Ujasiriamali gani huu wa kuvunja ndoa za watu……………………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujasiriamali gani huu wa kuvunja ndoa za watu……………………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Apr 25, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huyu kijana amegeuka kuwa hatari hapa mtaani ninapoishi. Mpaka sasa kuna ndoa kama saba hivi ambazo inaonekana jahazi linaelekea kuzama kutokana na ushushushu wa huyu kijana anayedai eti amejiajiri ili kujikimu na maisha.

  Anachofanya ni kumfuatilia mume wa mtu ambaye anamhisi ni mkware, akishagundua ana nyumba ndogo mahali atahakikisha anajuana na hiyo nyumba ndogo ili apate taarifa za jamaa na ikiwezekana anampiga picha huyo nyumba ndogo kisha anamfuata mke wa jamaa na kujenga naye urafiki na wakizoeana anamweleza kwamba anayo siri kubwa na anaomba ahakikishiwe usalama wake.

  Akihakikishiwa usalama wake anamuuliza mke wa muhusika, kama akimpa taarifa kuwa mumewe anayo nyumba ndogo pamoja na ushahidi atamlipa kiasi gani……………Mke akikubali dili, anamwaga siri zote pamoja na picha na details nyingi tu alizokusanya ili mke aweze kumulika mwizi.

  Akishakabidhi ushahidi anakunja mkwanja wake kisha anasepa na kuacha timbwili nyuma………………Wanawake hapa mtaani wanampenda kweli na wanapeana namba zake za simu. Sasa hivi huyu kijana anatengezeza mkwanja ile mbaya. Ila nimesikia wanaume wanamuwinda ili wamfanyie kitu mbaya……………………..
   
 2. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  aje kitaa tumtoe haja kubwa... maana wengine mabwabwa

  yeye anaangalia upande mmoja tu wa shilingi, haangalii athari nyingine kwa victims
   
 3. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Anachokitafuta atakipata soon
   
 4. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Huyo kuna kitu anatafuta huyo! Subiri uone!
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hiyo fani ni kama amesomea ni intelijensia wa nguvu ..............maana amenunua hata Bodaboda ili imrahisishiea misele yake ya kutaduta data za wanaume wanaosaliti ndoa zao apate kuishi................
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Apr 25, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi, mi nina mtazamo tofauti kidogo. Ingawa kazi yake inaleta majuto na kuhatarisha usalama wa ndoa, lakini pia nahisi kwa kiasi inaweza kusaidia kupunguza ukware wetu sisi vidume wenye kupenda nyumba ndogo.

  Natafakari, labda huyo kijana angetusaidia na sisi wanaume kwa kutupigia uchunguzi wa kina kwa wake zetu ili tuwe na uhakika kuwa hatuibiwi! Mke wangu, kupitia kijana huyo akiwa na uhakika kuwa sina nyumba ndogo na mimi kupitia kwa huyo kijana kujihakikishia kuwa wife hagawi huoni hapo amani itatawala nyumbani? Au aanzishe kampuni kabisa tumlipe kuondoa ukware mtaani ambao ungeweza kutusababishia magonjwa, ugomvi na umaskini? Kuumbuliwa kwa kupenda nyumba ndogo si haki yangu ninayoistahili??! Just joking!!!
   
 7. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #7
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Labda tumshauri awe anachunguza pande zote...........!
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Apr 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,164
  Trophy Points: 280
  Huyu kijana soon tutamuona kwenye mitandao mbalimbali akiwa anachezewa na wahuni. Tabia ya ufitini ni mbaya sana.
   
 9. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #9
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Afungue kampuni ili iwe biashara rasmi, Mtambuzi unaogopa kumulikwa?????

  Hahahahaaaa
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Apr 25, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Ggggrrrrhhh! Mbona kaniwahi huyu! Mi nataka nisajili kampuni kabisa ya cheaters hunters. Mbona hata ulaya zipo hizi dingi? Acheni ukware muwe na amani, usilaumu microscope kwa kukutwa na malaria! Tumia chandarua yenye ngao!
   
 11. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #11
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Wenzetu majuu walirasimisha hii biashara long time,wanaitwa 'private investigators' wana leseni kabisa.Hii njemba ifungue na ofisi kabisa,tena ngoja nimwambie mtambuzi anipe namba ya simu ya mbunifu huyu,kuna mtu anamendea mtu wangu wa karibu humu mmu.
   
 12. PetCash

  PetCash JF-Expert Member

  #12
  Apr 25, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 1,679
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Huyo Jamaa huwa anaweza kufuatilia wanawake na kukusanya data zao kama wana mafiga ya ziada pia?
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Huyu mwanaume ana hatarii.... Ana hatari kwake mwenyewe na hata walomzunguka. Kakazana anatafuta taarifa za waume wanaotoka nje.... nani kamwambia wanawake hua hawatoki kabisa? Anatumia vigezo gani na inamhusu nini? Hata hio nyumba ndogo lazima itatoa details sababu wengi hawana busara na ujinga wake anaweza fikiria kuachika kwa nyumba ndogo ni gurantee ya yeye kuolewa. Huyo hafai kabisaa!
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huyu mimi simfagilii, maana anafanya kama udaku................Kama ingekuwa anafanya hivyo baada ya kuombwa, basi isingekuwa ni jambo la kushangaza.................Lakini huyu anaangalia familia ambazo kipato kipo.........hasa kama mke anafanya kazi aua ni mjasiriamali, hapo anajua kuna dili.............lakini sisi ambao wake zetu ni wauza maandazi na chapati uswazi tumesalimika..............
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  Apr 25, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kwamba itapunguza Ukware? hio ni kudanganyana HP.... Hio ndoa itavunjika.... ikiwezekana mwanaume ataoa tena na atacheat vile vile.... na kwa upande mwingine siamini kua ndoa zote ambazo anachonganisha kweli zavunjika. Ingekua anapeleleza wanawake na kupelekea waume zao sawa! Katka ndoa ambazo zipo hadi sasa ni aslimia zaidi ya 60 ambayo wake imewatokea kujua kua mume wake alichepuka/anachepuka nje ya ndoa.....
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nakwambia Da' AshaDii huyu kijana kalizua balaa hapa mtaani wanume hawa amani na ndoa zaop zimeingia Kidamisi.........Hata zile ndoa zilizokuwa zikipigiwa mfano nazo zimetikiswa maana kidudu mtu keshatia fitna..........Hivi unaweza vipi kukanusha wakati kuna data zote.........Kuanzia picha za huyo hawara, na kama ulipaki gari eneo hilo, utakuta limefotolewa na kama uliwahi kumnunulia vitu mbalimbali zikiwemo samani za ndani kutoka home shopping centre wakati kwako una samani chakavu kutoka keko.................Lazima hapo timbwili liibuke.....................
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huyu ni wa wanawake tu, wanaume hatuna nafasi.................!
   
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Huyu aliangalia jinsia ambayo itapokea idea yake haraka...............wanaume huchukuwa muda kukubaliana na jambo lolote..............Hivi AshaDii kama anakujia mtu kama huyu na mapicha kibao ya hubby wako akijivinjari na nyumba ndogo..........utamsikiliza au utamtimua? (Siombei litokee hilo.........I am just thinking)
   
 19. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #19
  Apr 25, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Anko huyo mtu itabidi uwe makini nae hata ukimsalimia jirani mwema habari zimefika kwa mama nanihii..
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Apr 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Ukosefu wa ajira balaa...unatia kichefu chefu kweli.
   
Loading...