Ujenzi wa plant ya madini ya dhahabu inaweza kugarimu shilling ngapi hasa kwa kiwanda cha kati?

David kagenzi

Member
Nov 20, 2023
11
14
Jamani naomba kuuliza kuhusu ujenzi wa plant ya madini ya dhahabu inaweza kugarimu shilling ngapi hasa kwa kiwanda cha kati au hata kikubwa.
 
Jamani naomba kuuliza kuhusu ujenzi wa plant ya madini ya dhahabu inaweza kugarimu shilling ngapu hasa kwa kiwanda cha kati au hata kikubwa.
Kiwanda cha kat almost million 300 mkuu kikubwa watafte Acacia wakupe consultation. Ila kwa kuanzia hata million 15 inawez fanya jambo

mrangi
 
Ujenzi wa plant ya madini inategemeana, ila Cha kwanza kabisa ni eneo unalotaka kujenga hiyo plant yako, Cha pili ni ukubwa wa sehemu ya kuweka kapi yako, halafu Cha tatu ni ukubwa wa hizo tank zako, unataka ziwe ngapi na pia columu yako iweje jitahid sana usiwe karibu na makazi ya watu ili kuepuka migogoro, Pia eneo lako kuwepo na uhakika wa kupata maji ya ya uhakika mtaji wako uweke kati ya million 25, 30 au 40 kutegemeana na wewe mwenyewe unavyotaka kuwekeza
 
Fafanua kidogo...
Kiwanda cha Dhahabu kinafanyaje?
Unaweka mchanga wanasafisha au?
Kwa maelezo ya kawaida tu hivi ni viwanda vidogo vidogo ambayo huwa vinatumika katika uchejuaji wa madini hasa dhahabu hasa ukiwa na mzingo ama lundo kubwa la mchanga kama fuso 30, hivyo plant inatumika kuvuna dhahabu inayopatikana kwenye huo mchanga kwa kutumia process ya cyanide na madawa mengine, hyo ni kifupi tu mkuu japo ni elimu Pana Kiasi
 
Je kama mnayo hiyo plant napataje huo mchanga?
Au ndo wanaochimba wanakuja kuleta?mnagawana vipi hiyo Dhahabu?
 
Je kama mnayo hiyo plant napataje huo mchanga?
Au ndo wanaochimba wanakuja kuleta?mnagawana vipi hiyo Dhahabu?
Mkuu Suala la plant ni kama vile wewe uwe na kiwanda Cha kuchejua madini na kazi Yako wewe unakodisha kwa watu wenye huo mchanga, lundo au makinikia ko we unakuwa unafanya biashara na wao kwa kukodisha kwa watu, na inategemeana na kazi mara nyingi huwa ni wiki mbili mpaka mwezi, mchanga unapatikana kwa kuchimba duarani na ile dhahabu inayopatikana baada ya process yote huwa ni kwao siyo yako maaana wewe unakuwa umeisha lipwa hela yako ya kukodisha plant yako, kwako wanaleta mchanga kwa ajili ya kuchenjua tuu baada ya kuuchimba
 
Kwanini uikimbie?
Kwa sababu huna hela(mtaji) ya kuwapa watu wa kukusanyia lundo,na ukizingatia faida ako ni riba ya hela ulizowapa,Kodi ya kuwakodishia plant wakati wa kuozesha na kapi.

Nakazia siyo tu ujenge plant uwe pia na MTAJi tofauti na apo utakua umejenga majengo ya kujikingia mvua wachunga ng'ombe.
 
Mtaji kama kiasi gani unatosha ?
 
Back
Top Bottom