Ujasusi na uongozi: Mafanikio ya rais Putin katika kuirejesha tena Urusi

Raisi Jakaya Kikwete alikuwa na mpango wa haya mambo ya nishati ya nyuklia.
Lakini Maveteran wengi wa Usalama walishauri kwamba itakuwa ni hatari kwa taifa kwasababu Tanzania kuna rushwa sana hivyo hiyo teknolojia ya Nyuklia au madini ya Uranium yanaweza yakaanguka kwenye mikono ya makundi hatari ya kigaidi.
Hata wataalamu (Scientists) wanaosomea haya mambo ya nyuklia duniani kote huwa wanaangaliwa sana kwa jicho la tatu,
sasa kwa jinsi mifumo ya nchi yetu inavyolega na watu wanauzana kwasababu za Kisiasa na kimaslahi kama ambavyo tumeshuhudia tokea awamu ya pili unategemea hawa wanasayansi hawatakuwa sumaku ya utekaji kweli ???

Ushauri mwingine walisema inawagharimu sana mataifa makubwa kwenye kutunza vile vinu,
Pamoja na utupaji taka za Nyuklia ambao inasemekana ni gharama mno kwa nchi kama yetu.
Isitoshe ukisoma hata mtaji unaohitajika kurutubisha ile Yellow Cake ni pesa kubwa sana sanaa.
Tupilia mbali bado hujapeleka mamia ya wanasayansi nchi za nje kusoma.
Wanasema Tanzania bado hatujajiandaa.

NB: Lakini kubwa zaidi wazungu wanasema sisi tunaweza kuuza madini kwa nchi korofi kama Korea Kaskazini na Iran,
Kwasababu Tanzania tumeshawahi kupata kashfa miaka mingi nyuma kwamba tunaongoza kwa kuficha magaidi hatari hapa nchini kwetu. Pia miaka ya karibuni tumeshutumiwa kuwasaidia Iran na Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Hivyo kuwa na hii teknolojia kunaweza kuleta Unnecessary Attention ya mataifa makubwa nchini mwetu ambapo mambo yetu mengi ya kiulinzi na kiusalama yatakuwa hatarini. Inamaanisha Majasusi ya CIA, MI6, BND, MOSSAD na mengine yanaweza kupanua wigo wa kazi zao hapa nchini hadi wakapenya kila sekta kuhakikisha kweli tunakuwa na matumizi salama ya nyuklia (Watawala wetu hawatapendwa sana kumulikwa na hawa wazungu)

Japo, binafsi nasema kama nchi inabidi tubadilishe Mtazamo wa kifikra.
Hizi fikra za wale wazee wa miaka ya 60's, 70's na 80's inabidi zifanyiwe tathmini kwa upya ili nchi iendelee.
Dunia kila baada ya masaa 24 inapiga hatua kubwa sana ambazo hazimsubiri mtu, na taifa imara ambalo halitataka kuendana na kasi ya dunia basi ni lazima litakuwa katika huruma ya mataifa yenye nguvu. Kama tunahitaji viwanda basi ni lazima tujipange kuzalisha nishati ya kutosha kwa matumizi ya wananchi, wawekezaji na nyingine tuuze hata nje ya nchi.

Nawapenda sana wakina Dr. Kitine, Mzee Warioba, Mzee Mahiga na wengine wote ambao ni First Generation,
Lakini ili hili taifa liende mbele kuna mpaka ni lazima hawa wazee wawekewe, kwasababu naona wengi wao wana Nostalgia ya kutaka Tanzania ya mwaka 2018 ya karne ya 21 iwe kama ile ya miaka ya 1970's ya karne ya 20 ambayo wao waliishi na kuona ni Golden Age. Hatutawatenga kabisa lakini tunahitaji kutengeneza Mzani wa Chuma ambao utahakikisha mawazo ya wazee yanakuwa Realistic kuweza kulinganana hali ya sasa na pia mawazo ya kizazi cha vijana hayatishia misingi ya taifa. Hawa wazee wetu wameshachoka sana na ifike mahali hata kama tunawahitaji ni lazima wakae katika nafasi ya kushauri tu na siyo kimaamuzi. Japo Tanzania tuna changamoto kubwa sana ya kukosa Skilled Manpower hasa kwa vijana, japo naamini tukiweza kufanya Professional Synchronization tutaikabili hii changamoto.

ENOUGH WITH POLITICS OF FEAR......
THIS COUNTRY HAS TO MOVE FORWARD AT A GOD SPEED.
WE ARE 100 YEARS BEHIND THE WEST AND 60 BEHIND THE EAST,..WE NEED TO CATCH UP.
OR WE ARE GOING TO BE THE VICTIMS OF EASTERN ECONOMIC DEVELOPMENT JUST AS WE WERE TO THE WESTERN.
EXACTLY CHIFU,
 
Rushwa ikidhibitiwa na tukawa na uzaelendo pia tukiondoa masuala ya uchama( uccm, uchadema, ucuf..) naiman tutapiga hatua kubwa kimaendeleo.

Raisi Jakaya Kikwete alikuwa na mpango wa haya mambo ya nishati ya nyuklia.
Lakini Maveteran wengi wa Usalama walishauri kwamba itakuwa ni hatari kwa taifa kwasababu Tanzania kuna rushwa sana hivyo hiyo teknolojia ya Nyuklia au madini ya Uranium yanaweza yakaanguka kwenye mikono ya makundi hatari ya kigaidi.
Hata wataalamu (Scientists) wanaosomea haya mambo ya nyuklia duniani kote huwa wanaangaliwa sana kwa jicho la tatu,
sasa kwa jinsi mifumo ya nchi yetu inavyolega na watu wanauzana kwasababu za Kisiasa na kimaslahi kama ambavyo tumeshuhudia tokea awamu ya pili unategemea hawa wanasayansi hawatakuwa sumaku ya utekaji kweli ???

Ushauri mwingine walisema inawagharimu sana mataifa makubwa kwenye kutunza vile vinu,
Pamoja na utupaji taka za Nyuklia ambao inasemekana ni gharama mno kwa nchi kama yetu.
Isitoshe ukisoma hata mtaji unaohitajika kurutubisha ile Yellow Cake ni pesa kubwa sana sanaa.
Tupilia mbali bado hujapeleka mamia ya wanasayansi nchi za nje kusoma.
Wanasema Tanzania bado hatujajiandaa.

NB: Lakini kubwa zaidi wazungu wanasema sisi tunaweza kuuza madini kwa nchi korofi kama Korea Kaskazini na Iran,
Kwasababu Tanzania tumeshawahi kupata kashfa miaka mingi nyuma kwamba tunaongoza kwa kuficha magaidi hatari hapa nchini kwetu. Pia miaka ya karibuni tumeshutumiwa kuwasaidia Iran na Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Hivyo kuwa na hii teknolojia kunaweza kuleta Unnecessary Attention ya mataifa makubwa nchini mwetu ambapo mambo yetu mengi ya kiulinzi na kiusalama yatakuwa hatarini. Inamaanisha Majasusi ya CIA, MI6, BND, MOSSAD na mengine yanaweza kupanua wigo wa kazi zao hapa nchini hadi wakapenya kila sekta kuhakikisha kweli tunakuwa na matumizi salama ya nyuklia (Watawala wetu hawatapendwa sana kumulikwa na hawa wazungu)

Japo, binafsi nasema kama nchi inabidi tubadilishe Mtazamo wa kifikra.
Hizi fikra za wale wazee wa miaka ya 60's, 70's na 80's inabidi zifanyiwe tathmini kwa upya ili nchi iendelee.
Dunia kila baada ya masaa 24 inapiga hatua kubwa sana ambazo hazimsubiri mtu, na taifa imara ambalo halitataka kuendana na kasi ya dunia basi ni lazima litakuwa katika huruma ya mataifa yenye nguvu. Kama tunahitaji viwanda basi ni lazima tujipange kuzalisha nishati ya kutosha kwa matumizi ya wananchi, wawekezaji na nyingine tuuze hata nje ya nchi.

Nawapenda sana wakina Dr. Kitine, Mzee Warioba, Mzee Mahiga na wengine wote ambao ni First Generation,
Lakini ili hili taifa liende mbele kuna mpaka ni lazima hawa wazee wawekewe, kwasababu naona wengi wao wana Nostalgia ya kutaka Tanzania ya mwaka 2018 ya karne ya 21 iwe kama ile ya miaka ya 1970's ya karne ya 20 ambayo wao waliishi na kuona ni Golden Age. Hatutawatenga kabisa lakini tunahitaji kutengeneza Mzani wa Chuma ambao utahakikisha mawazo ya wazee yanakuwa Realistic kuweza kulinganana hali ya sasa na pia mawazo ya kizazi cha vijana hayatishia misingi ya taifa. Hawa wazee wetu wameshachoka sana na ifike mahali hata kama tunawahitaji ni lazima wakae katika nafasi ya kushauri tu na siyo kimaamuzi. Japo Tanzania tuna changamoto kubwa sana ya kukosa Skilled Manpower hasa kwa vijana, japo naamini tukiweza kufanya Professional Synchronization tutaikabili hii changamoto.

ENOUGH WITH POLITICS OF FEAR......
THIS COUNTRY HAS TO MOVE FORWARD AT A GOD SPEED.
WE ARE 100 YEARS BEHIND THE WEST AND 60 BEHIND THE EAST,..WE NEED TO CATCH UP.
OR WE ARE GOING TO BE THE VICTIMS OF EASTERN ECONOMIC DEVELOPMENT JUST AS WE WERE TO THE WESTERN.
 
Ni kweli kabisa ujasusi ni muhimu katika uongozi.lkn ndugu yangu nikwambie tu hawa wengi unaowaona kuwa ni viongozi wengi wanatokea tiss mfano h.polepole ni mtu wa tiss totally p.makonda kadhalika.shida ni vipaumbele vyao wanawaza watawale ili watajirike lkn si kwa manufaa ya nchi.yapo mengi kwa leo inatosha.
Duh!! kama chakubanga na bashite nao ni Tiss ,bas hii taasis iko icu na sio muda itakua mortuary!?bashite tiss?? Chakubanga tiss???
Inasikitisha.huko tiss wanafundisha basi kama product zao ndio hiz??
Taasis gan inayoshindwa kudhibit staff wake?????
 
Mafanikio ya Urusi kwa sasa inayoongozwa na rais mwenye misimamo thabiti aliyekuwa KGB wa zamani Vladimir Vladimirovich Putin ni yakushangaza kwa wengi hasa western block USA na allies wake wa NATO.

Urusi hii nchi ina historia yake ndefu sana na ya kuvutia kwenye vitabu vya historia kwa wale wanaopenda kusoma vitabu ukitafuta utaipata hapa sitaweza kueleza hata humu jamvini wadau wengi wameandika.

Kiufupi miaka ya hivi karibuni ilipitia katika misukosuko ya kiuchumi na kuifanya USA iwe inatamba kwa mikogo na majigambo lukuki na hii misukosuko ilianzia mwanzoni mwa miaka ya 1990 mara baada ya vita baridi kumalizika na kupelekea kusambaratika kwa USSR.
USA na allies wake walichukulia hilo kama ushindi mkubwa sana kwao kwani waliamini huo ni mwisho wa zile nguvu kubwa za Urusi.

Sasa akatokea huyu mtu anaitwa Vladimir Vladimirovich Putin KGB wa zamani ambayo sasa inajulikana kama FSB hawa ni majasusi wa Urusi, aliapa kuiongoza Urusi kuwa na nguvu kubwa kijeshi, Urusi yenye nguvu kubwa na taifa lisiloyumba kiulinzi na kiusalama kuilinda Urusi dhidi ya maadui hasa USA na NATO.

Ameshafanya mengi na amepata mafanikio makubwa katika uongozi wake hadi sasa NATO wanashangaa imekuwaje hawa watu wanakuja tena?(Coming back of Russians.)
Lakini mafanikio na misimamo isioyumba ya uongozi wa Putin vimejengwa kwenye misingi ile ya ujasusi wake aliupata kule KGB, yani uongozi wake upo kiujasusi ujasusi.

Naamsha mjadala tu hapa kuwa kuna uhusiano upi kati ya ujasusi na uongozi hasa tukijenga hoja zetu kwa mfano wa rais wa Urusi Putin.
Majasusi wengi hutumia akili za kiwango cha juu kwenye kazi zao na wanakuwa wazalendo ingawa sio wote mimi huwa nafikiria pia ingesaidia sana hata marais wa hizi nchi maskini za kiafrika wapitie mafunzo ya ujasusi ili kuamsha akili na uzalendo na hatimaye kuongoza mataifa yao na kuushinda umaskini uliokithiri.


Wakuu mwaonaje haya mambo, karibuni kwa hoja.
Kwa lugha nyingine ujasusi ni umbea ila nashangaa watu wanapinga umbea wa aina zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
alipokuwa na miaka 16 alienda makao makuu ya KGB na kuomba kujiunga. wakamwambia wao ndiyo hufuata watu. akawauliza ni kozi gani itammsaidia kujiunga, wakamwambia sheria na chuo kweli alisomea sheria. mbongo leo ukienda makao makuu ya TISS unaweza chezea vitasa.
Wee jamaa fala sana ujue

Nimecheka kinyamaaa
 
Putin ni namba nyingine alikua na rank ya juu sana kule KGB sasa tutalinganisha vipi na viongozi wa afrika hata kama walikua wamo idarani lakini hawakuwai hata kushiriki/kuratibu/kupafom operation/mission moja ya kibabe na ikawa completed ...
 
Mkuu herikipaji ,
Mosi, Umesoma vitabu vya UFUNUO WA YOHANA, NABII ISAYA, NABII DANIELI na NABII EZEKIELI?
Majibu yako haya yote utayapata humo ndani ni kwanini Urusi imeinuka kutoka mavumbini hadi kufika hapa leo.
Unaweza kudharau haya ninayosema lakini huu ndiyo ukweli na wala haukimbiliki; wachambuzi wa masuala ya ulinzi hawawezi kukubali hadharani lakini usiku kucha wanashinda wakisoma Utabiri wa NOSTRADAMUS, MAYANS na BIBLIA.

Pili
, Sidhani kama Ujasusi wa Vladmir Putin ndiyo umeifanya Urusi kufika hapo ilipofika leo.
Urusi tokea mwaka 1982-1984 ilishawahi kutawaliwa na Yuri Andropov ambaye alikuwa bosi wa K.G.B kwa miaka 15 lakini bado hali ya nchi ilikuwa mbaya sana hasa kwenye Uchumi.
Mathalani, George Bush alishawahi kuwa Jasusi mkubwa (MKURUGENZI MKUU) katika idara ya C.I.A lakini alitawala kwa miaka 4 na utawala wake una historia ya kuwa na sera mbovu sana nchini humo.

Deng Xiaoping hana historia yoyote ya Ujasusi lakini utawala wake tokea mwaka 1978-1989 ndiyo umeifanya nchi ya Uchina kuwa na:
-Mfumo Imara wa Soko la kimataifa,
-Mfumo Imara wa kiuchumi,
-Mfumo Imara wa Siasa ya Chama Kimoja,
-Mfumo Imara na mitaala bora kabisa ya Elimu na
-Mifumo Imara ya Kiulinzi na Usalama (Kuanzia Ujasusi, Ulinzi wa mipaka, Ulinzi wa tamaduni na Udhibiti mzuri wa mali za Ummah)

Japo Majasusi wengi wana nafasi kubwa ya kuwa viongozi wazuri kwenye nchi endapo tu akiwa na kipawa na vinasaba vya Uongozi thabiti.

Tatu, Uongozi wa Vladmir Putin umekuwa na mafanikio makubwa sana na wenye urahisi kwasababu ya mifumo iliyojengwa na watawala wa Urusi kabla yake. Kwenye suala zima la Sayansi na Teknolojia Putin amekuta Urusi imeendelea sana, yeye kazi yake ilikuwa ni kusimamia na kuendeleza kwa uthabiti. Makampuni karibia yote makubwa ya Urusi Vladmir Putin ameyakuta yameshaanzishwa, mfano mzuri:

  • Gazprom (Kampuni kubwa la gesi Urusi) limeanzishwa mwaka 1989 kwenye utawala wa Mikhail Gorbachev.
  • Rosneft (Kampuni la mafuta) limeanzishwa mwaka 1993 kwenye utawala wa Boris Yeltsin.
  • Ularvagonzavod UVZ (Kampuni la mashine na silaha) limeanzishwa mwaka 1936 na Joseph Stalin.
  • Tupolev TU (Kampuni la ndege) limeanzishwa mwaka 1922 kipindi cha Utawala ya Vladmir Lenin.
  • JSC Kalashnikov Concern (Kampuni la silaha) limeanzishwa mwaka 1807 na mfalme Alexander.

Ukimsoma mwandishi maarufu duniani Milan Kundera kwenye Riwaya lake la IGNORANCE anasema kwamba Urusi ni tofauti sana na mataifa ya kifashisti kwasababu mafanikio yake yameunganishwa na tamaduni yao, dini zao na historia yao. Hivyo tofauti na Ujerumani, Italia au Japan ambapo Ufashisti ulikufa mara tu baada ya viongozi kama Adolf Hitler, Benitho Mussolini na Hedaki Tojo kufariki.

Mfano mwingine hai kabisa ni nchi ya Marekani, ambapo Maraisi wengi wamefanikiwa kutokana na mifumo ambayo ilijengwa hata kabla wao hawajazaliwa au kuwepo Madarakani. Mfano Ronald Reagan ndiye raisi aliyefanikiwa sana kwenye historia ya Marekani tangu Vita ya Pili ya dunia kuisha mwaka 1945. Lakini vitu vyote vizuri alivikuta vimeshajengwa muda mrefu sana na yeye kazi yake ikawa ni kusimamia kwa kupitia sera yake ya REAGANOMICS, mfano mzuri tu:

  1. C.I.A ilikuwa na nguvu sana kipindi cha Ronald Reagan lakini ilianzishwa mwaka 1947 na raisi Harry S Truman.
  2. Mifumo bora kabisa ya Kiutawala hapa duniani (Demokrasia, Utawala wa Katiba na sheria, Uhuru wa mahakama na mgawanyo wa madaraka) alivikuta vimeanzishwa na wakina George Washington, Thomas Jefferson, James Monroe, John Adams na Benjamin Franklin kuanzia mwaka 1776 wanapata uhuru hadi mwaka 1787 wanaandika katiba.
  3. Nguvu kubwa ya kijeshi (Military Industrial Complex) imeanza kipindi cha utawala wa Franklin Delano Roosevelt 1933-1945 na kuendelea na Harry S Truman mpaka leo.
  4. Mifumo na Mitaala bora kabisa ya Elimu ameikuta (Vyuo kama Harvard, Yale na Stanford vilikuwepo) alichofanya ni kuboresha tu. Mwaka 1985 Marekani na Japan waliiga mtaala wa Elimu wa nchi ya Urusi ya Kisovieti na kuuboresha kuweza kukidhi mahitaji ya nchi zao.

Nne, Uzembe wa mataifa ya Magharibi yenyewe ndiyo yameifanya Urusi kurudi kwa nguvu. Wakati Urusi inakaribia kuanguka miaka ya themanini mwishoni na tisini mwanzoni kulikuwa na makubaliano baina ya Serikali ya Mikhaili Gorbachev na George Bush kwamba Urusi ingesitisha vita na kuzipa Uhuru nchi kama Poland, Latvia, Estonia na zinginezo ambazo zingependa kujitoa kwenye Jamhuri ya Kisovyeti. Lakini haya yangefanyika tu endapo umoja wa kujihami wa nchi za Magharibi N.A.T.O hautajitanua tu hata kwa Inchi moja wala Sentimeta moja kuelekea Ulaya Mashariki kwenye nchi ambazo bado zina maslahi ya Urusi. Kwa bahati zaidi Mikhaili Gorbachev alikuwa akihudhuria kwenye vikao vya G7 mnamo siku za mwisho za Jamhuri ya Kisovieti na alikuwa akiomba mkopo kwa mataifa hayo ili kunusuru uchumi wa Urusi, lakini tofauti na Ufaransa hakuna taifa lililokubali kumpa mkopo wakati tayari alikuwa ameshakubali kufanya matakwa yao ya kuinganisha Ujerumani kwa Kuvunja Ukuta wa Berlin.

Utawala wa William Jefferson Clinton ulikiuka masharti na kuamua kufanya ubabe kwa kuanza kuitanua N.A.T.O kwa kasi kuielekea nchi ya Urusi ambayo ilikuwa imeshakubali kuweka silaha chini na kutafuta amani. Unakumbuka walivyoanza kuilipua YUGOSLAVIA ambayo kwenye Historia Warusi wanachukulia SLAVS kama ndugu zao wa damu; na kama wewe ni msomaji mzuri utakumbuka kwamba chanzo cha VITA YA KWANZA ya dunia ni pale ambapo URUSI hakukubali kuona UJERUMANI na AUSTRIA-HUNGARY wanaipa masharti nchi ya SERBIA. Mwaka 1914 AUSTRIA ilivyoitangazia vita SERBIA kwa kushindwa kuwapelekea wauaji wa Arch-Duke Ferdinand basi URUSI chini ya Mfalme Nicholas Ramanov waliitangazia vita Austria na yakatoe yaliyotokea mpaka mwaka 1917.

Lakini William Jefferson Clinton na Madeline Albright waliipuuza hii historia na kuanza kuvunja makubaliono waliyowahi kufanya na Gorbachev. Mwaka 1999 nchi za Czech, Poland na Hungary zikajiunga na N.A.T.O na watu wengi walililamika sana akiwemo Gorbachev na Boris Yeltsin lakini U.S.A wakawapuuza. Warusi walichukulia hili kama Usaliti hasahasa pale ambapo N.A.T.O miaka ya 1990's ikiongozwa na Marekani iliamua kufanya uvamizi dhidi ya Jamhuri za YUGOSLAVIA na kuanza kulipua KOSOVO ambayo ni sehemu yenye maslahi makubwa na Urusi pia ndiyo sehemu iliyomfanya Mrusi aingie kwenye Vita ya Kwanza ya dunia mwaka 1914. Hili jambo hadi kijarida cha National Interest wanalaani kwa kusema kwamba haya yalikuwa ni makosa ya kiufundi kwa Utawala wa William, unaweza kujisomea mwenyewe hapa How Bill Clinton Made America More Ambitious—and Dangerous

George Bush Mdogo naye akandelea kufanya ujinga, kaitoa Marekani kwenye mkataba wa ABM (Anti-Ballistic Missile Treaty 1972) na kuamua kutengeneza makombora ya masafa Marefu. Walipoulizwa na Urusi kuhusu hili wakasema na nyinyi tengenezeni kama mnaweza sisi hatuna tatizo. Mwaka 2000 PENTAGON ilipeleka ripoti ya Uchambuzi wa Ulinzi kwa raisi George Bush kwamba serikali ya Urusi hasa jeshi lake lipo hoi, Nchi imechoka na rushwa, utawala mbovu, vita ya Chechenya na Ugaidi. Kama ikiendelea hivyo basi kufika mwaka 2004 Jeshi la Urusi na nchi inaweza isiwepo kabisa hapa duniani kwasababu itakuwa imeshasambaratika zaidi. Serikali ya Marekani wakiongozwa na Media zao wakayaamini haya na kuanza kujifanyia wanayotaka. Nyuma ya pazia Warusi wakaanza kujipanga na kuungana hasa hasa baada ya kujua kwamba Marekani anataka kuwafutilia mbali ya uso wa dunia.

George Bush baada ya kuona Urusi imeanza kuwa na nguvu, Vita za Afghanistani na Iraq zimeenda vibaya na wakati huo huo Uchina anachuana naye sana kibiashara akachanganyikiwa hadi mwaka 2004 bila hata kufikiria madhara yake, akaamua kuziingiza nchi saba zilizojirani na Urusi kwenye Umoja wa kujihami wa NATO. Marekani akavuta mipaka zaidi baada ya kusogea karibu kabisa na Urusi kupitia Georgia mwaka 2008 na tunakumbuka wote nini ambacho Vladmir Putin alimfanya Mikhail Sakhasvilli ambaye alikuwa raisi wa Georgia.

Mjaluo wetu Barack Obama huyo naye kaingia kichwa kichwa huko UKRAINE na SYRIA sehemu zenye maslahi makubwa ya Urusi. Kumbe hakujua kwamba anazidi kuwafanya Warusi wapate sababu ya kujijenga kijeshi mpaka leo hii Marekani inapigwa mikwara na Kremlin ova siyo taifa kubwa hapa duniani. Juzi Henry Kissinger kasema kama Marekani itataka kumshinda Uchina basi ni lazima iunde urafiki na Urusi, na hii ndiyo njia pekee (Hakuna njia mbadala). Hii inamaanisha hata Ujuio na sera za Donald Trump ni mipango ya wakubwa hapa duniani, maana ukiona mtu kama Henry Kissinger anasema Trump anaweza kuijenga Marekani basi Ujue la mgambo limelia.
Hivyo Vladmir Putin kufika hapa alipo pia Ujinga wa mataifa ya Ulaya umechangia kwa kiasi kukubwa Warusi wamuunge mkono Putin na kuona kama ni mwokozi wao kwa wakati kama huu.

Tano, Marekani anazidi kumfanya Vladmir Putin na Urusi wawe na nguvu ya zaidi ya hapa walipo kwasababu hana jinsi nyingine ya kumshinda Mchina isipokuwa kupitia ushawishi wa URUSI tu. Hili amelisema juzi Henry Kissinger ambapo alikiri kwamba ili Marekani iweze kufanikiwa kumthibiti Mchina mwenye nguvu kubwa ya kiuchumi hana jinsi zaidi ya kutumia ushawishi wa nchi ya Urusi. Alisema Donald Trump ni kiongozi ambaye dunia haijawahi kumuona na hivyo basi akijenga mahusiano mazuri na Moscow basi Uchina itapata shida sana kukua kijeshi.

Hii sera kwenye Sayansi ya Siasa inaitwa Divide et Impera ambapo taifa moja linawagawa mataifa mawili au zaidi na kusababisha chuki baina yao ili liwatawale vizuri. Imetumika sana hii sera hapa duniani hasa hasa kwetu Afrika kipindi cha Ukoloni au Ujerumani aliitumia hii sera sana kipindi cha Chancellor Otto Von Bismarck ambapo mataifa mengi yalipandikiziwa chuki ili yatawaliwe kirahisi na nchi ya Prussia ambayo ilikuja kuwa Ujerumani. Kibaya zaidi hii sera Henry Kissinger mwenyewe aliitumia kuwafarakanisha Warusi na Wachina kipindi cha Vita Baridi na bila Warusi kufikiria wakaingia mkenge na mwishowe sera ikazaa matunda mazuri sana. Mwaka 1960's Urusi alianza kuzozana na Uchina na hatimaye mwaka 1969 serikali ya Leonid Brezhnev ailifikiri hadi kutumia silaha za nyuklia dhidi ya Uchina, ambapo waliwauliza Wamarekani ambao walikuwa hawampendi Mchina kwamba tukimpiga Uchina ninyi msiingilie. Wamarekani wakakataa na kuamua kutumia mwanya kumvuta Uchina Upande wake ili kumzorotesha Urusi na Mwishowe kikatokea kitu kinachoitwa SINO-SOVIET SPLIT.

Mwaka 1972 raisi Richard Nixon akaenda hadi Uchina kutembelea Great Wall ambapo alifanya kikao na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Zhou Enlai pamoja na baadae raisi wa nchi hiyo Mao Zedong. Walikubaliana kuanza mikataba ya kibiashara na kufungua masoko yote hii kumkomoa Urusi. Ikumbukwe kipindi hiki sera maarufu ya Uchina moja ( ONE CHINA POLICY) ndiyo ilizaliwa. Ili kumkomoa Urusi serikali ya Marekani ikaamua kutambua kwamba Taiwan ni jimbo halali la Uchina japo linajitawala lenyewe. Ukikumbuka vizuri mwaka huo huo Uchina ilikuwa haina kiti katika baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa mataifa na hivyo Taiwan ndiyo ilikalia hicho kiti pamoja na kupewa kura ya VETO: Lakini mwaka huo kwa mara ya kwanza serikali ya Marekani ikaitambua serikali ya Kikomunisti ya Uchina kama Serikali halali ya nchi hiyo. Ghafla mwaka huo huo Uchina ikarudishwa kwenye Baraza la Ulinzi la Umoja wa Mataifa na kupewa kura ya VETO huku Taiwan ikitolewa. Marekani kamfungulia Masoko Uchina na kuanza kuwasomesha Wachina bure huku Wachina wakianza kukua kwa haraka sana kiuchumi.

Matokea ya hii sera Uchina akaanza kupingana na Urusi sehemu nyingi hapa duniani hadi kupelekea ushawishi wa Urusi kupungua kwa kasi hasa barani Afrika kuanzia miaka ya 1970. Mfano mzuri Uchina alimuunga mkono Muingereza nchini Angola dhidi ya taifa la Urusi na Cuba, kwenye kuvamia Afghanistani Wachina walikuwa upande wa Marekani kinyume kabisa na Urusi tofauti na ilivyokuwa kwenye vita ya Vietnam hivyo kupelekea Urusi kushindwa kujitanua kwa kasi. Mwisho wa haya ni kwamba Urusi ilididimia hadi kufika mwaka 1991 huku Uchina likikua kwa haraka sana. Sasa Marekani amekuwa mkubw na Ukomunisti na Jamhuri ya Kisovieti hazipo, adui mkubwa kwa Uchumi wa Marekani ni Uchina, hivyo basi kipindi hiki Henry Kissinger na wataalamu wengine wanapendekeza kwamba Watumia sera hiyo hiyo ya Divide et Impera na kutengeneza THE SECOND SINO-SOVIET SPLIT. Matokeo yake ni kwamba Urusi na lazima itakuwa na nguvu sana kwasababu Marekani hatampinga sana kwasababu Muungano wa Uchina na Urusi kutoke mwaka 2014-2016 umeleta madhara makubwa kwa Marekani hivyo ni bora hawa wasiwe wote. Donald Trump anawachuki sana Wachina na Kuwakumbatia Warusi, yote hii ni mikakati kwasababu naamini Wamarekani huwa wanafanya sana hesabu ya hatua zao hata kama ni za hovyo.

Putin na Urusi watazidi kuwa na nguvu sana kama sera za Trump na Kissinger zitaanza kutumika kuwagawanya hawa marafiki wawili. Japo sijajua sana kama Uchina wataachana na Urusi au lah, au kama Marekani anaweza kumshinda Mchina kwa hatua alipofika sasa. Lakini yote tisa Urusi akicheza karata yake vizuri anaweza kuwa anakula kotekote Washington na Beijing, hana cha kupoteza kabisa kwasababu mataifa yote haya (Marekani na Uchina) wanahitaji Ushawishi wa Moscow kumshinda mwenzake.

Mwaka 2017-2020 tutaona mengi sana ya Vladmir Putin
.......
Huu ni mtazamo tu Mkuu..............
Tumeanza kuona
 
Back
Top Bottom