Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,205
- 5,332
Siku moja nikiwa usingizini ndipo maono yakaniijia kama ilivyokuwa kwa yohana wa ufunuo tofauti yake na mimi ikawa ndogo yeye alifunuliwa(aliambiwa maana ila mimi sikuambiwa maana zaidi ya kushuhudia),
Tazama nafsi ilikaribia mbingu mbele ya kiza kinene na tazama nilipofumbua macho yangu katika roho naliona mpangilio wa ajabu na kustaajabisha wa nyota mbalimbali
Tazama kulikuwako na mbingu mbili moja ni ile tuionayo kila siku lakini nyuma yake kulikuwako na ile mbingu ya pili na katika hii mbingu yakustaajabisha ipo tafsiri ya yale makundi ya nyota niliyoyaona katika mbingu ile ya kwanza yaani zile zodiac signs(constellations)
Kilichonishangaza zaidi nikuziona nyota zote jinsi zilivyo na michoro yake niliyoifahamu kupitia kwenye magazeti,vitabu n.k katika dunia hii tuishio zikiwa katika umbile la binadamu,wanyama, wadudu, mashujaa n.k
Nilikosa jibu kwanini iwe hivyo kule mbinguni? Na je ni nani huyo aliyeichora mbingu nakuinakshi kwa maumbo yenye rangi ya kupendeza na maumbile mbalimbali?
Pale pale nikasadiki kuwa Mungu yupo na ndie mchoraji,muhunzi na mratibishaji wa kila kilichopo pale kwa maana hata pamoja na uwezo waziada niliokuwa nao katika maono sikuweza kukaribia hata nukta ya umbali zilipo nyota zile nilizozishuhudia,
Ila swali lililonitesa hata baada ya kuzinduka nakutoka kwenye maono hayo ambayo siwezi kuelezea maajabu na siri chache nilizoshuhudia huko, nilijiuliza je ni wangap wameshayashuhudia yale niliyoyaona?
Na kama bado imekuaje michoro ile ile na maumbo yaleyale niliyoyashuhudia kwa macho yangu tuwe tukiyajua nakuyachora katika dunia yetu?
Tumeenda mbali zaidi na kuiba baadhi ya siri zilizoko kule kuhusiana na mahusiano yaliyopo kati ya nyota na maisha ya mwanadamu(kwa kutumia tarehe ya kuzaliwa)n.k
Je,mwanadamu amejua hivi vyote kupitia msaada wa viumbe visivyoonekana, ama kwa njia kama yangu au kuna siri kubwa ya uumbaji ambayo baadhi ya watu wanayo lakini wameifumba dunia kwa makusudi ya mazuri au mabaya? Au wenda mwanadamu angefunuliwa elimu hii angeweza kumjua vyema muumba wake nakumpa sifa au ingemletea dhahama ya uasi na kutenda maovu?
Naomba kushusha kalamu nakuishia hapa, yumkini sikulazimishi huyaamini haya niyanenayo ila imekupasa kutafakari kwa kina kwa nini wapo wasoma nyota toka zama za kale na walikuwa wakibashiri na vitu vinatokea kweli hata kabla ya kristo, Je, ni siri gani iliyofichika katika elimu hii?