Ujenzi Hatarishi Makumbusho Dar

Ujenzi Hatarishi Makumbusho Dar

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,990
Reaction score
34,838
Hivi ujenzi wa majengo haya yanayoota kama uyoga jijini Dar kuna utaratibu wa kufuatilia kujua kama taratibu na usalama kuzingatiwa wakati wa ujenzi?

Hapa napita makumbusho kuna jengo linajengwa la CTL LTD nimeshuhudia mafundi wakiendelea na ujenzi wa ghorofa ya nane huku wakipandisha nondo kwa kuzivuta kwa kamba iliyoungwaungwa kihuni toka chini hadi ghorofa ya nane!!!

Pale ndio njia ya daladala zinazoingia na kutoka makumbusho na watembea kwa miguu kibao....zile nondo zikiporomoka zitaleta maafa....kamba zenyewe zimeungwa kihuni tu......

Acheni kuhatarisha maisha ya watu bana.....
 
Back
Top Bottom