Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,161
- 48,426
Mtu mjinga siku zote ni mtaji wa mtu mwerevu. Na siku zote watu laghai na waovu huzuia watu wajinga wasierevushwe maana huo ndiyo utakuwa msiba wao.
CCM tangu baada uchaguzi wa mwaka 2000, imekuwa ikitumia ujinga wa baadhi ya watanzania kuendelea kubaki madarakani.
Hebu ona mjinga anavyomlaumu mtu aliyeuawa ama kuteswa kwa kuwa tu anaipinga CCM. Kuna kosa gani kuipinga CCM?
Angalia mjinga mwingine asiyejua kutofautisha kati ya majengo ya shule na shule. Shule yenye wanafunzi kuanzia darasa la kwanza mpaka la Saba inawezaje kuwa na walimu hawafiki hata kumi?
Huyu mjinga mwingine aliyekuwa anasema kwa nini CHADEMA haitumii ruzuku yake kujengea zahanati leo yupo kimya haulizi swali hilo hilo kwa CCM.
Kuna mjinga anayewaza mtu kusoma si lazima aajiriwe. Sasa kwa nini mtu asome kwa zaidi ya miaka 15 au 20 halafu asipewe ajira? Kazi ya Serikali ni nini?
Sasa naelewa ni kwa nini Mwalimu Nyerere aliuweka Ujinga kuwa miongoni mwa wale maadui zetu watatu yaani Ujinga, maradhi na umaskini.