NEMC, Wizara ya Muungano na Mazingira ni wazi wameshindwa kudhiti uharibifu wa mazingira

Jorowe

Member
Jun 9, 2018
85
194
Kama umezaliwa kijijini kuanzia miaka ya 90 kurudi nyuma hebu jaribu kuvuta picha ya mazingira nyuma(mito, milima, mapori) jinsi yalivyokuwa then linganisha na leo ndio utaweza kukielewa ninachoenda kuzungumzia.

Nimezunguka sehemu nyingi za nchi hii kutoka kaskazini, mpaka kusini kanda ya kati mpaka lake zone, Hakika mazingira yanaharibiwa tena sio kidogo ni kwa kasi ya kutisha!

Nimekaa nikawaza sana kazi ya hii Wizara ya Muungano na Mazingira pamoja na NEMC ina maana hamuyaoni haya yanaoendelea?! Je baada ya miaka 30 au 50 mbele hii nchi si itakuwa jangwa!

Miaka 25 iliyopita iliyokuwa mito inaogopeka hata kuisogelea leo hii zimeshageuka kuwa Makorongo sio mito tena ule uoto wake haupo tena yaani ukiambiwa huu ulikuwa mto wenye uoto wa asili wa kutisha ni ngumu kuelewa!

Miaka 25 iliyopita sehemu zilizokuwa chemichimi au tepetepe kwa ajili ya kilimo cha miwa leo hii hata ukipanda viazi unaweza kuhitaji uvimwagilie maana pameshakuwa ardhi kame!

Mapori tengefu yamebakiza vichaka tu pamoja na nyasi hakuna tena miti, Watu wanajenga holela hadi kwenye vyanzo vya maji tena wakiwa na kibali halali kilichopitishwa na wahusika.

Tumebaki kuwasumbuwa wenye viwanda kwa faini kandamizi huku nchi ikigeuka JANGWA kwa kasi ya kutisha,

Inachekesha waziri anaona plastiki zilizoko kwenye mfuniko wa maji ni hatari kuliko miti inavyoteketea
Ukianzisha hata ka kiwanda kwa kuoka mikate unaona watu wa mazingira hawa hapa hadi unawaza hivi mazingira yanahusiana na viwanda tu

Kwa wenzetu wazungu unaweza kutembea hata zaidi ya 20km hapo ni ndani ya mji ukiwa ndani ya vivuli vya miti iliyopandwa barabarani huku kwetu serikali haina habari!

Kwanini serikali isianzishe mpango mkakati miji yote iwe ya kijani hata kama ni kwa kutumia nguvu kubwa ili kuyanusuru mazingira?!

NEMC Jafo na Wizara yako ya Muungano na Mazingira amkeni Vizazi vijavyo kuna hatari ya kuja kurithi Jangwa!
 
Tatizo ni siasa

Serikali ikikaza, wapinzani na wanasiasa wanapata platform ya kuropoka.
Serikali imeamua tuumie sote
 
Sizani mkuu kama hata inahitajika nguvu sana hadi kuwafanya wapinzani waropoke!

Hivi mfano walazimishe kila mwenye frame ya duka awe na mti mbele yake hapo ni kukaza?!

Au kila mkandarasi anayejenga barabarani atenge na na bajeti ya miti kwa pembeni na yenyewe kwani inahitajika nguvu?!

Kutolima kwenye mito na vyanzo vya maji wakiwatumia mabalozi wa nyumba kumi na wenyeviti wa vitongoji kwani hata inahitaji nguvu?!

Shida ni kwamba wameshindwa kuzuia kwenye kiini cha tatizo wanahangaika na matokeo ndio maana badala ya kumwajibisha anayekata mti wanahangaika na anayeubeba mkaa
 
Back
Top Bottom