Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa wilaya ya Chato mkoani Geita

Unao ushahidi gani kwamba fedha zinazojenga Chato hazina baraka za bunge?.
Serikali haiku-dispute hoja ya wapinzani kwamba bajeti ya bilioni 39 haikuwa imepitishwa na Bunge!

Unao ushahidi gani kwamba pesa zinazopatikana kwa maana ya mapato hazina mgawanyo sahihi wa matumizi kwa kila kona ya Tanzania?.

Kama kuna mushrooming ya ujenzi wa miundombinu Chato ghafla tu kwa kuwa Rais anatoka huko, unahitaji ushahidi gani tena?

Ziongelei relevance ya bunge, naongelea uwezo wa mbunge mmoja mmoja katika kutafuta uwekezaji kwa ajili ya maeneo wanayotoka, na sio kubakia kulalamikia kidogo kinachogawanywa kwa wote.

Kazi hiyo ni ya wabunge? Wapi imeandikwa kwenye Katiba ama Sheria? Kazi ya wabunge ni kuisimamia serikali. Hayo mengine siyo majukumu yao. Period.
 
1. Kwa ninavyoelewa miye, Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro ni KCMC tu, nyingine 2 ni zipi?
2. Hao watu milioni 4, ni wa Wilaya ya Chato au Mkoa wote wa Geita?
3. Kama Geita (Mji au Mkoa) haina "hata Hospitali ya Wilaya", (kitu ambacho SIYO kweli), kwanini Hospitali hiyo ya RUFAA isijengwe Geita Mjini ambako ni Makao Makuu ya Mkoa?
4. Je, Raisi angekuwa natoka sehemu nyingine ya Nchi (mfano Kankoko, Kondoa, Kisarawe, Nanyumbu, Momba, nk), bado Hospitali hii ya RUFAA ingejengwa Chato?
KCMC, Marangu na Kibong'oto. Milioni 4 mkoa mzima angalia sensa. Ilichukua part ya Mwz na part ya Shinyanga. Ijengwe wapi haina maana inahudumia watu wote. Airport ziko KIA na Arusha na Moshi. Geita hakuna.
 
1. Kwa ninavyoelewa miye, Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro ni KCMC tu, nyingine 2 ni zipi?
2. Hao watu milioni 4, ni wa Wilaya ya Chato au Mkoa wote wa Geita?
3. Kama Geita (Mji au Mkoa) haina "hata Hospitali ya Wilaya", (kitu ambacho SIYO kweli), kwanini Hospitali hiyo ya RUFAA isijengwe Geita Mjini ambako ni Makao Makuu ya Mkoa?
4. Je, Raisi angekuwa natoka sehemu nyingine ya Nchi (mfano Kankoko, Kondoa, Kisarawe, Nanyumbu, Momba, nk), bado Hospitali hii ya RUFAA ingejengwa Chato?
Nimesahau. KIA ilihengwa wakati Waziri wa Fedha ni Mtei na Waziri Mkuu Msu
 
Maelezo gani Mkuu unataka zaidi ya hiyo picha? Mbona picha hiyo ina maelezo ya kutosha kujua huu uzi unastahili kuwepo kwenye jukwaa lipi?
Mkuu achana na hayo mapopo ya uviciciemu. Hayanaga hoja kama makondoo mwitu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Salamu Chato, umejaa neema,
Magumashi yu nawe.
Umebarikiwa kuliko wilaya zote,
Na Magumashi, mzao wa ardhi yako, amebarikiwa.
Chato Takatifu, Wilaya ya Magumashi,
Utuombee sisi wakosefu,
Sasa na saa ya kutumbuliwa kwetu.

Amina.
 
Dah nimecheka sana. Hiki ni kipaji cha level nyingine kabisa.
 
Bugando ni ya taasisi ya dini kama ilivyo KCMC ya Moshi.

Kusini kuna Mbeya ni ya Rufaa na ipo siku nyingi.
Mtwara pale mikindani imajengwa ya Rufaa pia na ujenzi unaendelea.

Njombe tayari inajengwa ya Rufaa Mkoa na iujenzi ulizinduliwa na Waziri Mkuu january ya mwaka huu
Wewe acha kudanganya wajinga, mbeya na hizo unazo sema njombe lini zitakamilika?
Unajua hospital ya Musoma imechukua muda gani hadi sasa imekua mazalia ya popo?
Mbona mnatetea ujinga, kwani geita ni chato tu mbona kuna ushirombo, geita yenyewe ambayo iko katikati ya mkoa why chato?
_ Traffic light
_International airport
_ TRA
_ sasa hospital ya rufaa
Chato, why, why, why?
 
CHATO OYEEEEE! Tunakoelekea Ikulu itahamia CHATO! Kutoka Geita na Chato ni mbali sana lakini mkoani hakuwekwi huduma muhimu zinapelekwa CHATO! Mliochagua CCM Mungu anawaona, heri kupigia kura zimwo kuliko CCM!
 
Wewe acha kudanganya wajinga, mbeya na hizo unazo sema njombe lini zitakamilika?
Unajua hospital ya Musoma imechukua muda gani hadi sasa imekua mazalia ya popo?
Mbona mnatetea ujinga, kwani geita ni chato tu mbona kuna ushirombo, geita yenyewe ambayo iko katikati ya mkoa why chato?
_ Traffic light
_International airport
_ TRA
_ sasa hospital ya rufaa
Chato, why, why, why?
Acha kukurupuka!
Hospital ya Rufaa ya Mbeya ni ya siku nyingi na inafanya kazi pengine hata kabla hujazaliwa.
 
Walikuwa wanalalamika ufisadi. Sasa wanalalamika kujengwa hospitali. Kununuliwa ndege, kununuliwa meli, kuletwa kwa bomba la mafuta, kukamatwa kwa mchanga wa dhahabu, kupigwa vita madawa ya kulevya, kubomelewa nyumba zilizo kwenye eneo la ujenzi wa barabara na kadhalika. Ni matatizo mazuri.

Magufuli amesema wazi pamoja nakulitumikia taifa ni ujinga kiongozi kusahau maeneo ya kwao. Kumbukeni Cleopa Msuya alivyoendeleza wilaya ya Mwanga. Kama kina Kikwete na Mkapa walisahau kwao wakashughulikia kwa wake zao ni ubozi wao.

Halafu watu na akili zenu mko hapa kujadili hospitali ya rufaa. Huu ni ushamba babu kubwa. Madaktari ndio wanatakiwa wawe wa rufaa sio hospitali. Na madaktari wa rufaa wanakuwa na ofisi zao wenyewe. Hospitali zote kuu zinatakiwa ziwe na vifaa na ubora wa hali ya juu. Hakuna cha hospitali ya rufaa.

Na mjue tofauti ya hospitali, clinic, na vituo vya afya au ofisi za madaktari. Kwa jiji kama la Dar linatakiwa liwe na hospitali za ukubwa wa Muhimbili si chini ya tano. Na hakuna ujinga wa kusema eti moja katika hizo ni ya rufaa.
 
7a7f2b1512982e3e93252f1e95126243.jpg

Kama ni kweli haikupaswa kuwapo Geita? au tuna wivu?
 
Back
Top Bottom