Musoma Vijijini Waamua Kujenga "David Massamba Memorial Secondary School"

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,916
946

MUSOMA VIJIJINI WAAMUA KUJENGA, "DAVID MASSAMBA MEMORIAL SECONDARY SCHOOL"

Leo, Jumatano, tarehe 30.8.2023 ilikuwa siku ya maziko ya Gwinji la Lugha ya Kiswahili, Prof David Massamba nyumbani kwake Kijijini Kurwaki, Musoma Vijijini.

Wataalamu wenzake wa lugha ya Kiswahili, wakiwemo wanafunzi wake wanasema Marehemu alikuwa Gwinji na Mbobezi kwenye eneo la, "Fonolojia ya Kibantu" - hayupo mwingine tena wa kariba yake!

Musoma Vijijini wameamua kumuenzi Marehemu Prof David Massamba kwa kujenga sekondari mpya kijijini kwao itakayopewa jina lake na kuitwa, "David Massamba Memorial Secondary School." Ujenzi unaanza mwezi ujao, Septemba 2023.

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa. Hii ilikuwa sehemu ya matukio ya leo kwenye maziko ya Prof David Massamba.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 30.8.2023
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-08-30 at 23.47.11.mp4
    27.9 MB
Back
Top Bottom