Ujenzi wa barabara zisizo na ubora tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujenzi wa barabara zisizo na ubora tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mlimbwa1977, Feb 14, 2011.

 1. m

  mlimbwa1977 Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taifa la Tanzania limekumbwa na kirusi 'wizi' ambaye kwa hakika ataliangamiza kabisa bila juhudi za makusudi kuchuliwa na wananchi wenyewe.Kila kukicha hali ni bora ya juzi,gharama za maisha zinapanda kila kukicha,angalia mafuta yanapanda bei kwa kasi huku wanaotegemewa walau kupoza makali wanalipana mishahara minono,umeme imekuwa anasa,vjijini wanausikia harufu yake kwa mbali ikitokea mijini (hakuna juhudi zinazoonekana za kuwafikishia huduma hiyo walau kwa matumaini hata ya miaka thelathini ijayo),bei za vyakula zinapanda kila kukicha,yote haya chanzo chake ni kirusi wizi,maofisini ni wizi tu,manunuzi,ujenzi wa majengo mbalimbali hauonyeshi uhalisia wa matumizi yake.kila mtu anachukua chake mapema,hakuna anaejali,wakaguzi wa mahesabu ingawa wanaonekana kufanya vizuri kwa ripoti za hivi karibuni lakini hakuna kikubwa cha maana kinachofanyika,wengi wao wamebobea kwa kuomba rushwa,mahakamani,hospitali,ardhi,nk,Vyuoni/mashuleni wanafunzi wafanaulu kwa kuiba/kutazamia kwa wenzao.HALI NI TETE NI WIZI TU KILA MAHALI.

  Tuangalie ujenzi wa barabara zetu hasa maeneo ya mijini.Barabara karibu zote zinazojengwa hazina ubora unaotarajiwa licha ya uwepo wa wahandisi(Engineers) katika halmashauri zetu.Hivi karibuni nilibahatika kutembelea miji ya Lindi,Tabora,Mtwara,Kigoma na Dar es salaam.Kwa hakika barabara zinazojengwa/zilizojengwa ni wizi mtupu hazionyeshi ubora unaostahili.Angalia Dar es salaam,barabara ya Kilwa(Mbagala) hata kama ni ya msaada au vinginevyo ni aibu tupu.Hata barabara zinazojengwa hakuna kikubwa cha kujivunia,angalia upana wake na linganisha na wingi wa magari ,pia kadiria baada ya miaka kadhaa ijayo kinachofanyika sasa sio wizi mtu huo? WATANZANIA WENZANGU NINI KIFANYIKE SASA KUKOMESHA WIZI HUU?
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Usiseme sana! Hali ni mbaya kushinda maelezo!
   
Loading...