Ujio wa viwanda Tanzania NEMC mmejipanga?

Danken Mbombo

JF-Expert Member
May 30, 2015
651
339
Katika serikali hii ya awamu ya 5 Tanzania inaenda kuwa ya viwanda. Viwanda vinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu mazingira. Kama NEMC mmejipanga mnatakiwa kuchukua hatua za kutoa ushauri wa kitaalamu kabla ya ujenzi wa kiwanda chochote kwa lengo la kudhibiti au kuzuia uharibifu wa mazingira.

Msikae tu maofisini kusubiri taarifa ndipo mwende kutoza faini. Na inapotokea mnatoza faini basi kiwango cha faini kizingatie athari walizopata wananchi, aidha pesa inayotokana na faini, asilimia fulani ikahudumie walioathirika na uchafuzi wa mazingira.

Endapo NEMC mtalala unsingizi kipindi hiki yanaweza yakatufika kama ya China ambapo katika baadhi ya miji yao watu wanalazimika kutembea barabarani wakiwa wamevaa 'mask' za kufunika pua na midomo sababu halli ya hewa imechafuliwa na viwanda. Chonde chonde NEMC msitufikishe huko fanyeni kazi yenu kwa weledi
 
Back
Top Bottom