Mchakachuliwaji
Member
- Nov 23, 2010
- 31
- 0
Mkuu Ghorofa sio sana Tofali, Tofali ni nyama za kujazia tu, bali ghorofa ni ZEGE, (Nondo, Cement /Mchanga/Kokoto(ratio nzuri) ), Ningekushauri umtafute mtaalamu wa Soil kwanza aangalie hilo eneo lako (aina ya udongo, mfinyanzi, mchanga nk) na pia aangalie hilo eneo ni kavu ama ni eneo yowevu, ukishapata hayo majibu mtafute mtaalamu wa ujenzi akushauri utumie Nondo za milimeter ngapi kwenye Msingi, Colum na jamvi lenyewe,
badala ya kuvyetua tofali ningekushauri uanze kukusanya Nondo, kokoto, Mchanga na weka pesa ya cement, Tofali wala sio kitu cha kuumiza kichwa kama unajenga ghorofa
Kwanza hongera for progressive ideas but at each step of your undertaking "consult reliable people in the field". Najua utahitaji beams na nondo zenye ubora siyo zile za chuma recycled la sivyo zitapinda. Asante nadhani wataalamu tunao hap JF watakupa nyeti zote
Mkuu hapo umenikuna lugha uliyoitumia kwenye red uko BAKITA??hebu tudadafulie neno YOWEVU!Mkuu Ghorofa sio sana Tofali, Tofali ni nyama za kujazia tu, bali ghorofa ni ZEGE, (Nondo, Cement /Mchanga/Kokoto(ratio nzuri) ), Ningekushauri umtafute mtaalamu wa Soil kwanza aangalie hilo eneo lako (aina ya udongo, mfinyanzi, mchanga nk) na pia aangalie hilo eneo ni kavu ama ni eneo yowevu, ukishapata hayo majibu mtafute mtaalamu wa ujenzi akushauri utumie Nondo za milimeter ngapi kwenye Msingi, Colum na jamvi lenyewe,
badala ya kuvyetua tofali ningekushauri uanze kukusanya Nondo, kokoto, Mchanga na weka pesa ya cement, Tofali wala sio kitu cha kuumiza kichwa kama unajenga ghorofa