuwa cashier tu,mchango mchango upi?
Au hizo pesa ulikuwa unatoa mfukoni mwako?.

Watu kama huyu hasanali,tukikamata madaraka ni kuwaweka ndani kwa uhujumu uchumi bila dhamana hadi waozeemo
 
Usaliti ni laana mbaya sana .

Ulichosahau hapa ni kuwashukuru wote waliotumia pesa zao kama mimi na muda wao kukuhangaikia usiku na mchana kwenye uchaguzi mkuu 2015 , umesahau kuwashukuru hata waliokutilia mafuta kwenye gari lako .

Mungu hatokuacha utatandikwa laana ya ajabu sana .

Kama ulifanya hayo u nasubiri shukrani za nini?
Msaliti ni wewe usiyetambua ulifanyalo.
Amefanya maamuzi muache pambana na yako,endelea kutia mafuta na kukesha kwenye uchaguzi
 
Kweli wana bavicha ni kichomi kipya kwa taifa letu. michango yenu inadhihirisha kuwa mmebaki na mabichwa makubwa ya kutunga uongo na kutukana. mwacheni muhindi achape kazi chini ya chama makini CCM. nyie endeleeni na uzushi na upigaji madili ambayo siku si nyingi yanaenda kupotea nanyie mtapotea na viongozi wenu wapiga madili (mbowe, lema, mdee n.k).
 
Back
Top Bottom