Ujio wa Obama: Wachuuzi wafurushwa posta

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,438
4,454
Katika kile kinachoonekana kuwa ni maandalizi ya Rais Obama, leo askari wa Manispaa ya Ilala, Jiji la Dar es Salaam wameshiriki kuwaondoa wachuuzi wengi kando kando ya barabara. Eneo la Posta Mpya na Posta ya Zamani na maeneo mengi jirani, hali ni tofauti kabisa.

Shaka yangu ni kwamba mambo haya yanapofanywa kwa ajili ya wageni, yanakuwa hayana maana sana kwani mwisho wa siku yataibua vurugu kutokana na wachuuzi wengi kuona wamechwa wawepo hapo siku nyingi, na kwa hiyo wana haki ya kuwapo.
 
Hii ndo ile serikali dhaifu ya kujikomba.Serikali isiyofikiri na kutenda sawasawa.
 
Kwani bado ana ratiba ya kuja? Mbona kuna siku magazeti yaliandika kuwa ikulu ya marekani imefuta ziara ya Obama Tizii?
 
Nchi hii kwa vibweka, pale Ubungo waliwaondoa sababu ya usalama wao kutokana na kufanya biashara chini ya H.T ya Tanesco, na kwamba wanaongeza msongamano barabarani kwa biashara zao kufanyiwa kandokando ya barabarani.Sasa wamerudi wala hawana wasiwasi.
 
Hali leo ktk jiji la dar si nzuri baada ya polisi kwa kushirikiana na wagambo kuwaondoa wauza magazeti wote na shoe shine katikat ya jiji kwa madai kwamba wanachafua jiji tangu asubuh hakuna kusoma gazeti wala kung'arisha viatu
 
Amri imetolewa jiji liwe safi so wauza magazeti na wapiga kiwi hawatakiwi source chanel ten habari
 
Amri imetolewa jiji liwe safi so wauza magazeti na wapiga kiwi hawatakiwi source chanel ten habari

watanzania wenzangu tuwe makini,na huo ujinga unafanywa na viongozi wetu wa kutofikiria.
 
haya maamuzi ni kama ya Idd Amin wa Uganda alivyowamwaga omba omba na walemavu mto Nile ili kusafisha jiji la Kampala,kupokea ujio wa Queen Elizabeth.
 
Wangezuia kazi ya aina yeyote isifanyike au ndio ubaguzi,haya nyie wenye kazi zinazoeleweka na zenye mapato kwa taifa endeleeni.
 
haya maamuzi ni kama ya Idd Amin wa Uganda alivyowamwaga omba omba na walemavu mto Nile ili kusafisha jiji la Kampala,kupokea ujio wa Queen Elizabeth.

kwa hali hii lazima nchi iendelee kuchafuka,nitapigana kufa ili kizazi kijacho kiwe na mwelekeo mzuri
 
haya maamuzi ni kama ya Idd Amin wa Uganda alivyowamwaga omba omba na walemavu mto Nile ili kusafisha jiji la Kampala,kupokea ujio wa Queen Elizabeth.

kwa hali hii lazima nchi iendelee kuchafuka,nitapambana kufa ili kizazi kijacho kiwe na mwelekeo mzuri
 
Amri imetolewa jiji liwe safi so wauza magazeti na wapiga kiwi hawatakiwi source chanel ten habari


Kwa hiyo wauza magazeti na shoe shines watakula wapi siku zote Obama atakapokuwepo hapa nchini. Hebu mnaotoa hizi amri jaribuni kushirikisha ubongo wakati wa kufikiri.
 
Mji lazima uwe safi,kipindi cha Obama hawa watakuwa ni uchafu na baada ya Obama hawa ni wajasiliamari
 
Nimepata taarifa na pia nimeona askari polisi na askari kanzu wakikimbizana na vijana maeneo ya Stesheni na pia Mnazi mmoja. Polisi wnakamata wazururaji, wakikukuta wanakuuliza una shughuli gan sehemu hiyo? kama huna ishu ya muhimu wanakukamata na kukupeleka kituoni.

Pia wanawachukua omba omba wote huko mabarabarani na tetesi ni kwamba wanawauliza walipotoka na kuwarudisha huko mikoani. ni tafrania mjini, wapiga debe na watu wa kuzuga hapa mjini stend hapatoshi.

Nachojiuliza na pia ningependa hao waliotoa hilo agizo waelewe si mara ya kwanza kufanya hivyo ila mbona mambo haya yanajirudia?...kipindi cha nyuma kidogo ilikuwa ni marufuku kuzurura hovyo bila shughuli maalum sasa sijui sheria hiyo iliisha makali yake lini. Pia Mh. Kandoro kipindi akiwa mkuu wa mkoa Dar aliwaondoa omba omba ila walirudi na wapo had saiv.

Mimi ningependa watengeneze mpango mkakati wa kueleweka kuhusu hawa omba omba hususani wasio na dis-abilities, wangewapa hata mafunzo ya ufundi stadi ndio wawarudishe makwao! La sivyo watarudi tena. Pia wizara ya jinsia na watoto iandae sera za hao watoto wa mtaani, wawatengenezee makazi bora na pia wapate elimu. kuwaacha hivyo na kuwarudisha kwao sio suluhu ya kudumu.

Na tetesi ni kwamab wanasafisha mji kwa kuwaondoa hao omba omba na wazururaji mjin kisa anakuja Rais wa ile dola kubwa duniani! kama ni kweli mambo haya ni fedheha kubwa, siku zote hawa viongozi wetu wanawaona hawa omba omba wengine na watoo wachanga kabisa ila wanafumba macho kama hawawaoni vile! Leo kisa kuna ugeni ndio wanaanza kuwaondoa!!

Tanzania tubadilike tusiwe na plan za kukurupuka tuu, tuwe na mipango mkakati ya muda mrefu na sera nzuri si za kimaandishi na midomoni tu bali zinazokuwa na utekelezaji kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
 
Nimejiuliza sijapata jibu,polisi wamekuja mpaka maeneo ya TRA longroom,wanaumuuliza
mlinzi kama kuna watu humo ndani hawana kazi waje wawachukue,huku wamewachukua
watu kibao eti wamewakuta mitaa ya Samora na Stesheni wamesimama wanawake kwa
wanaume,eti watakwenda kujieleza kituoni.Leo nimeconclude kuwa polisi lazima uwe either
ulifeli mitihani au umekosa kazi nyingine ya kufanya'
 
hayo ni maandaliz ya rais wa nchi ile nahisi coz toka jana pale posta vijana waliwasulubu na wakaambiwa wasiweke biashara pembezoni,
 
Back
Top Bottom