Ujio mpya unanipa kiwewe

Ujio mpya unanipa kiwewe

grandMullah23m

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2017
Posts
248
Reaction score
339
Wakulungwa...Kwa Nia njema tu,

naombeni jinsi ya kukabililana na stress za mama kijacho maana naona Sasa kama kamtu kana maksudi.

Uzalendo unakuwa mgumu ndio kwanza mwezi wa tatu[emoji119]
 
Uko Gongo la Mboto, unaagizwa chips za kwa mpemba wa Kimara Bonyokwa!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Usipokua kauzu utazifuata kweli.
Ukizifuata ukirudi anasema sili mbona umechelewa sana
 
Acha kufanya mambo yanayomzingua
 
Omba asipatwe na hamu ya kunusa moshi wa gari maana atahitaji kukaa stendi ya Makumbusho asubuhi hadi jioni
 
Uko Gongo la Mboto, unaagizwa chips za kwa mpemba wa Kimara Bonyokwa!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Usipokua kauzu utazifuata kweli.

[emoji23][emoji23]hivi mnajua craving zilivyo wazee??
Hatufanyi kusudi mjue
 
Wakulungwa...Kwa Nia njema tu,

naombeni jinsi ya kukabililana na stress za mama kijacho maana naona Sasa kama kamtu kana maksudi.

Uzalendo unakuwa mgumu ndio kwanza mwezi wa tatu[emoji119]

Hafanyi kusudi bhana(naamini hivyo).
Fanya kumvumilia maana ni kipindi cha mpito,yatapita tu
 
[emoji23][emoji23]hivi mnajua craving zilivyo wazee??
Hatufanyi kusudi mjue
Ni makusudi matupu. Ukiniambia eti uko na hamu ya kunusa moshi wa gari, itabidi tu nikutoe wenge hata kwa makofi mawili.

What kind of craving is that?
 
Unaamua kuzitafuna mwenyewe kwa hasira. Ukimaliza anaanza kulia, anataka chips zake!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Unaamua Kwenda tena kwa Mpemba Bonyokwa kufuata Chipsi zake mara paap saa nane usiku,anakwambia mbona Asubuhi ishafika nataka Chai...!
 
Anadeka tuu na kwa kuwa wa kudekea yupo,,,mbona mahausi geli hawanaga hizo mbanga!!wakiwa wajawazito!!
 
[emoji23][emoji23]hivi mnajua craving zilivyo wazee??
Hatufanyi kusudi mjue
Hawajui tuu hawa yaani mpaka unahisi kuumwa ukikikosa unachotamani. Nishawahi tamani nyama usiku ikabidi mdogo wangu achinje kuku saa 5 usiku nikapika ile kuonja tuu nilijisikia raha kama nimeona ufalme wa mbingu.
 
Back
Top Bottom