Ujumbe ktk wimbo wa bahati bukuku-dunia haina huruma

Ujumbe ktk wimbo wa bahati bukuku-dunia haina huruma

Fugwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
1,676
Reaction score
664
Mumewake Bahati Bukuku alikuwa na hawara ambaye naye ana mume akitesa naye kwa rahazao na kusahau kabisa ndoa yake. Mwanamke huyo wa nje alionyesha dharauiliyokithiri dhidi ya Bahati Bukuku, Bahati akawa yeye siku zote ni mtu wakulia tu kwani mume wake alikuwa anamaliza wiki bila kuonekana nyumbani nahawara huyo kwa jeuri na kejeri wakiwa kitandani anampigia simu bahati iliasikilize wanavyotesa na mume wake.
Ilitokeasiku moja fumanizi likafanyika, mume wa Bahati kakatwa katwa mapanga naakatupwa kichakani wakidhani wameua. Kwa bahati yake walipita wasamaria wemawakamchukua na kumkimbiza hospitali wakidhani labda amepigwa na majambazi.Akiwa hospitali, yule hawara yake naye baada ya kupewa kichapo na mume wake,aliamua kumpigia simu Bahati kwa kejeri akisema nenda hospital kachukue maitiyako. Kwa vile siku zilikuwa zimepita mume wake bila kuonekana nyumbaniilimlazimu kwenda hospital na akamkuta mume wake hoi na hajitambui. Alipoongeana Daktari alimwambia lazima afanyiwe operation haraka ili kuokoa maisha yamume wake.
Bahatimbaya, Bahati hakuna na senti hata moja, ilibidi aende kwa rafiki yake mumewake ambaye wameshibana ili amwazime hela za kulipia operation hiyo, jamaaalitolea nje akisema hela aliyonayo ni ya kumpeleka uingereza kuangalia premierligi. Bahati hakukata tama ilibidi aende kuomba hela kwa wifi yake yaani dadawa mume wake, naye alimkatalia akisema hela yake ni ya kulipia ngoma ya sengereambayo anatarajia kuicheza kesho yake kwenye sherehe ya unyago wa mwanaye.Bahati alizidi kufanya jitihada ili apate hela siku hiyo, akaamua kwenda kuwekaBondi gari lao aina ya Range Rover Vague kwa Daktari, Daktari naye alikataa kwakigezo kwamba gari hilo ni kiwavi kwenye mafuta hivyo hawezi kulinunua.
Mpakakufikia hapo Bahati hakuwa na la kufanya kwani fursa zilizokuwepo za kupatahela ziligoma. Alienda kumwomba Daktari ili aokoe maisha ya mume wake, Daktarialimkubali kwa sharti la kumtaka Bahati avue chupi. Kwa vile Bahati alikuwa akimpenda mume wake alikubaliananaye na operation ikafanyika.
Mapenziyalikuwa ya motomoto na wakati mwingine Bahati akijilazimisha ilimradi mumewake apone na waendelee na maisha yao ya kawaida. Mume alipata nafuu nakuruhusiwa kurudi nyumbani. Wakati huo Bahati alikuwa ameshashika ujauzito nabaadae alijifungua mtoto mrembo wa kike.
Kashesheilianza hususan baada ya mume wake kupona. Kikao cha wanafamilia kiliitishwa naBahati akatakiwa awepo ili aseme mbele ya wazee wa ukoo na wanafamilia wenginekuhusu nani mwenye mtoto. Shemeji zakewalikuwa wachungu kwake kama pilipili, wifi zake walimkalia kooni kwamba anatakakuwaulia kaka yao, majirani zake na marafiki wote walimuona Malaya, rafiki yakemume wake aliyenyima hela za matibabu naye alimwambia kuwa anataka kuua rafikiyake yaani mume wake. Bahati alitamani Dunia imhurumie lkn fursa hiyo haikuwepona ikaamuliwa kwa vile motto aliyezaliwa ni wa vichakani basi auawe kwa kukatwakatwa mapanga.
Kablahukumu hiyo kutekelezwa alinyanyuka mzee wa ukoo mwenye busara akakiambia kikaokwamba kosa alilofanya Bahati haikuwa makusudi bali alikusudia kuokoa maisha yamume wake baada ya jitihada zote za kupata fedha za matibabu kukosekana naakaendelea akasema mtu ambaye hajafanya dhambi ya aina yoyote ainuke na awe wakwanza kumkata panga yule motto, wote walitazamana na wakainuka na kuondoka.
Je,ungekuwa wewe ndiye mume wa bahati ungeamua nini kwenye scenario kamahii?????????????
Mume wake Bahati Bukuku alikuwa na hawara ambaye naye ana mume akitesa naye kwa raha zao na kusahau kabisa ndoa yake. Mwanamke huyo wa nje alionyesha dharau iliyokithiri dhidi ya Bahati Bukuku, Bahati akawa yeye siku zote ni mtu wa kulia tu kwani mume wake alikuwa anamaliza wiki bila kuonekana nyumbani na hawara huyo kwa jeuri na kejeri wakiwa kitandani anampigia simu bahati ili asikilize wanavyotesa na mume wake.
Ilitokea siku moja fumanizi likafanyika, mume wa Bahati kakatwa katwa mapanga na akatupwa kichakani wakidhani wameua. Kwa bahati yake walipita wasamaria wema wakamchukua na kumkimbiza hospitali wakidhani labda amepigwa na majambazi. Akiwa hospitali, yule hawara yake naye baada ya kupewa kichapo na mume wake, aliamua kumpigia simu Bahati kwa kejeri akisema nenda hospital kachukue maiti yako. Kwa vile siku zilikuwa zimepita mume wake bila kuonekana nyumbani ilimlazimu kwenda hospital na akamkuta mume wake hoi na hajitambui. Alipoongea na Daktari alimwambia lazima afanyiwe operation haraka ili kuokoa maisha ya mume wake.
Bahati mbaya, Bahati hakuna na senti hata moja, ilibidi aende kwa rafiki yake mume wake ambaye wameshibana ili amwazime hela za kulipia operation hiyo, jamaa alitolea nje akisema hela aliyonayo ni ya kumpeleka uingereza kuangalia premier ligi. Bahati hakukata tama ilibidi aende kuomba hela kwa wifi yake yaani dada wa mume wake, naye alimkatalia akisema hela yake ni ya kulipia ngoma ya sengere ambayo anatarajia kuicheza kesho yake kwenye sherehe ya unyago wa mwanaye. Bahati alizidi kufanya jitihada ili apate hela siku hiyo, akaamua kwenda kuweka Bondi gari lao aina ya Range Rover Vague kwa Daktari, Daktari naye alikataa kwa kigezo kwamba gari hilo ni kiwavi kwenye mafuta hivyo hawezi kulinunua.
Mpaka kufikia hapo Bahati hakuwa na la kufanya kwani fursa zilizokuwepo za kupata hela ziligoma. Alienda kumwomba Daktari ili aokoe maisha ya mume wake, Daktari alimkubali kwa sharti la kumtaka Bahati avue chupi. Kwa vile Bahati alikuwa akimpenda mume wake alikubaliana naye na operation ikafanyika.
Mapenzi yalikuwa ya motomoto na wakati mwingine Bahati akijilazimisha ilimradi mume wake apone na waendelee na maisha yao ya kawaida. Mume alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Wakati huo Bahati alikuwa ameshashika ujauzito na baadae alijifungua mtoto mrembo wa kike.
Kasheshe ilianza hususan baada ya mume wake kupona. Kikao cha wanafamilia kiliitishwa na Bahati akatakiwa awepo ili aseme mbele ya wazee wa ukoo na wanafamilia wengine kuhusu nani mwenye mtoto. Shemeji zake walikuwa wachungu kwake kama pilipili, wifi zake walimkalia kooni kwamba anataka kuwaulia kaka yao, majirani zake na marafiki wote walimuona Malaya, rafiki yake mume wake aliyenyima hela za matibabu naye alimwambia kuwa anataka kuua rafiki yake yaani mume wake. Bahati alitamani Dunia imhurumie lkn fursa hiyo haikuwepo na ikaamuliwa kwa vile motto aliyezaliwa ni wa vichakani basi auawe kwa kukatwa katwa mapanga.
Kabla hukumu hiyo kutekelezwa alinyanyuka mzee wa ukoo mwenye busara akakiambia kikao kwamba kosa alilofanya Bahati haikuwa makusudi bali alikusudia kuokoa maisha ya mume wake baada ya jitihada zote za kupata fedha za matibabu kukosekana na akaendelea akasema mtu ambaye hajafanya dhambi ya aina yoyote ainuke na awe wa kwanza kumkata panga yule motto, wote walitazamana na wakainuka na kuondoka.
Je, ungekuwa wewe ndiye mume wa bahati ungeamua nini kwenye scenario kama hii?????????????
 
Follow my threads and you will know the answer very soon...!
 
Huwezi kutumia dhambi ili kutibia dhambi. Akajipange upya kwanza anadanganya kwa kutumia neno la Mungu
 
Huwezi kutumia dhambi ili kutibia dhambi. Akajipange upya kwanza anadanganya kwa kutumia neno la Mungu
Hajadanganya bali ulitaka udanfanywe kua hakufanya ivyo.
Hiyo aliyoongea ni reallity. Yanatokea hayo.
Ulitaka amalize kwa kudanganya watu kua mungu alishuka na kumpa izo ela?
 
Wimbo ule ni wa kishetani kabisa. Hauna maadili ya kikristo.
 
Kwa hiyo anatufundisha tukipata matatizo tumtumikie shetani ili kutafuta suluhu ya matatizo husika?
 
Mkuu Fugwe ni kweli (Kama unajua) huyo mwimbaji alifanya hivyo ama aliitumia tu kazi yake ya sanaa kuwasilisha yaliyotokea kwingine?
 
Back
Top Bottom