Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa wilaya ya Chato mkoani Geita

Mheshimiwa "raisi" wetu ni noma. Hiyo hospital ya rufaa ya Chato ikikamilika itaweka record kwa kanda ya ziwa. Maana ukiacha Dar ambako hata Amana nayo ni hospital ya rufaa basi wilaya ya Chato ndiyo pekee nchini isiyo na hadhi ya makao makuu ya mkoa itakayo kuwa na hospital ya rufaa.

Namwomba raisi akikamilisha CIA na hii hospital basi ajenge na mwendokasi kabisa Chato maana taa za barabarani tayari zipo na pia aboreshe bandari ya Chato iwe kubwa kuliko zote kanda ya ziwa.

It's our turn to eat! Read me between the lines!:)
Kuna ubaya?
 
Nadhani hapa amekuonyesha kuwa issue ni uwiano in population, je kwa hizo mbili zinazohidumia 4m na zile 13 ambazo moja ni ya Rufaa ya Kanda na hizo zingine za Mkoa nawilaya na zinazohidumia 1.8m kuna makosa gani kule kwenye population kubwa zikiongezwa


Hizo zilijengwa lini na serikali ipi?
Hebu tuache propaganda za kijinga za kuwachonganisha watu badala ya kusema ukweli.

Unajua kuna mikoa hata haijui kitu kinachoitwa miradi mikubwa ya maendeleo zaidi ya nguvu zao wenyewe.
Hospitali nyingi unazosema zimejengwa kwa nguvu ya wananchi kupitia taasisi za dini kwa kuuza mazao yao na kutoa sadaka.
Lakini chaajabu hiyo mikoa na maeneo unayosema wanautajiri mkubwa sana wa ng"ombe ,mbuzi ,kilimo ,uvuvi,madini n.k. lakini bado tangu uhuru bajeti kubwa zinakimbila huko lakino hakuna matokeo chanya mana hawataki kuwashirikisha wananchi zaidi ya kutaka kuwatumia kama chambo cha kupata kura kwa kuwaambia tumewaletea hiki na kile.
Watu wana mang'ombe kwa maelfu inakuwaje viongozi wao washindwe kuwaunganisha na kuwapa elimu ya kuunganisha nguvu zao na kuchanga na kujenga hospitali au vyuo au shule bora?

Hivi huko unakosema umewahi kuangalia hata huduma nyingine zisizo za kiserikali kama nyumba zao za ibada jinsi zilivyojengwa kwa kiwango kizuri na hao wenye utajiri mkubwa lakini wanabaki wakisubiri kubebwa na serikali ?
Au hizo nyumba za ibada nazo wamejengewa kwa najeti ya serikali?

Maeneo yenye wasomi wengi kama hayo lakini wanachojua ni kudharau watu wengine tu na kujaza makabrasha kwenye kabati lakini mpaka kanisa la pale nasikia lilijengwa na mkubwa mmoja .

Wabunge wao wanabaki kuwa na majungu tu na kugonga meza na kuipigia serikali magoti badala ya kuwapa ujasiri watu wao kwa kuwaaminisha kuwa wanauwezo wa kutumia wingi wao na mali zao walizo nao kujenga taasisi mbali mbali na kuleta maendeleo?

Hii sio sawa ?
Keki ya Taifa igawanywe sawa kila wilaya na wabunge waweke vipao mbele vyao huku wakitumia nguvu za wananchi wao kuhamasisha maendeleo.
Kuna maeneo watu wanauza mpaka kuku ili kujenga Hospitali ya kanisa au chuo kikuu cha kanisa lakini wengine wana miliki mpaka ng"ombe 1000 lakini hakuna hamasa ya kumwambia auze ngombe hata mmoja achangie shule ya chekechea.
Ni majungu tu na kuwadanganya watu kwa kusema kuwa wale walikula sasa ni zamu yetu!!!. Shame apon them!!
 
Kibinadamu na kibongobongo hakuna tatizo lolote kujenga hospitali chato kama pesa ingekuwa yake tena aweke na vifaa vizuri kushinda hata hospitali za ujerumani,marekani,India na ikiwezekana mtu yeyote asiyetokea kanda ya ziwa lazima aombe visa la sivyo hakuna matibabu.itapendeza.
 
Hivi TBA wanalipa kodi?...je vijana waliosomea hixo kazi na hawapewi tenda hixo wanajiajiri vipi? Tunakuzaje tax paying base?
 
Tafsiri yako ni ya miaka ya 70s
Tafuta ujuwe mpango unaoendelea wa Taifa juu ya ujenzi wa Hospital wilaya na rufaa kika Mkoa na za Kanda zitabaki kuwa za kanda.
Nikutaaru tu kuwa mwanzoni mwa mwaka Huu Waziri Mkuu alikuwa anazindua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huko Njombe. Hizi zinapokea referred wa kutoka Wilayani na za binafsi zenye hadhi ya kiwilaya.
Sasa kama mikoa yote ya kusini pamoja na mikoa yote ya nyanda za juu kusini kwa pamoja na ukubwa wake wote hazina hospital hata moja ya aina hiyo, why chato wakati kuna Bugando?
 
Back
Top Bottom