Ujue ugonjwa wa Kichocho (Bilharzia); Chanzo, dalili na tiba

Mkuu vipo viwili vya ivyo (ila sio ivyo huo ni mfano wa muundo wa izo dawa) ambazo zinamezwa kwa ajili ya kichocho na kama nyingine muundo huo huo nusu (yaani kinavunjwa ) wanapewa watafune nazani ni za minyoo.

Yah kama ni za muundo huo ni za kichocho na hiyo ya minyoo nayo inafanana na hiyo. Kwa umri wa wanao dawa ya minyoo lazima wameze kidonge kimoja kizima kwa sababu kina 500mg kama ni mebendazole au 400mg kama walipewa albendazole. Inawezekana dawa za kichocho ndio hizo walizovunjiwa maana walipewa kidonge kimoja na nusu. Lakini all in all dawa yoyote ile inaweza kuwa na side effect kutegemeana na mtu na mtu. Mojawapo kichwa kuuma, kizunguzungu, vipele, kutapika hata kuhara, hizo ni baadhi tu lakini kuna wakati anaweza kuwa na dalili hizo kama alikuwa na vimelea vya ugonjwa na akameza dawa.
 
Yah kama ni za muundo huo ni za kichocho na hiyo ya minyoo nayo inafanana na hiyo. Kwa umri wa wanao dawa ya minyoo lazima wameze kidonge kimoja kizima kwa sababu kina 500mg kama ni mebendazole au 400mg kama walipewa albendazole. Inawezekana dawa za kichocho ndio hizo walizovunjiwa maana walipewa kidonge kimoja na nusu. Lakini all in all dawa yoyote ile inaweza kuwa na side effect kutegemeana na mtu na mtu. Mojawapo kichwa kuuma, kizunguzungu, vipele, kutapika hata kuhara, hizo ni baadhi tu lakini kuna wakati anaweza kuwa na dalili hizo kama alikuwa na vimelea vya ugonjwa na akameza dawa.

Asante mkuu wangu asante sana kwa kunitoa wasiwasi....
 
Nami nashukuru sana kama maelezo yangu yamekuwa msaada kwako. Anytime unaweza niuliza kuhusu masuala ya afya pale ambapo nitakuwa na uwezo napo nitakujibu.

Asante mkuu nitakuwa nakuuliza...nina janga lingine ila acha kwa leo kesho nitaakuuliza
 
Kichocho.jpg


Kichocho ni ugonjwa unaosababishwa na minyoo ambayo humpata mtu anapotumia maji yaliyo na vijidudu hivyo vya maradhi hususan katika nchi za kitropiki (yaani zenye hali ya joto jingi). Bilharzia ni jina la kimelea cha ugonjwa huu.
Aina za minyoo inayosababisha ugonjwa wa kichocho kikuu kinachomuathiri binadamu ni hii ifuatayo: Mosi, Chistosoma mansoni ambayo imeenea katika nchi 53 na kwenye maeneo kadhaa ya Afrika, Caribbean, mashariki mwa Mediteranean na Amerika ya Kusini.


Aina ya Pili ni Chistosoma japonicum/ chistosoma mekongi, inayoathiri utumbo.

Tatu ni Chostosoma intercalatum- inayojulikana kama urinary bilharizia.
Na nne ni ile ya Chistosoma haematobium au urinary bilharzia, ambayo inaziathiri nchi nyingi za Afrika .
Ugonjwa wa kichocho unahesabiwa kuwa ugonjwa wa pili unaonea kwa wingi zaidi katika nchi zenye joto jingi.
Viini vya ugonjwa wa kichocho vilivyokomaa huishi katika mishipa kwenye kibofu na utumbo. Kimelea cha kike hutaga mayai mengi ambayo hutoka kwa mtu aliyeathiriwa na kwenda kwenye maji wakati wa kukojoa au haja kubwa. Mayai yanapokutana na maji huanguliwa na kutoa viluwiluwi ambao hupenya na kuingia ndani ya konokono wa majini.

Aidha viluwiluwi hawa hukuwa ndani ya konokono hao, kuongezeka na hatimaye kutoka. Ifahamike kuwa viluwiluwi hawa wana uwezo wa kupenya ndani ya ngozi ya mwanadamu na wakisha penya huingia hadi katika mishipa ya ini, ambako hukua na kukomaa. Baada ya hapo huingia katika mishipa ya kibofu cha mkojo na utumbo mpana.
Vimelea hivi hutaga mayai kwa wastani wa miaka 3 na nusu, na vinaweza kuongezeka zaidi. Mayai yanayotagwa katika kuta za utumbo mpana na kibofu husababisha madhara makubwa.

Hata hivyo iwapo ugonjwa wa kichocho hautatibiwa ipasavyo, unaweza kusababisha matatizo ya ini, utumbo mpana na ugonjwa wa figo. Aidha maambukizo yake yanaweza kuenea katika uti wa mgongo na hata wakati mwingine kuathiri ubongo.
Karibu watu milioni 600 duniani wako katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa kichocho tafit zimeeleza.


Ugonjwa unasababishwa na Nini?

Matatizo yafuatayo yanapelekea watu kupatwa au kuambukizwa ugonjwa wa kichocho: Umaskini uliokithiri, ufahamu mdogo kuhusu ugonjwa huo, usafi duni wa mazingira tunamoishi au kutoka kwa watu wanaohama kutoka katika nchi nyingine ambazo ugonjwa huo umeenea n.k.

Katika siku za awali wakati vimelea vya kichocho vinapoingia katika mwili wa mwanadamu, kijipele hujitokeza na baada ya kupita mwezi mmoja au miwili, mtu aliyekwishaambukizwa huanza kujisikia hali ya kuchoka, homa, homa ya baridi, huwa na kikohozi kikavu, maumivu ya misuli, maumivu ya tumbo, kuhara, na hukojoa mkojo ulio na damu. Kipindi hiki huenda sambamba na ukuaji wa minyoo katika mwili wa mwanadamu na hujulikana kama homa ya Katayama.
Hata hivyo kuwepo kwa damu katika mkojo ni dalili tosha ya kuonyesha kwamba mtu huyo amepatwa na kichocho cha mkojo au kitaalamu hujulikana kama urinary bilharzias. Na iwapo mgojwa hatatibiwa, anaweza kupata madhara mengine makubwa katika ini na bandama.


Kichocho uathiri zaidi watu gani?
Watu wazima wanaojishughulisha na kilimo na wale walio katika sekta ya uvuvi wako hatarini zaidi kukubwa na ugonjwa wa kichocho.
Kichocho kinachoathiri kibofu cha mkono huwaathiri watoto milioni 66 katika zaidi ya nchi 54 duniani na katika maeneo mengi watoto walio na umri wa kati ya miaka 10 na 14 wanaambukizwa ugonjwa wa kichocho. Kimsingi maradhi haya huathiri ukuaji wa watoto na mahudhurio yao shuleni.
Mtu anatakiwa kumuona daktari iwapo atakuwa amesafiri katika eneo ambalo lina maambukizo ya kichocho, iwapo ngozi yake itagusana na maji yenye vimelea vya ugonjwa huo na iwapo atakojoa mkono ulio na damu.


Namna ya kuzuia ugonjwa wa kichocho

Ugonjwa wa kichocho unaweza kuzuiwa kwa urahisi iwapo kanuni za kiafya zitazingatiwa. Hata hivyo hadi sasa hakuna chanjo iliyopatikana ya kudhibiti ugonjwa huo.
Si maji yote ni salama kwenye maeneo yaliyo na ugonjwa huu. sehemu hatari zaidi za ugonjwa huo ni maeneo kama vile kingo za maziwa, mito na mabwawa ambapo maji yametuama na kuna uoto wa mimea.
Sehemu salama ni kama vile katika fukwe za bahari na zile zenye mawimbi ambazo si rahisi kukuta konokono wa majini. Mabwawa ya kuogelea ni salama iwapo yatanyunyiziwa dawa ya klorini.

Ili kuweza kukabiliana na kuzuia maambukizo ya ugonjwa wa kichocho, masuala yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa: Miongoni mwao ni kuacha kuoga kwenye maji yaliyotuama kama vile ya kingo za mabwawa, mito n.k.
Licha ya hayo pia hakikisha kuwa maji ya kunywa ni salama kwa kuyachemsha na kuyachuja ili kuuwa vijidudu vya maradhi. Unaweza pia kuchemsha maji ya kuoga angalau kwa nyuzi joto 65 kwa muda wa dakika tano.

Maji yaliyohifadhiwa kwenye tanki kwa muda usiopungua masaa 48 ni lazima yawe salama kwa ajili ya kuogea. Kama unalima, unashauriwa kuvaa mabuti marefu ya mpira, Mtu anapaswa kumuona daktari baada ya kuwa na dalili za ugonjwa na yeye ndiye atakayemuainishia dawa za kutumia.
Ni matarajio yangu kwamba tukifuata kanuni na misingi yote hiyo ya kiafya niliyoitaja, tutashinda vita dhidi ya maradhi ya kichocho.

Ukiwa na Shida yoyote ile unaweza kunitafuta Kwa mawasiliano

Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu What's App +447459370172
 
Kanda ya ziwa kinara kwa maambukizi ya kichocho

TUESDAY , 2ND FEB , 2016
Mikoa ya Kanda ya Ziwa imetajwa kuwa na kiwango cha juu cha maambuki ya ugonwa wa kichocho yanayofikia kiasi cha asilimia 50.



kichocho.JPG

Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imeanza kutekeleza mpango wake wa kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele na imepanga kutoa chanjo za magonjwa ya kichocho kwa watoto wenye umri wa kwenda shule kuanzia Februari 4 mwaka huu lengo likiwa kuwaondolea watoto wadogo hatari ya kupata ugonjwa huo.

Maambukizi ya ugonjwa wa kichocho ni makubwa zaidi katika maeneo ya kanda ya ziwa ambapo yanafikia asilimia 50 hali inayoitaka serikali kuchukua hatua za karibu zaidi kukabiiliana na ugonjwa huo katika mikoa hiyo.

Akiongea leo jijini Dar es salaam mratibu wa taifa wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele katika wizara hiyo Dkt Pendo Mwingira amesema kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo ni kikubwa katika mikoa hiyo kutokana na uwepo wa vyambo mbalimbali.

Kufuatia hali hiyo Dkt. Mwingira amesema zoezi la kutoa chanjo hiyo litahusisha watoto wenye umri wa kwenda shule pamoja na watoto ambao hawajaanza shule watapata nafasi ya kupewa chanjo hiyo kuanzia Februari 4 mwaka huu.

Dkt. Mwingira ameongeza kuwa ugonjwa huo umekuwa ukienezwa na konokono katika maeneo ya maji yaliyosimama, katika mito pamoja na katika mabonde ya mpunga na madimbwi ya maji.

chanzo: eatv
 
Jaman ndugu zangu kuna ugonjwa fulani hivi ni kwamba;

Nikiwa nakojoa nahisi maumivu makali sana kwenye njia ya mkojo. Nahisi mle ndani kuna vidonda hasa panapounganikia kibofu na uume.

Nmetumia dawa nyingi sana lakini hakuna kilichosaidia ikiwemo siproxacilin, dox, flagily, na pia nimechoma sindano 6 lkn hakuna kilichonisaidia. Naombeni msaada ndugu zangu hili tatizo ni la mda mrefu sana.

Halafu pia na misuli ya uume imelegea si-perform vizuri kitandani ni dakika 1 tu mpaka kesho.

Msaada tafadhali
 
Pole sanaa ila kwa sababu tatizo ni la mda mref nahisi linachukua mda kupona kama ulitumia dozi ya vidonge na sindano vikapooza tatizo nakushauri urudie dozi mkuu .
 
Umeishakaa maeneo ya kando mwa ziwa Victoria? Pima kichocho. Ukiwa nacho ukikojoa mwishoni mkojo unauma halafu kanatoka kachembe ka damu hapo sasaaa. Kapime kichocho
 
Hizo dawa ulipewa hospital au uliamua tu kujinunulia pharmacy? Si kila ugonjwa unatibiwa na Ciproflaxin ama flagyl. Jaribu kwenda hospitali kwanza upimwe kisawa sawa halafu upewe dawa. Maradhi mengine tunajiongezea kwa kumeza dawa kimazoea. Pole.
 
Jaman ndugu zangu kuna ugonjwa flani hiv ni kwamba
Nikiwa nakojoa nahisi maumivu makali sana kwenye njia ya mkojo. Nahisi mle ndani kunavidonda hasa panapounganikia kibofu na uume. Nmetumia dawa nyingi sana lakini hakuna kilichosaidia ikiwemo siproxacilin, dox, flagily, na pia nimechoma sindano 6 lkn hakuna kilichonisaidia. Naombeni msaada ndugu zangu hili tatizo ni la mda mrefu sana. Nisaidieni tafadhali.
Halafu pia na misuli ya uume imelegea siperfome vizuri kitandani ni dkka 1 tu mpaka kesho.
Msaada tafadhali
Kwa haraka una dalili kama za UTI lakini inaweza ikawa inepanda juu kusababisha Cystitis (maambukizi katika kibofu). Japokuwa pia kuna magonjwa mengine zaidi ya hayo yanayoweza kuleta hali kama hiyo pia including Cancer, lakini tusiombee hayo.
Unahitaji kwenda hospitali kubwa iliyo karibu yako ambapo utapimwa mkojo, damu na vipimo vya ultrasound na Xray maalum ya kuangalia njia ya mkojo.
Hatahivyo nakushauri kunywa maji mengi na kutumia kinga unapofanya mapenzi.
 
kaijage mkiza pole mkuu,
kwa dawa ya kiarabu jaribu hii:- tumia abdalasini iliyosagwa na asali safi/origino (changanya katika kiombe) unywe, uanze na vijiko 3 alfajiri na adhuhuri na usiku...siku kadhaa utaona tija.., kama hakuna dalili ya uponyi... basi sitisha tiba hiyo!!

Au mfollow MziziMkavu ktk posts zake !!
 
Fanya kipimo kinaitwa culture and sensitivity(mkojo)..

Na kama una mpenz ni bora mtibiwe wote.

Na ukipewa dose jitaidi kumaliza kbsa
 
Niliwahi kupata tatizo kama lako hilo mkuu na nikatumia dawa hizo hizo na sindano juu (gentamycine) lakini wapii. Nikaenda hospitali kubwa nikafanyiwa kipimo kikubwa zaidi cha mkojo kinaitwa urine culture ndio akaonekana bacteria anayesumbua na kutibiwa. Kwenye majibu ya kipimo pia niliorodheshewa list ya dawa ambazo haziwezi kummudu bacteria huyu (ambazo kimsingi zote nilikuwa nimeshatumia). So mkuu achana na hayo madawa kwanza yatakuua figo ni makali mno. La msingi ingia mfukoni tafuta hospitali makini yenye wataalamu makini ukafanye kipimo cha uhakika uone tatizo ni nini. Hizi hospitali zetu za nchi ya viwanda hazitibu mkuu ni vituo vya kukomaza maradhi na kusindikizana akhera tu. Kule wanafanya kazi kwa mazoea tu, mf. ukimtajia dalili hizo ye anaconclude tu ni STD anakutwanga dozi moja amazing. Unapokwenda kutibiwa kwingine usiache kumwambia Dr. historia ya matibabu yako na dawa ulizotumia. Binafsi Dr. alishangaa sana nilipomueleza historia ya matibabu yangu na akanipa kauli moja kuwa kwny tatizo langu ilitumika bunduki kuua mbu.
 
Jaman ndugu zangu kuna ugonjwa fulani hivi ni kwamba;

Nikiwa nakojoa nahisi maumivu makali sana kwenye njia ya mkojo. Nahisi mle ndani kuna vidonda hasa panapounganikia kibofu na uume.

Nmetumia dawa nyingi sana lakini hakuna kilichosaidia ikiwemo siproxacilin, dox, flagily, na pia nimechoma sindano 6 lkn hakuna kilichonisaidia. Naombeni msaada ndugu zangu hili tatizo ni la mda mrefu sana.

Halafu pia na misuli ya uume imelegea si-perform vizuri kitandani ni dakika 1 tu mpaka kesho.

Msaada tafadhali
Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo

Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo ni bakteria maambukizi katika sehemu yanjia ya mkojo. Yanapoathiri sehemu ya chini wa njia ya mkojo, maambukizi haya hujulikana kama sisititisi ndogo (maambukizi ya kibofu). Yanapoathiri sehemu ya juu ya njia ya mkojo, maambukizi haya hujulikana kama pilonifritisi (maambukizi ya figo). Dalili katika sehemu ya chini ya njia ya mkojo ni pamoja na uchungu wakati wa kukojoa na aidha kukojoa kila mara au kuhisi haja ya kukojoa (au zote). Dalili za maambukizi ya figo pia huhusisha homa na maumivu katika mwanya wa fupanyonga. Katika watu wazee na watoto wachanga, dalili haziwi wazi kila wakati. Kisababishi kikuu cha aina hizi mbili niEscherichia coli.Hata hivyo, katika matukio machache, bakteria zinginezo, virusiau kuvu zinaweza kuwa ndivyo visababishi.

Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo hutokea mara nyingi zaidi katika wanawake kuliko wanaume. Nusu ya idadi ya wanawake huambukizwa katika wakati fulani maishani mwao. Marudio hutokea mara nyingi. Vipengele visababishi vilivyo hatari ni pamoja na ngono na pia historia ya kifamilia. Maambukizi ya figo yanaweza kufuatia maambukizi ya kibofu. Maambukizi ya figo pia yanaweza kusababishwa na maambukizi ya damu. Utambuzi katika wanawake wachanga wenye afya unaweza kutazamwa kwa msingi wa dalili pekee. Utambuzi unaweza kuwa mgumu kwa watu walio na dalili zisizo wazi kwani bakteria zinaweza kuwepo hata kama mtu huyu hana maambukizi. Katika matukio yenye matatizo au ikiwa matibabu hayajafaulu, uchunguzi wa vimelea katika mkojo wakati mwingine husaidia. Mtu aliye na maambukizi ya kila mara anaweza kutumia kipimo kidogo cha antibiotikikama namna ya kuzuia.

Matukio madogo ya maambukizi katika mfumo wa viungo vya mkojo hutibiwa kwa urahisi kwa kutumia mfululizo wa antibiotiki. Hata hivyoupinzani dhidi ya antibiotiki zinazotumika kutibu hali hii, unaendelea kuongezeka. Watu walio na matukio yenye matatizo, wakati mwingine hushurutika kutumia antibiotiki kwa muda mrefu zaidi au watumie antibiotiki zinazodungwa ndani ya misuli. Ikiwa dalili hazipungui baada ya siku mbili au tatu, mtu atahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi. Katika wanawake, maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo ndiyo maambukizi yanayotokea mara nyingi zaidi katika aina zote za maambukizi ya bakteria. Asilimia kumi ya wanawake hupata maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo kila mwaka.



Dalili na ishara

Maambukizi ya sehemu ya chini ya mfumo wa viungo vya mkojo pia hujulikana kama maambukizi ya kibofu. Dalili zinzotokea mara nyingi zaidi ni hisia za kuchomeka wakati wa kukojoana kukojoa kila mara (au kuhisi kukojoa) bila mchozo wa uke na maumivu mengi.[1] Dalili hizi zinaweza kutofautiana kutoka dalili zisizo kali hadi dalili kali[2]. Katika wanawake wenye afya njema, dalili hizi hudumu kwa wastani wa siku sita . [3] Baadhi ya watu huwa na maumivu juu ya mfupa wa kinene au kwenye maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo. Watu walio na maambukizi katika sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo au pilonifritisi (maambukizi ya figo), wanaweza kuwa na maumivu katika maumivu ya fupanyonga, homa au kichefuchefu na kutapika. Dalili hizi huambatana na kikundi cha dalili za maambukizi ya upande wa chini cha mfumo wa viungo vya mkojo.[2] Mkojo huwa na damu mara nadra sana[4] au kuwa na piuria (usaha katika mkojo)

Nenda kapime hospitali utumie dawa usipo pona nitafute nipate kukutibia.Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr.MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App +447459370172
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom