herikipaji
JF-Expert Member
- Aug 23, 2016
- 1,198
- 1,364
Mafanikio ya Urusi kwa sasa inayoongozwa na rais mwenye misimamo thabiti aliyekuwa KGB wa zamani Vladimir Vladimirovich Putin ni yakushangaza kwa wengi hasa western block USA na allies wake wa NATO.
Urusi hii nchi ina historia yake ndefu sana na ya kuvutia kwenye vitabu vya historia kwa wale wanaopenda kusoma vitabu ukitafuta utaipata hapa sitaweza kueleza hata humu jamvini wadau wengi wameandika.
Kiufupi miaka ya hivi karibuni ilipitia katika misukosuko ya kiuchumi na kuifanya USA iwe inatamba kwa mikogo na majigambo lukuki na hii misukosuko ilianzia mwanzoni mwa miaka ya 1990 mara baada ya vita baridi kumalizika na kupelekea kusambaratika kwa USSR.
USA na allies wake walichukulia hilo kama ushindi mkubwa sana kwao kwani waliamini huo ni mwisho wa zile nguvu kubwa za Urusi.
Sasa akatokea huyu mtu anaitwa Vladimir Vladimirovich Putin KGB wa zamani ambayo sasa inajulikana kama FSB hawa ni majasusi wa Urusi, aliapa kuiongoza Urusi kuwa na nguvu kubwa kijeshi, Urusi yenye nguvu kubwa na taifa lisiloyumba kiulinzi na kiusalama kuilinda Urusi dhidi ya maadui hasa USA na NATO.
Ameshafanya mengi na amepata mafanikio makubwa katika uongozi wake hadi sasa NATO wanashangaa imekuwaje hawa watu wanakuja tena?(Coming back of Russians.)
Lakini mafanikio na misimamo isioyumba ya uongozi wa Putin vimejengwa kwenye misingi ile ya ujasusi wake aliupata kule KGB, yani uongozi wake upo kiujasusi ujasusi.
Naamsha mjadala tu hapa kuwa kuna uhusiano upi kati ya ujasusi na uongozi hasa tukijenga hoja zetu kwa mfano wa rais wa Urusi Putin.
Majasusi wengi hutumia akili za kiwango cha juu kwenye kazi zao na wanakuwa wazalendo ingawa sio wote mimi huwa nafikiria pia ingesaidia sana hata marais wa hizi nchi maskini za kiafrika wapitie mafunzo ya ujasusi ili kuamsha akili na uzalendo na hatimaye kuongoza mataifa yao na kuushinda umaskini uliokithiri.
Wakuu mwaonaje haya mambo, karibuni kwa hoja.