Ujasusi wa kisaikolojia

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
821
2,072
Nadharia za kijasusi karibu zote zinamsimamo unaofanana, japo zinaweza kutofautiana mwelekeo tu kulingana na tukio, Tukio kama la mauaji, ujambazi ama la ugaidi kiuchunguzi yanaweza kufanana kwa namna moja ama nyingine, uzito wayo utakuja kama hakuna mtuhumiwa/watuhumiwa waliokamatwa kwakuhusishwa nayo, na jambo hili linaweza kubaki kwenye dhamiri ya wapelelezi husika tu kuamua kuhitimisha uchunguzi wao, au kusimama kwenye mizani ya kisiasa katika taaluma pana kama hii. Hili litategemea zaidi mwelekeo wa taifa hilo.

Ushahidi usio na shaka unaoweza kupatikana toka kwa watuhumiwa hata wangekuwa miamoja au milioni katika tukiomoja ikiwa kutakuwa na dhamiri ya kuujua ukweli wa matukio hayo ni sehemu ya weledi muhimu katika fani hii mtambuka. Sehemu kubwa ya kiuchunguzi huwa katika kubaini ukweli toka kwa watuhumiwa (suspects), hapa ndipo kazi ya ujasusi wa kisaikolojia huhitajika (Forensic Psychology).

Nadharia hii tunaweza kuiangazia kwa mwanasaikolojia Edward Geiselman ambaye ni miongoni mwa waliofanya tafiti nyingi sana kuhusiana na Cognitive interview ( mahojiano ya utambuzi ) katika chuo kikuu cha California. Njia hizi ndizo zinazotumika na wapelelezi duniani kote hadi leo, ingawa kuna maboresho ya kiteknolojia.

Kwenye ujasusi kuna jambo linaitwa "Cognitive load", unapomuuliza maswali mtuhumiwa aliye mbele yako, yaani unamuuliza swali anakakaa kwa muda Fulani (dakika mbili au tano hivi) kulitafuta kichwani jibu lake,. Wakati huo huo anajiandaa, unaongeza mzigo mwingine wa swali , kijasusi wanasema unampa " Mental Energy". ikimaanisha ili aweze kufunguka zaidi, watoto wa mjini wanasema kutiririka.

Yote haya katika ujasusi nikutaka kumbaini muhusika na kumpelekea kukiri, huku ukimhoji kama rafiki na kwa upole na kama anataka chochote wakati wa mahojiano unaweza kumpa mfano sigara, kinywaji, chakula nk. Mbinu hii inaitwa (Confession Oriented Method with Distinctly Parent Tone).

Kuna mbinu nyingine inatumiwa ili mradi kumtia hatiani mtuhumiwa ama kumuachilia kwakujiridhisha hahusiki. Kuna mbinu nyingine inatumiwa ili mradi kumtia hatiani mtuhumiwa ama kumuachilia kwakujiridhisha hahusiki. Njia hii ni ya kawaida sana ya kijasusi ya kumhoji mtu ukimuangalia mwili wake hasa macho. Katika macho tunatafuta kumbukumbu yako na ubunifu wako, maana kuna watu wajanja duniani lakini kwa falsafa hii wengi wanafeli.

Mtu yeyote akitaka kukumbuka kitu au jambo lolote wakati ukimuhoji kwakumuangalia machoni, Macho yake huenda kulia, wataalamu wa "Cognitive Interviews" wanaelewa ubongo wake wa kumbukumbu unaanza kufanya kazi. Anapoanza kufikiri (Thinking), macho yake yanaenda juu kushoto hapo, yakiashiria utambuzi wa jambo katika ubongo wa kati, na ndipo uongo na ukweli unaupatia hapo kwa mtuhumiwa, huku usiache kumuongeza maswali ya kumchanganya mtuhumiwa, dhumuni lako wewe liwe kuusoma mwili wa mtuhumiwa, huku yeye anapaparika na maneno. Hii inaitwa (Mental note of the suspect's eye activity).

Kuna mbinu nyingine ambayo hata watu wote huwa wanaitumia, inaitwa ya kiuandishi habari ( journalistic approach) na wapo waandishi wa habari makanjanja wa mjini, kwakuijua tu hiyo dhana, basi hujiita Usalama wa Taifa, wakati ni vibaka, Kwa wale waliosoma uandishi habari utakumbuka dhana hii, ili uandike habari na iitwe habari lazima kuwepo na kitu kiitwacho 5W ( Five W). 5W ni maneno 5 kwa kizungu ambayo ni (Where, When, What , Who, Why) , wataalam wa mambo ya habari na mawasiliano (journalism) waliokwenda shule waliongeza lingine ambalo ni "How" ...........

Ni weekend ya #SafishaGhala kutoka Mbutu shambani,

Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi kwa punguzo la zaidi ya nusu bei @ 30,000/= badala ya bei halisi ya 80,000/=

Lipia 30,000 kwa 0715865544 au 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo.

Walioko nje ya Dar watachangia nauli ya 8,000 tu
 
Avatar yako tu, imenoga, mmmmm! imenisaidia kukaa hapa muda mrefu tangu asubuhi. uko wapi mkuu!
 
Back
Top Bottom