Ujue mbuyu wenye miaka zaidi ya 500, unaoweza kubadili jinsia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Makumbusho ya Kaole, Bagamoyo yana mti aina ya mbuyu wenye miaka zaidi ya 500.

Mbali na kuwa na umri mkubwa, mti huu unaambatana na imani ambazo zilikuwa za watu wa eneo hilo.

Mti huu unasadikiwa kuwa unapozungukwa kushoto kwenda kulia mtu anaongeza umri wa kuishi na vinginevyo anapunguza umri wa kuishi.

Pia ukizungukwa zaidi ya mara saba hubadili jinsia, ambapo inasemekana kama mtu ni mwanaume anaanza kuwa na tabia za kike na wa kike anaweza kuwa na tabia za kiume.

IMG_20201220_101747_098.jpg
 
Uongo, hata kama umechoka kuishi na unataka kujiondokea zake, bado wapo wanadamu wako tayari kuufunga minyororo ya chuma ili waendelee kubaki nao na kuutumia.
 
Mimi na Crew yangu tulifika hilo eneo tukapata habari zake, tukauzunguka mti huo mara 7, ilikua for fun hakuna mtu aliweka imani ya kinachoelezwa,

Pia kuna kisima hapo hapo Kaole wanasema kipo tangu karne ya mbali huko hakikauki maji pia hakina chumvi licha ya kua karibu na bahari, watu wana nawa na wengine wanakunywa maji yake kwa ajili ya kupata baraka.
 
Makumbusho ya Kaole, Bagamoyo yana mti aina ya mbuyu wenye miaka zaidi ya 500.

Mbali na kuwa na umri mkubwa, mti huu unaambatana na imani ambazo zilikuwa za watu wa eneo hilo.

Mti huu unasadikiwa kuwa unapozungukwa kushoto kwenda kulia mtu anaongeza umri wa kuishi na vinginevyo anapunguza umri wa kuishi.

Pia ukizungukwa zaidi ya mara saba hubadili jinsia, ambapo inasemekana kama mtu ni mwanaume anaanza kuwa na tabia za kike na wa kike anaweza kuwa na tabia za kiume.

View attachment 1654983
Ngoja niwahi siti
 
Mkuu mleta mada, tumia akili ndogo tu- mchukue jamaa hapo mwambie una shs 10,000 utampa kama atauzunguka mbuyu mara 10.

Naamini utapata watu wengi sana wa kuuzunguka, Sasa utaamua uongeze bajeti kutokana na wingi wa watu ama utafiti utaishia hapo!!!
 
Nilifika hapo miaka 2 iliyopita. Mwongoza watalii alitueleza kuwa huo mbuyu kweli una miaka mingi kama ulivyosema.

Inasemekana miaka hiyo ya nyuma, eneo linalozunguka huo mbuyu, watu wakiamka asubuhi wanakuta eneo ni safi, bila kuona anayesafisha ni nani.

Wakati huo bado kuna makazi ya watu, ilikuwa inaaminika kuwa ukiuzunguka mbuyu huo mara kadhaa, basi unaongeza umri wako wa kuishi. Hii ya kubadili jinsia....mpya.
 
Mimi na Crew yangu tulifika hilo eneo tukapata habari zake, tukauzunguka mti huo mara 7, ilikua for fun hakuna mtu aliweka imani ya kinachoelezwa,

Pia kuna kisima hapo hapo Kaole wanasema kipo tangu karne ya mbali huko hakikauki maji pia hakina chumvi licha ya kua karibu na bahari, watu wana nawa na wengine wanakunywa maji yake kwa ajili ya kupata baraka.
Oooooh kumbe babeeh ulienda? Why hukunichukua na mie?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom