Ujasusi Sebuleni Kwetu

 
Chief umefanya makosa ya kiuandishi hapo kwenye "Bayat" usahihi ni "Baiya" (Kiapo cha utiifu).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaona katika makala kuonyesha Odeh aliingia kenya mwaka gani ? Naomba unisaidie katika hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh umetisha sana bro. Shukrani sana kwa tag ...nieleze tu ukweli wewe unajua aise! Mungu azidi kukubariki kwa stories tamu kama hizi za kusisimua.

Sehemu ya tatu lini mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaona katika makala kuonyesha Odeh aliingia kenya mwaka gani ? Naomba unisaidie katika hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app

  • Wadih El Hage, a.k.a. Mohamed Sadeek Odeh, a.k.a. Mohamed Rashed Daoud Al-'Owhali, a.k.a. Khalfan Khamis Mohamed
CategoriesConspiracy, TerrorismLinks
back to topSummary
Wadih El-Hage, 40, is a naturalised American citizen who was born in Lebanon. He has admitted being Osama bin Laden's personal secretary. He was accused of being the key organiser of the Kenya cell and of setting up front companies in Kenya for Al-Qaeda. He left Kenya almost a year before the bombings, after being questioned by the FBI in Africa. At the time of the bombings, he was living in Arlington, Texas, with his wife, April, and seven children. El Hage claimed he only worked for bin Laden in legitimate businesses and had no contact with him since 1994. El Hage was charged with conspiracy to murder Americans.

On 29 May 2001, El Hage was convicted for conspiracy to kill United States officers and employees engaging in official duties and conspiracy to destroy buildings and property of the United States. In addition, he was found guilty of giving false statements to a federal jury (perjury). On the basis of this conviction, El Hage was sentenced to life in prison without the possibility of being released.
ICD - Bin Laden et al. - Asser Institute
 
Shukrani,nimepata pakuanzia. Naendelea kusoma kaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu na mimi naomba unitag, ili nipate huu uhndo vizuri zaidi.
 
Tatizo lako bold unatoa mada halafu unakimbia
Maswali tumuulize nani

E&K
 
Hongera kwa uzi nzuri nataman uendelee
 

UJASUSI SEBULENI KWETU



SEHEMU YA TATU





Katika sehemu iliyopita tuliona namna ambavyo Odeh alianza kutengeneza mtandao kwa 'ku-recruit' vijana wa Kitanzania ambao alikuwa anasali nao msikiti mmoja hapa Dar es Salaam.

Nilieleza pia kwamba oparesheni ambayo ilikuwa inapaswa kutekelezwa hapa Afrika Mashariki ilikuwa inaitwa Kaaba kwa Kenya ambalo ni jina la jiwe lililopo mji mtakatifu wa Maka na hapa Tanzania Oparesheni hiyo iliitwa Al-Aqsa ambalo ni jina la moja ya misikiti muhimu zaidi katika uislamu uliopo huko Jerusalem.

Baada ya zoezi zima la 'recruitment' kukamilika hatua ambayo ilikuwa inafuata ni utekelezaji mzima wa oparesheni. Jambo la msingi sana kukumbuka ni kwamba mpaka kufikia hatua hii undani hasa wa oparesheni kwa mfano 'targets' na siku lengwa ya utekelezaji wa tukio ilikuwa ni siri kubwa kwa uongozi wa juu pekee.

Kwa mfano, kuna bwana mmoja anaitwa Ali Mohammed ambaye nilimuelezea sana kwenye makala ya 'Behind The Curtain' ambaye aliwahi kuwa Meja kwenye jeshi la Misri akiwa kama mtaalamu wa 'counter-terrorism' na baadae kwenda kuishi ng'ambo California nchini Marekani na hata kuoa huko Mmarekani na pia kujiunga na jeshi la Marekani na kupangia kituo cha Fort Bragg. Baadae alipanda cheo na hata kuwa mkufunzi katika kituo cha kijeshi cha Marekani cha J.F. Kennedy International Warfare School akiwa kama mtaalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati.
Lakini baadae alitorokea nchini Afghanistan kujiunga na Mujahedeen ambao walikuwa wanapigana na Urusi na serikali ya Afghanistan ya kipindi kile ambao walikuwa ni vibaraka wa Urusi. Huko Afghanistan ndiko alikutana na Bin Laden na kuibuka kuwa kiungo muhimu mno ndani ya Al-Qaida na hata kuhusika kama moja wa wakufunzi wakuu wa kijeshi wa Al-Qaida.

Pale mara ya kwanza nilipoeleza kwamba Odeh alitembelewa na mlinzi binafsi wa Bin Laden, huyu ndiye ambaye nilikuwa namuongelea. Alikuwa ni mwambata wa karibu mno wa Bin Laden na msiri wake wa karibu.
Odeh alipoenda Sudan kuonana na Bin Laden na kupeleka ripoti kuhusu intelijensia ambayo alikuwa amekusanya nchini Kenya… alitoa pendekezo kuhusu sehemu nne ambazo wanaweza kufanya shambulio. Ya kwanza ilikuwa ni Ofisi ya Kilimo ya Marekani nchini Kenya, Ubalozi wa Ufaransa, Ubalozi wa Marekani na Kituo cha Utamaduni cha Kenya ambacho kilikuwa kinafadhiliwa na Marekani na huvutia watalii wengi Kimarekani.

Kwa hiyo hata Ali Mohammed alipomtembelea Odeh nchini Kenya na kumtaka ahamie Mombasa ili kujiandaa na Oparesheni awali hakumueleza hasa ni 'target' ipi ambayo Bin Laden alikuwa ameichagua.


Kwa hiyo mpaka kufikia hatua hii maandalizi yalikuwa yamefikia hatua nzuri… timu zote mbili za hapa Dar es Salaam na ile ya Nairobi zilikuwa zinasubiri maelezo tu ni nini cha kufanya.

Kuna suala la muhimu sana hapa naomba twende sawa ili usipate mkanganyiko wa majina na mtiririko wa madaraka katika oparesheni hizi kadiri ambavyo tunaendelea na makala. Naomba niweke sawa sawa na kwa mkazo zaidi…

Odeh alihusika na kufanya 'recruitment' na kukusanya intelijensia kwa mji wa Dar es Salaam na Nairobi na kisha kuziwasilisha nchini Sudan ambako Bin Laden alikuwapo kipindi hicho.
Kisha Bin Laden alimtuma mlinzi wake binafsi na msiri wake Ali Mohammed kwenda Nairobi kumpa maagizo Odeh kuhamia Mombasa na kumpa fedha za kununulia boti. Kisha huyu Ali Mohammed akarejea Sudan kwa Osama.

Baada ya haya yote kukamilika Bin Laden alimuingiza mtu wa kuja kuongoaza oparesheni zote hizi mbili aliyeitwa Ali Saleh. Ali Saleh alikuwa ndiye kiongozi wa Oparesheni ya Dar es Salaam na ile ya Nairobi.

Ni vyema kutochanganya watu hawa watatu. Mohammed Sadiqq Odeh, Ali Mohammed na Ali Saleh.

Huyu Ali Saleh wana kitu kimoja ambacho wanafanana na Ali Mohamed, wote asili yao ni Misri. Ali Saleh jina lake halisi anaitwa Abdullah Mohammed Adbullah. Kabla ya kujiunga na vikundi vya msimamo mkali, Ali Saleh (Abdullah) alikuwa mcheza soka maarufu sana huko kwao Misri. Kipindi ambacho kiwango chake kilikuwa kwenye kilele alikuwa ni tegemeo la timu ya Taifa ya Misri. Lakini baadae kama mwenzake naye alitimkia Afghanistan kwenda kujiunga na Mujahedeen kupinga uvamizi wa Urusi na ushawishi wao ndani ya serikali ya Afghan. Baadae alipanda ngazi mpaka kufikia kuwa moja ya mtu mwenye kuaminiwa na Osama na moja ya wasiri wake.

Ndani ya kikundi cha Al-Qaida kuna ule uongozi wa juu kabisa, yaani ile 'inner circle' ambayo wenyewe Al-Qaida wanaiita 'Shura' na kuna kamati ya uongozi wanaiita 'Fatwah Committee'.
Ali Saleh alikuwa ni mjumbe wa mabaraza yote haya mawili.

Sasa huyu ndiye akatumwa na Bin Laden kuja Afrika Mashariki kusimamia Oparesheni Kaaba na Oparesheni Al-Aqsa.

Baada ya Ali Saleh kutua Nairobi alianza kupanga majukumu kwa ufanisi mkubwa.

Kwanza kabisa alitengeneza vitengo vya utendaji… kila 'cell' ilikuwa na vitengo vinne;

i) Kitengo ch Intelijensia
ii) Kitengi cha Utawala
iii) Kitengo cha mipango na maandalizi
iv) Kitengo cha utekelezaji


Mfumo wa utendaji katika cell ulikuwa katika namna ambayo kiongizi wa kitengo cha Intelijensia, Chief of Intelligence alikuwa ndio kiongozi wa vitengo vingine vyote na pia msaidizi wa Ali Saleh katika cell husika.
Kiongozi huyu wa Intelijensia alikuwa na kazi ya kufanya surveillance ya target, kutambua udhaifu wa target zao na kuhakikisha wale walioko kwenye vitengo vingine wanatekeleza majukumu yao na pia kupima ufanisi wao.

Ali Salahe pia aliweka mfumo ambao ulikuwa unatumiwa na Al-Qaida kwenye cell zao nyingine nyingi duniani ambao kwenye ulimwengu wa ujasusi unajulikana sana kama "leaderless resistance".
Kwamba wanachama wa cell kila mmoja anafanya kazi kwa kujua majukumu yake tu pasipo kujua kiundani majukumu ya watu wa kitengo kingine. Na pia wanachama wa cell wanakuwa wanaishi mbali mbali. Kwa mfano katika cell ya Kenya, Odeh alikiwa akiishi Mombasa wakati wenzake walikuwa wakiishi Nairobi.
Hii ilikuwa makusudi ili kusaidia Cell isiweze ku-collapse ikitokea mmoja amekamatwa kwa mfano na pia ilikiwa ni kinga kama ikitokea cell ikiwa 'infillitrated' na adui asiweze kujua siri zote.



Pale Nairobi, Ali Saleh alimteua kijana anayeitwa Abdullah Mohammed Fazul kuwa Chief of Intelligence na kama ambavyo nimeeleza hii ilimaanisha pia alikiwa ndiye kiongozi msaidizi wa Ali Salehe kwa cell ya Nairobi. Fazul ni Mkenya ambaye wazazi wake wana asili ya visiwa vya Comoro. Fazul alikiwa ni 'mchawi' wa mifumo ya kompyuta. Miaka michache iliyopita alikuwa amehitimu chuo kikuu akiwa mwanafunzi bora wa kwanza kwa darasa lake. Wenzake walimuita kwa code name ya "Harun".

Odeh kutokana na ubobezi wake wa milipuko alipewa kitengo cha "mipango na maandalizi". Yule Mkenya mwingine niliyemuelezea kwenye sehemu ya kwanza, Mustafa Fadhil (code name 'Hussein') ambaye alimsaidia Odeh kupata mke mkenya waliporejea kutoka Somalia, alipewa kitengo cha utekelezaji kutokana na kuufahamu vyema mji wa Nairobi.



Hapa Dar es Salaam nako cell iliundwa kwa mtindo huo huo… yule jamaa Mzanzibari wa Mdimuni anayeitwa Hamis (jina lake kamili ni Khalfan Khamis Mohammed au 'KK Mohamed' kama wenzake walivyopenda kumuita) ambaye ndiye alimuingiza 'fupi' kwenye mtandao huu hatari, yeye aliteuliwa na Ali Salehe kuwa chief of intelligrnce na kwa hiyo kiongozi wa cell ya hapa Dar es Salaam.

Kwa kuwa hapa Dar es Salaam kiswahili ndiyo lugha kuu, Ali Saleh akampanga 'fupi' (Ahmad Ghailani) kuwa kiongozi wa kitengo cha mipango na maandalizi akisaidiwa na mkenya anaitwa Sheikh Sewadan na mwenzake aliyeitwa Fahid.
Kwenye kitengo cha utekelezaji alipangwa muarabu ambaye wenyewe walimuita code name "Ahmed Mjerumani".


Kwa hiyo cell zilikiwa zimekamilika… na hivyi kazi ilikiwa imeanza rasmi.

Kitabu changu cha kwanza NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI & UJASUSI kimekamilika... mwezi huu september kitakuwa mkononi mwako. Kaa tayari...



Habib
To Infinity and Beyond
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…