Ujenzi wa leo na matumizi sahihi ya milango

Ujenzi wa leo na matumizi sahihi ya milango

Dafugwadu

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
4,733
Reaction score
5,251
Jf kwa wakubwa na wadogo salaam. Jambo moja ambalo nimelishuhudia vya kutosha ni hili ambalo naomba niwashirikishe halafu tuchambue kwa pamoja.
Ni kuhusu nyumba nyingi sana zilizojengwa kisasa ni kwa nini ule mlango mkubwa ambao ndio unatumika kuingilia Sebuleni huwa hautumiki badala yake unatumika ule mlango wa kuingilia jikoni kisha ndio uende tena Sebuleni!? Yaani pamoja na mbwembwe zote za urembo wa barazani lakini hapapitiki hata dada wa kazi akideki lazima azunguke hata makufuli yanayofungia yale magrill unaweza kuta yana kutu kwa nini huu mlango hautumiki? Ilikuwa na haja gani ya kuuweka sasa!
Hebu tusaidiane kuwazuwa nione kama kuna wenye mawazo kama yangu.
 
mimi niliuliza mtu akanijibu ni mambo ya kishirikina.ila nyumba kubwa za wazito ni nadra kukutana na hii.
 
Mlango wa dharula eti unatumika kukiwa na shughuli maalumu kama msiba,harusi au ugeni wowote mkubwa..
Kwa kawaida ule mlango unakuwa ni mkubwa watu wanaona uvivu kuutumia ule wakati mdogo upo
Kingine ni kwa ajili ya usalama ule mlango upo jirani na sebule kuufungua fungua unakaribisha wezi kingine mtu akiwa jikoni anapika hawezi kuskia mtu akiingia sebuleni na nyumba nyingi watu wengi wanaoshinda nyumbani hukaa jikoni kwa mida mrefu..husaidia kumuona au kuskia mtu anaeingia sebuleni
 
mimi niliuliza mtu akanijibu ni mambo ya kishirikina.ila nyumba kubwa za wazito ni nadra kukutana na hii.
Siyo za wazito to ata watu wakawaida wanatumia mlango wa seblem,malanyingi ukiona mlango wa kuingilia sebleni au tumiki wengi wao uwa wamepanga siyo wenye nyumba.
 
Jf kwa wakubwa na wadogo salaam. Jambo moja ambalo nimelishuhudia vya kutosha ni hili ambalo naomba niwashirikishe halafu tuchambue kwa pamoja.
Ni kuhusu nyumba nyingi sana zilizojengwa kisasa ni kwa nini ule mlango mkubwa ambao ndio unatumika kuingilia Sebuleni huwa hautumiki badala yake unatumika ule mlango wa kuingilia jikoni kisha ndio uende tena Sebuleni!? Yaani pamoja na mbwembwe zote za urembo wa barazani lakini hapapitiki hata dada wa kazi akideki lazima azunguke hata makufuli yanayofungia yale magrill unaweza kuta yana kutu kwa nini huu mlango hautumiki? Ilikuwa na haja gani ya kuuweka sasa!
Hebu tusaidiane kuwazuwa nione kama kuna wenye mawazo kama yangu.
Labda wewe mkuu
 
Kuna kitu cha ziada ambacho wengi mnakisahau.

Mara nyingi nyumbani huwa hakuna baba, mama, mtoto mwenye nyumba ambaye anashinda nyumbani mathalani sebureni, inapotokea wote hawapo binti anafanya kazi zote akiwa jikoni na uwani.

Pale mnaporudi mnajua kuwa mtamkuta uwani hama jikoni akifanya kazi za home, hali hiyo imepelekea kuzoeleka kwa jamii.

Hakuna cha uchawi, udambwidambwi wala ulozi.
Na....
 
Kwa nilivyowaza mimi kuhusu ‘mlango wa nyuma’ aisee mnisamehe.... eti siku hizi unatumika sana..!!
 
Mwandishi uwe unafafanua vzur...
Hapa nachokiona Mimi hujamaanisha mlango tunaoufikiria sisi... Na wengi watafeli kujua ulichomaanisha...ila nimependa sana uwezo wako wa kuficha Lengo lako.. Na Umelenga majibu kutoka Kwa watu wazima.. Ila watoto Watajibu mlango hautumiki kisa hausigeli.. Hahaaaaa..

Mi majibu yangu ni kuwa tumrudie Mungu atuepushe na laana Hiyo.
 
home ule mlango mkubwa nna uwakika hatujawahi tumia zaidi ya mara 10, sababu kubwa zaidi niza kiusalama, mazoea pia mkubwa kulinganisha na wajikoni.
 
Mwandishi uwe unafafanua vzur...
Hapa nachokiona Mimi hujamaanisha mlango tunaoufikiria sisi... Na wengi watafeli kujua ulichomaanisha...ila nimependa sana uwezo wako wa kuficha Lengo lako.. Na Umelenga majibu kutoka Kwa watu wazima.. Ila watoto Watajibu mlango hautumiki kisa hausigeli.. Hahaaaaa..
Mi majibu yangu ni kuwa tumrudie Mungu atuepushe na laana Hiyo.
Hapana ni mlango wa nyumba na sio ule mlango ambao binadamu anapita mara moja tu katika maisha yake yote.
 
Back
Top Bottom