Ujenzi wa Soko kuu Mwanza

Ujenzi wa Soko kuu Mwanza

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Wananchi wa Jiji la mwanza walifurahi sana walipoona Soko la zamani likivunjwa kupisha ujenzi wa soko mpya. Soko lilipovunjwa wafanyabiashara walisambaa maeneo mbalimbali ili wapate nafasi ya kuendelea na biashara zao.

Kibaya zaidi maeneo waliopelekwa ni maeneo hatarishi na hakuna huduma za kijamii kama vyoo. Wanapanga bidhaa zao chini kwenye maeneo machafu kabisa na hii huhatarisha afya za walaji.

Linalosikitisha sasa ni barabara ya Nyerere. Nusu ya barabara imevamiwa yaani wafanyabisahara wanapanga bidhaa zao kama mihogo, michicha, nyanya, viazi n.k barabarani, Serikali inawaona na iko kimya. Jana nilishuhudia gari kubwa la Scania lilitaka kuvamia wafanyabiashara hawa liliposhindwa kugeuza kwenye kona.

Jamani hivi tuna uongozi wa Jiji?. Mambo ni hovyo kabisa. Kila mtu anajichukulia mamlaka yake. Hapana, hapana nchi haiendeshwi hivyo. Tunatakiwa tufuate sheria, kanuni na taratibu.

Mbaya zaidi ni ujenzi wa soko kuu kutoendelea. Sasa ni muda mrefu hakuna kinachoendelea. Kama Serikali ilijua hivyo kwa nini sasa ilivunja Soko Kuu. Sasa hivi wananchi wanateseka sana kwa kukosa eneo la kununulia bidhaa zao. naishauri Serikali iwe maakini sana na uamuzi wowote kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.
 
Lengo lako unataka waondolewe hao waliopanga barabarani? Au lengo lako soko liendelee kujengwa? Ni kweli serikali muda mwingine huwa inakurupuka toka wafukuzwe mle sioni hata kinachoendelea, watasingizia Corona.
 
Naunga mkono hoja...kama walijua watastuck wangeahirisha tu wakajenga next time.. Naona ilemela mradi wao wa stendi unaendelea,nyamagana sijui wanakwama wapi.
 
Back
Top Bottom