Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,338
- 144,823
- Thread starter
- #21
Uongo.Kwa tamaduni za wenzetu, hasa Wamarekani, kama kuna jambo ovu anajua limefanyika na anataka kuliweka wazi, atafanya hivyo hata kama hana ushahidi. Na haijalishi amekaa nalo moyoni miaka mingapi. Serikali inaweza kumsaidia kuchunguza/kutafuta ushahidi kama jambo hilo lina maslahi mapana kwa taifa. Mfano, Marekani kuna kesi nyingi tu za ubakaji/udhalilishaji wa kijinsia (kama ile "Me Too" movement) ambazo zimeripotiwa hata miaka 40 baadae na serikali imezichunguza na baadhi ya watuhumiwa kutiwa hatiani.
Huo utamaduni wa Wamarekani wa wapi?
Marekani niijuayo mimi haipo hivyo.
Kwenye medani za uandishi wa vitabu vya maana ni muhimu kwanza kufanya utafiti na kupata ushahidi halafu ndo unaweka hizo taarifa zako kwenye kitabu.
Siyo kinyume chake.
Eti unaandika uzushi. Halafu ukiulizwa kama una ushahidi, unasema huna.
Mambo hayako hivyo.
Fanya kwanza utafiti. Jiridhishe na usahihi wa taarifa zako. Halafu ndo andika kitabu chako.
Hiyo ndo Marekani niijuayo mimi na ambayo naijua vizuri sana tu.
Mary Trump ni mzushi na wala hafichi kuwa ni mzushi.