Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Ujerumani yashangazwa kutoendelezwa Reli ya Kati
Na Mashaka Mgeta
Serikali ya ujerumani imesema ni aibu kwa Tanzania kuiacha reli ya kati inayoendeshwa na Shirika la Reli nchini (TRL) kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
Ujerumani ni Taifa lililojenga reli ya kati wakati wa utawala wa kikoloni na kutoa msaada wa matengenezo yake nyakati tofauti.
Balozi wa Ujerumani nchini, Guido Herz, alisema hayo juzi katika mahojiano maalum na magazeti yanayochapishwa na The Guardian Limited, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Alikuwa akizungumzia maandalizi ya adhimisho la miaka 20 tangu Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi zilipoungana rasmi Oktoba 1990 na kuruhusu kuvunjwa kwa Ukuta wa Berlin.
Herz alisema hali ya reli hiyo hivi sasa inasikitisha licha ya kuwa katika mazingira bora ya kibiashara kwa kuhudumia abiria na mizigo upande wa Tanzania na nchi jirani.
Amesema Ujerumani haiwezi kutoa msaada wa kuikarabati reli ya kati, inayosimamiwa na Kampuni ya Reli nchini (TRL).
Hatupo tayari kuisaidia reli ya kati hata kama serikali serikali ya Tanzania itatuomba kufanya hivyo, kwa sababu reli kwa sasa haifanyi kazi, alisema.
Herz alisema kama pangekuwa na utawala mzuri, utoaji wea huduma wa reli hiyo usingeibua mazingira yaliyosababisha ishindwe kufanya kazi.
Alisema reli ya kati ni miongoni mwa fursa kubwa za kiuchumi nchini, na akaonyesha mshangao wake kwa nini serikali imeshindwa kuifufua na kuiboresha ili ifanye kazi kwa ufanisi ..
Habari zaidi katika Nipashe leo Ukurasa wa 3.
My take:
1. Kwenye red: Balozi anajua ni ufiisadi tu uiliokithiri ndani ya CCM, ila hakutaka tu kumuumbua JK wakati huu. Dr Slaa akifika Tabora na Kigoma aliongelee sana sana hili, hadi masikio ya mashabiki wa JK yapasuke.
2. Ingekuwa ndiyo Dr Slaa kayasema haya, Kinana angejibu kwamba anatafuta umaarufu. Siyo kweli Kinana?