Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,302
- 144,615
Mary Trump, ni mtoto wa kaka yake na Rais Donald Trump, aitwaye Frederick Trump.
Huyu Mary kaandika kitabu kuhusu baba yake mdogo, yaani Rais Trump.
Kwenye hicho kitabu chake, katoa kila aina ya tuhuma.
Moja ya tuhuma alizotoa ni kwamba, Rais Trump alimlipa mtu hela ili amfanyie mtihani wa SAT ili aweze kupata udahili katika chuo kikuu cha Pennsylvania, moja ya vyuo bora kabisa Marekani na duniani na moja ya vyuo vilivyomo kwenye kundi la ivy league.
Mary Trump, akihojiwa na mwandishi wa habari wa ABC, Bw. George Stephanopolous, alipoulizwa kama anaweza kuthibitisha hayo madai yake kuwa ni ya kweli, akasema hawezi.
Sasa, msije mkadhani namzushia. Huyu hapa yeye mwenyewe akijibu kuwa hawezi kuyathibitisha hayo madai yake yaliyomo kwenye hicho kitabu chake.
Anzia kwenye dakika ya 1:58.
Kama hilo hawezi kuthibitisha:
1] Kwa nini kaliweka kwenye kitabu chake?
2] Mangapi mengine kayazusha?
3] Mzushi kama huyo anaaminikaje?
Inashangaza sana kuona watu wakimrejea huyu mzushi wamjadilipo Rais Trump.
Trump ana makando mengi mno yanayothibitishika. Hakuna haja wala ulazima wa kumrejea mzushi kama huyo Mary, ili kupata pointi za kumpondea Trump!
Aibu.