Ujue vyema mfumo wa umeme wa jua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujue vyema mfumo wa umeme wa jua

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mahesabu, Apr 22, 2011.

 1. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  SAID Mahupa, mfanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam anazungumzia adha ya umeme inayoendelea kuitikisa Tanzania akisema: “Suala la mgawo wa umeme limekuwa tatizo sugu lisilo na hatima.” Mahupa ambaye ni mmoja wa watu waliohitimu mafunzo ya ufundi katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wakati huo ikiitwa Chuo cha Ufundi Dar es Salaam, anaongeza kuwa: “Tatizo ni kwamba watu wengi hawajatambua kwamba upo umeme unaotokana na vyanzo vingine hasa umeme wa jua ambao una faida nyingi kulinganisha na huu wa kawaida.” “…Unajua, ingawa watu wengi huogopa zile gharama za awali, ukweli ni kwamba umeme huu ambao ni wa uhakika, una faida nyingi japo kutokana na kutokujua, wengi wanadhani ni ghari na hivyo, wanaukimbilia ule wa gridi ya taifa ingawa unawasulubu. Hii ni kwa kuwa penye miti hakuna wajenzi.”
  Said Mahupa anaongeza: “Umeme wa jua ni kama nabii asiyeheshimika kwao, ndiyo maana utaona japo upo bila usumbufu, bado si watu wengi wanaoutumia na si kwamba wanauchukia, isipokuwa tu, hawajaufahamu ulivyo na hasa hasa faida zake.”
  Katika kulizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Ufundi wa kampuni ya umeme utokanao na mionzi ya jua ya ENSOL TANZANIA LIMITED, Mhandisi Prosper Magali, anasema: “Inashangaza kuona hata katika kipindi kama hiki cha sikukuu ya Pasaka, watu wanaiadhimisha kimya kimya ndani ya giza kutokana na tatizo la umeme wa kutegemea maji ya mvua ambayo siyo ya uhakika.” Kuhusu faida za umeme wa mionzi ya jua dhidi ya umeme wa gridi ya taifa, Mhandisi Magali anasema: ”Kuna faida ni nyingi japo watu hawazijui na ndiyo maana tunapenda kutoa elimu hii kwa umma na bahati mbaya, wengine wanazijua lakini wanaogopa zile gharama za awali.” Anasema, miongoni mwa faida kubwa za umeme wa jua ni kwamba wa uhakika na haukatiki. Anasema mtu akianza kuutumia, ni wazi kuwa hautapata gharama za malipo zaidi ya zile za awali, hivyo ni tofauti kabisa na umeme wa kawaida ambao humtaka mteja kulipia kila mwezi na wengine karibu kila baada ya siku kadhaa kwa kuwa wana mita za LUKU.
  Mhandisi huyo mtaalamu wa umeme anasema, umeme wa jua hauna gharama za uendeshaji na uzalishaji maana hauhitaji mafuta wala maji kuuzalisha na badala yake, unahitaji mionzi ya jua ambayo ipo mahali popote na haiuzwi.
  Kwa mantiki hiyo, anasema umeme huo ni rafiki wa mazingira kwani pia, hautoi moshi wala kelele wakati wa kuuzalisha kama ilivyo kwa jenereta.
  Anafafanua zaidi kuwa umeme wa jua hauunguzi vifaa wala kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara hasa mfumo unapokuwa umejengwa kwa makadirio sahihi na wataalamu.
  ‘Umeme huu unafika kila mahali hata vijijini kwa kuwa hauhitaji nguzo na upatikanaji wake hauhitaji na hauna urasimu wowote,” anasema Magali na kuongeza kuwa, matumizi ya umeme utokanao na mionzi ya jua, ni moja ya njia sahihi za kupunguza matumizi ya umeme wa gridi ya taifa ili utumike vyema viwandani kuzalisha mali.
  Hata hivyo, mtaalamu huyo anasisitiza kuwa, umeme huo kwa kiasi kikubwa unahitaji nidhamu. Anasema Ili kupata matumizi bora, mtumiaji hatakiwi kununua vifaa vya sola bila ushauri wa kitaalamu kwani hutofautiana kutegemea na aina na saizi ya matumizi ya muhusika.
  Mtaalamu huyo kutoka ENSOL Tanzania Limited anasema ili mfumo wa umeme wa jua ukamilike, unahitaji vitu kadhaa ikiwamo mionzi ya jua ambayo ipo mahali popote na hailipiwi na pia, moduli ya sola (solar panel).
  Kuhusu betri, anasema hutumika kuhifadhi umeme toka kwenye moduli ili utumike kwenye vifaa wakati wa usiku au nyakati za mawingu mazito kunapokosekana jua.
  Kidhibiti chaji hutumika kuimarisha utendaji wa betri na kuongeza maisha yake. Kimsingi Magali anasema, “Betri huharibiwa kwa kutoa kiasi kikubwa cha umeme kwenda kwenye matumizi au kuingiza chaji zaidi ya kiwango kinachotakiwa toka kwenye sola panel.
  Anaongeza kuwa: “Inverter; ni kifaa kinachogeuza mkondo wa umeme toka mkondo nyoofu (DC) na kuwa katika mkondo geu (AC) ambao ni kama ule wa TANESCO au jenereta.”
  Anavitaja vifaa vingine kuwa ni pamoja na kidhibiti chaji, betri ya sola, kigeuza mkondo pamoja na vifaa vingine vya kuunganisha mkondo kama waya, swichi, skrubu na taa.
  “Sola paneli” anasema Mhandisi Magali, “Ni kifaa kinachobadili mionzi ya jua kuwa umeme. Huu ndio mhimili wa mfumo wa umeme wa jua
   
 2. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Je, hiyo solar power system inaweza kutumika kwa kupikia majiko ya umeme na kazi zingine zinazokaribiana na hiyo?
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  Jee waweza chomea vyuma?ie welding
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  poa mtz mpaka aone kapewa bure ndo anaamini vinginevyo abadiliki..
   
 5. mseseve

  mseseve JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 518
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  tunaomba mchanganuo zaid kuhusu kiwango cha umeme kinachohtajika katika nyumba ya kawaida
   
 6. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii mada ilishawahi kuzungumzwa si zamani sana hapa JF, kwa ufupi umeme wa jua nguvu zinakusanywa na solar panel ambazo zipo na uwezo tofauti (watts) lakini ukusanyaji huu huishia kwenye betri za 12v au hata 24v; hapo kifaa kinachofata ni inverter kubadili 12v/24v kwenda 220v/240v. Matumizi yako ni kujua kifaa/vifaa utakavyotumia vina-kula watts ngapi.
  Mfano wa nyumba: bulbs za kisasa (energy efficient) 8w mpaka 18watts...ukichukulia ni taa ngapi kwa wakati mmoja zitawaka basi utakua umepata jibu jumla ya watts zitakazo tumika kwa wakati mmoja hivyo ndio jibu la solar panel yako/zako (in watts).
  Ukifanya search kuna maelezo na links humu JF.
  Kuhusu majiko ya umeme/welding machines sio rahisi ukiangalia wattage za vifaa hivyo ni katika +1000 watts na zaidi. Umeme wa jua ni kama back-up ya taa na vifaa vyenye wattage ndogo.
  * betri ni kama zilivyo za gari.....yaani gari ndogo betri ndogo, basi/lori betri lazima iwe heavy duty kadhalika na kwa upande wa umeme wa jua matumizi makubwa pia yanahitahi heavy duty battery.
   
 7. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  mkuu umeme jua ki ukweli unafaa kwa mtu mwenye pesa tu.sio maskini kama mimi.kwanini?1. Unapo nunua system ya solar kila kifaa huwa ghali,kwanza connection yake inahitaji waya za kuanzia 2.5 mmt mpaka 6 mmt.betri,panel,invetor na huyo fundi pia ni wa bei mbaya. Maana hata ufungaji wa umeme wa kawaida upo tofati na wa jua.
   
Loading...