Ujenzi ukisiliza watu ujengi

Inategemeana na mambo mengi hata hiyo 30m bado ni nyingi au ndogo kwa mwingine,mfano hiyo nyumba kwenye aviator yangu ni 4 bedroom house imecost around 24m pande za swax
umejenga nyumba ya ukubwa gani? na vifaa ulivyotumia je? halafu swax ndo wapi boss?
 
Hiyo 30milion huku kwetu unajenga ghorofa la maana binafsi nimejenga nyumba ya vyumba viwili sebule na jiko choo ndani kwa milion 4 tu ....
aisee kumbe heri kukimbia mjini kwa kweli. ina maana huku watu wanatembelea nyumba barabarani na vi-bebiwoka vyao!
 
Ila wewe umevunja records
Mkuu amini kabisa, nyumba iko mipeko/mbande na bati tayari nimeshanunua 110, gharama ya bati ni 3,289,000 @ 29,900 na kwenye ujenzi hadi sasa hela niliyotumia no 13m ambapo na katika hiyo toa 5,500,000 niliyonunulia kiwanja
 
Hongera sana mkuu,
 
Ni kweli Watu wanatishana wakati hata bei ya mchanga wa bagamoyo hawajui bei, hata bei ya msumali au cement hajui,kutwa kutaja bei za juu tu na kukatisha tamaa.
 


Mkuu sijui kama nakusoma vizuri. Nimejenga kijijini na wala sijamaliza. And I mean kijijini haswa. (Angalizo: am building a proper house with all modern amenities you would think of huko mjini). Hiyo bei ya mbao in very unrealistic. In fact Mimi nimechana mbao kutoka shambani Kwangu. Mbao nilijaribu kufuata mwenyewe porini bado nikaona bei haikamatiki. Tofali za shs 100 in zipi? Labda utueleweshe! Tofali za kuchoma moja nilinunua kwa shilling 35! Na Fuso moja inabeba tofali 5000! Sasa mkuu nyumba ya trip moja in ya kuishi au kufugia sungura?

Labda baada ya kuanza Ujenzi nitoe ushauri. Kama unataka kujenga wewe anza. 95 % ya wengi humu ushauri wao hautakuwa applicable kwako. Ujenzi wa kijijini hauna urahisi wowote. Nanunua cement kwa 17500....hapo in baada ya dangote kuishusha.....maana cement ilifika mpaka 21000!

My advise....nyumba zinatofautiana. Ukitaka hata nyumba ya shillingi 20M unaweza kujenga. Swali in je: umejenga nyumba au umejenga shelter?
 
Mkuu safi sana, tupo njia moja
 
Acha kutisha watu
 
Mafundi wamekuibia sana, milioni 15 unajenga nyumba standard kabisa.
 
Duuh siwezi kudanganya na kwa faida ya Nani ukweli nimejenga huku kwetu cement ni 13000 tu

Na tofali inategemea na size kuna vile vidogo sana huku ni 50,ya kawaida ni 100 makubwa ni 200

Na mbao ndio bei yake huku sijui sasa wewe upo kijiji gani na ukumbuke utofauti wa maisha lazima uwepo..ndio mana nikaongelea huku mie nilipo gharama ndio izo..

Ningekuwa na uwezo ningetupia kapicha....ukweli nyumba imesimama aswaa kama una hela hiyo na upo mlalo nitafute lazima utajenga tu.
 
mimi tatizo kiwanja kilik
KIWANJA KILIKUWA SQ 1468 UKUTA UMEKULA SANA PESA KUZUNGUSHIA MATOFALI CHOTE
 
umejenga nyumba ya ukubwa gani? na vifaa ulivyotumia je? halafu swax ndo wapi boss?
Swax=sumbawanga,nyumba=12mx112m self contained yenye 3 bedroom,kitchen,store,public WC/sh ,,materials ni za kawaida tu,tofali nilifyatua mwenyewe,nikajengea udongo na cement,,mafundi ni jamaa zangu na pia mie ni professional wa ujenzi so nilidesign ramani na kusimamia ujenzi mwenyewe
 
NIMEKUELEWA UWANJA WANGU NI MKUMBWA SQ 1595 UKUTA UMEKULA SANA NA NYUMBA VYUMBA 4 NA SITTING ROOM NA SELF ZOTE SIO MBAYA
 
Tatizo unakuta mtu hajawahi kujenga hata banda la sungura lakini anatoa ushauri.
 
shukrani mkuu na hongera zako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…