Ujumbe huu wa Makonda unamlenga nani?

Ujumbe huu wa Makonda unamlenga nani?

Hatari sana huyu ndugu.....anajiamini balaa..hadi anapitiliza..sifikiri kama ubongo wake huwa unachuja na kuidentify potential impacts ya maneno yatakayotoka mdomoni....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye hio clip anasema
" La nne ni kwa wale ambao mnafikiri mna vyeo vikubwa kuliko mimi, mjifunze kuwa na nidhamu kidogo nawazidi vitu vingi sana na hatulingani. Unaweza ukawa tunalingana kwa umri tumekuwa pamoja ba tumesoma pamoja lakini NAKUZIDI SANAA, kwa hio kidogo uwe na nidhu na wakubwa zako wananitambua."
Mwisho wa kunukuu.
Sasa swali langu ni kuwa huu ujumbe umemlenga nani?
Huyu bwana mdogo kampa nini Jiwe!

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Huyu bwana ananikumbusha ubabe wa Dk Kleruu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliyeuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa Desemba 25, 1971 na Mzee wetu Mamwindi wa pale Ismani

Nilikuwa mdogo ila nilikuwa nina akili ya kujua nn maana ya nikisikia mtu kauwawa,nakumbuka nilkuwa ninepelekwa mjini kutembezwa sikukuu nilikuwa nimetoka Kijijini kiwere,wakati nipo maeneo ya mshindo ndipo taarifa za huyu bwana kuuwawa nilizisikia,mzee wangu uso wake ulionesha kujawa fulaha na akatamka maneno ya kihehe yaliyomaanisha kuwa "HAKIKA HUYU BWANA NI MWANAUME",

Mwalimu alisikitishwa sana na hbr ile ila wengine walisema ni matokeo ya mwl kutosikiliza alipoambiwa juu ya ubabe wa mtumishi wake kipenzi!!!!!dah sikukuu iliishia mshindo tukaludi kijijini maana polisi walitapakaa mjini!

Mwl alikuwa akipenda mtumishi bhasi hata mseme nini juu ya mtumishi huyu mtakuwa mnajisumbua,kwa mfano alikuwapo RC Songambele, huyu bwana hakujua hata kusoma ila Mwl kwa mapenzi yake alimpa ukuu wa wilaya hadi ukuu wa mkoa matokeo yake watu wakawa wanapiga pesa kwa uzembe wa Songambele (Rejea kisa cha Tanesco aliposainishwa documents za kuidhinisha malipo hewa)

huyu bwana nae asije akafanya historia ijiludie maana maisha yake na Mkuu wa kaya yanafanana na ya Docta kleruu na Mwalimu (wote marehemu).
 
Precisely, anakera sana. Maneno yake yana ukakasi kuyasikiliza, ni mtu mjivuni anayedhani atakuwa hapo alipo siku zote.
Kweli mababu zetu waliona mbali sana hasa kwenye ule msemo wa masikini akipata masabuli hulia mbwata.
 
Saint Ivuga anayeambiwa hayo maneno ni mwanaharakati wa muziki WakaziMusic.. Pale Mkuu wa Mkoa wa Dar - Makonda alipowaita wasanii kupitia Steve Nyerere na Wakazi akahitaji kupewa wito rasmi. Steve akachonga sana.

Wakazi akaandika waraka 'Toilet Paper Inapolicheka Dodoki..' Ingia Instagram 'page' ya Wakazimusic utaiona..
 
huyu bwana ananikumbusha ubabe wa Dk Kleruu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliyeuawa kwa kupigwa risasi ya kichwa Desemba 25, 1971 na Mzee wetu Mamwindi wa pale ismani,

Nilikuwa mdogo ila nilikuwa nina akili ya kujua nn maana ya nikisikia mtu kauwawa,nakumbuka nilkuwa ninepelekwa mjini kutembezwa sikukuu nilikuwa nimetoka Kijijini kiwere,wakati nipo maeneo ya mshindo ndipo taarifa za huyu bwana kuuwawa nilizisikia,mzee wangu uso wake ulionesha kujawa fulaha na akatamka maneno ya kihehe yaliyomaanisha kuwa "HAKIKA HUYU BWANA NI MWANAUME",

Mwalimu alisikitishwa sana na hbr ile ila wengine walisema ni matokeo ya mwl kutosikiliza alipoambiwa juu ya ubabe wa mtumishi wake kipenzi!!!!!dah sikukuu iliishia mshindo tukaludi kijijini maana polisi walitapakaa mjini!

Mwl alikuwa akipenda mtumishi bhasi hata mseme nini juu ya mtumishi huyu mtakuwa mnajisumbua,kwa mfano alikuwapo RC Songambele,huyu bwana hakujua hata kusoma ila Mwl kwa mapenzi yake alimpa ukuu wa wilaya hadi ukuu wa mkoa matokeo yake watu wakawa wanapiga pesa kwa uzembe wa Songambele(Rejea kisa cha Tanesco aliposainishwa documents za kuidhinisha malipo hewa)

huyu bwana nae asije akafanya historia ijiludie maana maisha yake na Mkuu wa kaya yanafanana na ya Docta kleruu na Mwalimu(wote marehemu)
historia hujirudia
 
Back
Top Bottom