Ujue ugonjwa wa Kichocho (Bilharzia); Chanzo, dalili na tiba

N

Nandi jr

Member
Joined
Feb 27, 2015
Messages
96
Points
95
N

Nandi jr

Member
Joined Feb 27, 2015
96 95
Hawajafikisha mkuu... wananiambia walikuwa wanapewa kutokana na vimo vya urefu....alafu izo daw ni mbili tofauti mkuu wangu..yani kwa ujumla ni vitatu
Kati ya hizo dawa walizopewa je kuna kidonge kimoja kilikuwa kidogo na cha duara na je unamaanisha kuwa walipewa vidonge viwili hivyo vya kichocho na kingine ambacho sio? Katika ukuaji wa mtoto urefu huwa unaendana na uzito japokuwa kuna wakati mtoto anaweza akawa na uzito usioendana na urefu wake na ndio maana wanawapima urefu. Sometimes inaweza kutokea ukamoverdose mtoto kwa sababu wapo ambao urefu wao unakuwa tofauti na uzito. Naomba uniambie kuhusu hiyo dawa nyingine tofauti waliyopewa.
 
cute b

cute b

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2014
Messages
16,549
Points
2,000
cute b

cute b

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2014
16,549 2,000
Kati ya hizo dawa walizopewa je kuna kidonge kimoja kilikuwa kidogo na cha duara na je unamaanisha kuwa walipewa vidonge viwili hivyo vya kichocho na kingine ambacho sio? Katika ukuaji wa mtoto urefu huwa unaendana na uzito japokuwa kuna wakati mtoto anaweza akawa na uzito usioendana na urefu wake na ndio maana wanawapima urefu. Sometimes inaweza kutokea ukamoverdose mtoto kwa sababu wapo ambao urefu wao unakuwa tofauti na uzito. Naomba uniambie kuhusu hiyo dawa nyingine tofauti waliyopewa.
Mkuu vipo viwili vya ivyo (ila sio ivyo huo ni mfano wa muundo wa izo dawa) ambazo zinamezwa kwa ajili ya kichocho na kama nyingine muundo huo huo nusu (yaani kinavunjwa ) wanapewa watafune nazani ni za minyoo.
 

Attachments:

N

Nandi jr

Member
Joined
Feb 27, 2015
Messages
96
Points
95
N

Nandi jr

Member
Joined Feb 27, 2015
96 95
Mkuu vipo viwili vya ivyo (ila sio ivyo huo ni mfano wa muundo wa izo dawa) ambazo zinamezwa kwa ajili ya kichocho na kama nyingine muundo huo huo nusu (yaani kinavunjwa ) wanapewa watafune nazani ni za minyoo.
Yah kama ni za muundo huo ni za kichocho na hiyo ya minyoo nayo inafanana na hiyo. Kwa umri wa wanao dawa ya minyoo lazima wameze kidonge kimoja kizima kwa sababu kina 500mg kama ni mebendazole au 400mg kama walipewa albendazole. Inawezekana dawa za kichocho ndio hizo walizovunjiwa maana walipewa kidonge kimoja na nusu. Lakini all in all dawa yoyote ile inaweza kuwa na side effect kutegemeana na mtu na mtu. Mojawapo kichwa kuuma, kizunguzungu, vipele, kutapika hata kuhara, hizo ni baadhi tu lakini kuna wakati anaweza kuwa na dalili hizo kama alikuwa na vimelea vya ugonjwa na akameza dawa.
 
cute b

cute b

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2014
Messages
16,549
Points
2,000
cute b

cute b

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2014
16,549 2,000
Yah kama ni za muundo huo ni za kichocho na hiyo ya minyoo nayo inafanana na hiyo. Kwa umri wa wanao dawa ya minyoo lazima wameze kidonge kimoja kizima kwa sababu kina 500mg kama ni mebendazole au 400mg kama walipewa albendazole. Inawezekana dawa za kichocho ndio hizo walizovunjiwa maana walipewa kidonge kimoja na nusu. Lakini all in all dawa yoyote ile inaweza kuwa na side effect kutegemeana na mtu na mtu. Mojawapo kichwa kuuma, kizunguzungu, vipele, kutapika hata kuhara, hizo ni baadhi tu lakini kuna wakati anaweza kuwa na dalili hizo kama alikuwa na vimelea vya ugonjwa na akameza dawa.
Asante mkuu wangu asante sana kwa kunitoa wasiwasi....
 
N

Nandi jr

Member
Joined
Feb 27, 2015
Messages
96
Points
95
N

Nandi jr

Member
Joined Feb 27, 2015
96 95
Asante mkuu wangu asante sana kwa kunitoa wasiwasi....
Nami nashukuru sana kama maelezo yangu yamekuwa msaada kwako. Anytime unaweza niuliza kuhusu masuala ya afya pale ambapo nitakuwa na uwezo napo nitakujibu.
 
cute b

cute b

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2014
Messages
16,549
Points
2,000
cute b

cute b

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2014
16,549 2,000
Nami nashukuru sana kama maelezo yangu yamekuwa msaada kwako. Anytime unaweza niuliza kuhusu masuala ya afya pale ambapo nitakuwa na uwezo napo nitakujibu.
Asante mkuu nitakuwa nakuuliza...nina janga lingine ila acha kwa leo kesho nitaakuuliza
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,238
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,238 2,000
1352582_Kichocho.jpg


Kichocho ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo ambayo humpata mtu anapotumia maji yaliyo na vijidudu hivyo vya maradhi hususan katika nchi za kitropiki (yaani zenye hali ya joto jingi). Bilharzia ni jina la kimelea cha ugonjwa huu.
Aina za minyoo inayosababisha ugonjwa wa kichocho kikuu kinachomuathiri binadamu ni hii ifuatayo: Mosi, Chistosoma mansoni ambayo imeenea katika nchi 53 na kwenye maeneo kadhaa ya Afrika, Caribbean, mashariki mwa Mediteranean na Amerika ya Kusini.

Aina ya Pili ni Chistosoma japonicum/ chistosoma mekongi, inayoathiri utumbo.


Tatu ni Chostosoma intercalatum- inayojulikana kama urinary bilharizia.
Na nne ni ile ya Chistosoma haematobium au urinary bilharzia, ambayo inaziathiri nchi nyingi za Afrika .
Ugonjwa wa kichocho unahesabiwa kuwa ugonjwa wa pili unaonea kwa wingi zaidi katika nchi zenye joto jingi.
Viini vya ugonjwa wa kichocho vilivyokomaa huishi katika mishipa kwenye kibofu na utumbo. Kimelea cha kike hutaga mayai mengi ambayo hutoka kwa mtu aliyeathiriwa na kwenda kwenye maji wakati wa kukojoa au haja kubwa. Mayai yanapokutana na maji huanguliwa na kutoa viluwiluwi ambao hupenya na kuingia ndani ya konokono wa majini.


Aidha viluwiluwi hawa hukuwa ndani ya konokono hao, kuongezeka na hatimaye kutoka. Ifahamike kuwa viluwiluwi hawa wana uwezo wa kupenya ndani ya ngozi ya mwanadamu na wakisha penya huingia hadi katika mishipa ya ini, ambako hukua na kukomaa. Baada ya hapo huingia katika mishipa ya kibofu cha mkojo na utumbo mpana.
Vimelea hivi hutaga mayai kwa wastani wa miaka 3 na nusu, na vinaweza kuongezeka zaidi. Mayai yanayotagwa katika kuta za utumbo mpana na kibofu husababisha madhara makubwa.


Hata hivyo iwapo ugonjwa wa kichocho hautatibiwa ipasavyo, unaweza kusababisha matatizo ya ini, utumbo mpana na ugonjwa wa figo. Aidha maambukizo yake yanaweza kuenea katika uti wa mgongo na hata wakati mwingine kuathiri ubongo.
Karibu watu milioni 600 duniani wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kichocho tafit zimeeleza.


Ugonjwa unasababishwa na Nini?

Matatizo yafuatayo yanapelekea watu kupatwa au kuambukizwa ugonjwa wa kichocho: Umaskini uliokithiri, ufahamu mdogo kuhusu ugonjwa huo, usafi duni wa mazingira tunamoishi au kutoka kwa watu wanaohama kutoka katika nchi nyingine ambazo ugonjwa huo umeenea n.k.

Katika siku za awali wakati vimelea vya kichocho vinapoingia katika mwili wa mwanadamu, kijipele hujitokeza na baada ya kupita mwezi mmoja au miwili, mtu aliyekwishaambukizwa huanza kujisikia hali ya kuchoka, homa, homa ya baridi, huwa na kikohozi kikavu, maumivu ya misuli, maumivu ya tumbo, kuhara, na hukojoa mkojo ulio na damu. Kipindi hiki huenda sambamba na ukuaji wa minyoo katika mwili wa mwanadamu na hujulikana kama homa ya Katayama.
Hata hivyo kuwepo kwa damu katika mkojo ni dalili tosha ya kuonyesha kwamba mtu huyo amepatwa na kichocho cha mkojo au kitaalamu hujulikana kama urinary bilharzias. Na iwapo mgojwa hatatibiwa, anaweza kupata madhara mengine makubwa katika ini na bandama.


Kichocho uathiri zaidi watu gani?
Watu wazima wanaojishughulisha na kilimo na wale walio katika sekta ya uvuvi wako hatarini zaidi kukubwa na ugonjwa wa kichocho.
Kichocho kinachoathiri kibofu cha mkono huwaathiri watoto milioni 66 katika zaidi ya nchi 54 duniani na katika maeneo mengi watoto walio na umri wa kati ya miaka 10 na 14 wanaambukizwa ugonjwa wa kichocho. Kimsingi maradhi haya huathiri ukuaji wa watoto na mahudhurio yao shuleni.
Mtu anatakiwa kumuona daktari iwapo atakuwa amesafiri katika eneo ambalo lina maambukizo ya kichocho, iwapo ngozi yake itagusana na maji yenye vimelea vya ugonjwa huo na iwapo atakojoa mkono ulio na damu.


Namna ya kuzuia ugonjwa wa kichocho

Ugonjwa wa kichocho unaweza kuzuiwa kwa urahisi iwapo kanuni za kiafya zitazingatiwa. Hata hivyo hadi sasa hakuna chanjo iliyopatikana ya kudhibiti ugonjwa huo.
Si maji yote ni salama kwenye maeneo yaliyo na ugonjwa huu. sehemu hatari zaidi za ugonjwa huo ni maeneo kama vile kingo za maziwa, mito na mabwawa ambapo maji yametuama na kuna uoto wa mimea.
Sehemu salama ni kama vile katika fukwe za bahari na zile zenye mawimbi ambazo si rahisi kukuta konokono wa majini. Mabwawa ya kuogelea ni salama iwapo yatanyunyiziwa dawa ya klorini.


Ili kuweza kukabiliana na kuzuia maambukizo ya ugonjwa wa kichocho, masuala yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa: Miongoni mwao ni kuacha kuoga kwenye maji yaliyotuama kama vile ya kingo za mabwawa, mito n.k.
Licha ya hayo pia hakikisha kuwa maji ya kunywa ni salama kwa kuyachemsha na kuyachuja ili kuuwa vijidudu vya maradhi. Unaweza pia kuchemsha maji ya kuoga angalau kwa nyuzi joto 65 kwa muda wa dakika tano.


Maji yaliyohifadhiwa kwenye tanki kwa muda usiopungua masaa 48 ni lazima yawe salama kwa ajili ya kuogea. Kama unalima, unashauriwa kuvaa mabuti marefu ya mpira, Mtu anapaswa kumuona daktari baada ya kuwa na dalili za ugonjwa na yeye ndiye atakayemuainishia dawa za kutumia.
Ni matarajio yangu kwamba tukifuata kanuni na misingi yote hiyo ya kiafya niliyoitaja, tutashinda vita dhidi ya maradhi ya kichocho.

Ukiwa na Shida yoyote ile unaweza kunitafuta Kwa mawasiliano Bonyeza hapa.Mawasiliano
 
EMMYGUY

EMMYGUY

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Messages
8,518
Points
2,000
EMMYGUY

EMMYGUY

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2015
8,518 2,000
Asante Mkuu kwa Ushauri na Elimu, nimejifunza kitu.
 
Ashura9

Ashura9

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
740
Points
500
Ashura9

Ashura9

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
740 500
Kanda ya ziwa kinara kwa maambukizi ya kichocho

TUESDAY , 2ND FEB , 2016
Mikoa ya Kanda ya Ziwa imetajwa kuwa na kiwango cha juu cha maambuki ya ugonwa wa kichocho yanayofikia kiasi cha asilimia 50.
Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imeanza kutekeleza mpango wake wa kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele na imepanga kutoa chanjo za magonjwa ya kichocho kwa watoto wenye umri wa kwenda shule kuanzia Februari 4 mwaka huu lengo likiwa kuwaondolea watoto wadogo hatari ya kupata ugonjwa huo.

Maambukizi ya ugonjwa wa kichocho ni makubwa zaidi katika maeneo ya kanda ya ziwa ambapo yanafikia asilimia 50 hali inayoitaka serikali kuchukua hatua za karibu zaidi kukabiiliana na ugonjwa huo katika mikoa hiyo.

Akiongea leo jijini Dar es salaam mratibu wa taifa wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika wizara hiyo Dkt Pendo Mwingira amesema kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo ni kikubwa katika mikoa hiyo kutokana na uwepo wa vyambo mbalimbali.

Kufuatia hali hiyo Dkt. Mwingira amesema zoezi la kutoa chanjo hiyo litahusisha watoto wenye umri wa kwenda shule pamoja na watoto ambao hawajaanza shule watapata nafasi ya kupewa chanjo hiyo kuanzia Februari 4 mwaka huu.

Dkt. Mwingira ameongeza kuwa ugonjwa huo umekuwa ukienezwa na konokono katika maeneo ya maji yaliyosimama, katika mito pamoja na katika mabonde ya mpunga na madimbwi ya maji.

chanzo: eatv
 
K

kaijage mkiza

New Member
Joined
Oct 19, 2016
Messages
4
Points
45
K

kaijage mkiza

New Member
Joined Oct 19, 2016
4 45
Jaman ndugu zangu kuna ugonjwa fulani hivi ni kwamba;

Nikiwa nakojoa nahisi maumivu makali sana kwenye njia ya mkojo. Nahisi mle ndani kuna vidonda hasa panapounganikia kibofu na uume.

Nmetumia dawa nyingi sana lakini hakuna kilichosaidia ikiwemo siproxacilin, dox, flagily, na pia nimechoma sindano 6 lkn hakuna kilichonisaidia. Naombeni msaada ndugu zangu hili tatizo ni la mda mrefu sana.

Halafu pia na misuli ya uume imelegea si-perform vizuri kitandani ni dakika 1 tu mpaka kesho.

Msaada tafadhali
 
Gerry1

Gerry1

Member
Joined
Nov 25, 2015
Messages
58
Points
95
Gerry1

Gerry1

Member
Joined Nov 25, 2015
58 95
Pole sanaa ila kwa sababu tatizo ni la mda mref nahisi linachukua mda kupona kama ulitumia dozi ya vidonge na sindano vikapooza tatizo nakushauri urudie dozi mkuu .
 
N

niah

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Messages
6,185
Points
2,000
N

niah

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2015
6,185 2,000
Umeishakaa maeneo ya kando mwa ziwa Victoria? Pima kichocho. Ukiwa nacho ukikojoa mwishoni mkojo unauma halafu kanatoka kachembe ka damu hapo sasaaa. Kapime kichocho
 
Jamalm335

Jamalm335

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Messages
2,079
Points
2,000
Jamalm335

Jamalm335

JF-Expert Member
Joined Aug 5, 2015
2,079 2,000
Hizo dawa ulipewa hospital au uliamua tu kujinunulia pharmacy? Si kila ugonjwa unatibiwa na Ciproflaxin ama flagyl. Jaribu kwenda hospitali kwanza upimwe kisawa sawa halafu upewe dawa. Maradhi mengine tunajiongezea kwa kumeza dawa kimazoea. Pole.
 
D

drbinagi

Member
Joined
May 12, 2013
Messages
8
Points
45
D

drbinagi

Member
Joined May 12, 2013
8 45
Jaman ndugu zangu kuna ugonjwa flani hiv ni kwamba
Nikiwa nakojoa nahisi maumivu makali sana kwenye njia ya mkojo. Nahisi mle ndani kunavidonda hasa panapounganikia kibofu na uume. Nmetumia dawa nyingi sana lakini hakuna kilichosaidia ikiwemo siproxacilin, dox, flagily, na pia nimechoma sindano 6 lkn hakuna kilichonisaidia. Naombeni msaada ndugu zangu hili tatizo ni la mda mrefu sana. Nisaidieni tafadhali.
Halafu pia na misuli ya uume imelegea siperfome vizuri kitandani ni dkka 1 tu mpaka kesho.
Msaada tafadhali
Kwa haraka una dalili kama za UTI lakini inaweza ikawa inepanda juu kusababisha Cystitis (maambukizi katika kibofu). Japokuwa pia kuna magonjwa mengine zaidi ya hayo yanayoweza kuleta hali kama hiyo pia including Cancer, lakini tusiombee hayo.
Unahitaji kwenda hospitali kubwa iliyo karibu yako ambapo utapimwa mkojo, damu na vipimo vya ultrasound na Xray maalum ya kuangalia njia ya mkojo.
Hatahivyo nakushauri kunywa maji mengi na kutumia kinga unapofanya mapenzi.
 
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2014
Messages
11,293
Points
2,000
Zamiluni Zamiluni

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2014
11,293 2,000
kaijage mkiza pole mkuu,
kwa dawa ya kiarabu jaribu hii:- tumia abdalasini iliyosagwa na asali safi/origino (changanya katika kiombe) unywe, uanze na vijiko 3 alfajiri na adhuhuri na usiku...siku kadhaa utaona tija.., kama hakuna dalili ya uponyi... basi sitisha tiba hiyo!!

Au mfollow MziziMkavu ktk posts zake !!
 
bryan2

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Messages
2,272
Points
2,000
bryan2

bryan2

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2016
2,272 2,000
Fanya kipimo kinaitwa culture and sensitivity(mkojo)..

Na kama una mpenz ni bora mtibiwe wote.

Na ukipewa dose jitaidi kumaliza kbsa
 
MNYAMAKAZI

MNYAMAKAZI

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2014
Messages
2,133
Points
2,000
MNYAMAKAZI

MNYAMAKAZI

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2014
2,133 2,000
Niliwahi kupata tatizo kama lako hilo mkuu na nikatumia dawa hizo hizo na sindano juu (gentamycine) lakini wapii. Nikaenda hospitali kubwa nikafanyiwa kipimo kikubwa zaidi cha mkojo kinaitwa urine culture ndio akaonekana bacteria anayesumbua na kutibiwa. Kwenye majibu ya kipimo pia niliorodheshewa list ya dawa ambazo haziwezi kummudu bacteria huyu (ambazo kimsingi zote nilikuwa nimeshatumia). So mkuu achana na hayo madawa kwanza yatakuua figo ni makali mno. La msingi ingia mfukoni tafuta hospitali makini yenye wataalamu makini ukafanye kipimo cha uhakika uone tatizo ni nini. Hizi hospitali zetu za nchi ya viwanda hazitibu mkuu ni vituo vya kukomaza maradhi na kusindikizana akhera tu. Kule wanafanya kazi kwa mazoea tu, mf. ukimtajia dalili hizo ye anaconclude tu ni STD anakutwanga dozi moja amazing. Unapokwenda kutibiwa kwingine usiache kumwambia Dr. historia ya matibabu yako na dawa ulizotumia. Binafsi Dr. alishangaa sana nilipomueleza historia ya matibabu yangu na akanipa kauli moja kuwa kwny tatizo langu ilitumika bunduki kuua mbu.
 

Forum statistics

Threads 1,342,645
Members 514,741
Posts 32,758,629
Top