SoC02 Ujasiri wa Mke ukaokoa Ndoa yake

Stories of Change - 2022 Competition

Trump Jr

Member
Jan 19, 2017
26
35
Maisha ya familia mpya huanza kwa uchumba na ndoa.

Kijana mmoja wa kisukuma alipata kufungishwa ndoa na wazazi wake kama tamaduni zetu za kitanzania zilivyo.

Ndoa ilifanyika na kufana, mtihani ulikuja kuanzia siku ya kwanza ya ndoa.

Baba mzazi wa mwanaume alimpatia mtoto wake wa kiume zaidi ya redio akamwambia mkiwa chumbani uwe unasikiliza redio hii, basi kijana wa watu kila siku wakiwa faragha na mke wake yeye hulala mwisho wa kitanda na kuwasha redio yake, anauchapa usingizi mpaka asubuhi.

Siku zikapita, wiki zikakatika mara mwezi mmoja na zaidi, ndipo Mke akaona avunje ukimya kwa kuongea na Mama Mkwe (Mama wa Mwanaume) Mke alianza kwa kusema "Mama naomba nikuambie jambo, mimi tokea mmetufungisha ndoa, mwenzangu hajawahi kunigusa, tukifika ndani yeye analala upande wake na kuwasha redio mpaka asubuhi"

Mama Mkwe akaona jambo hili alifikishe kwa Baba Mzazi ambaye ni mumewe, Mzee wa Kaya alimchukua kijana wake machungani, walipokuwa huko alimuonesha mwanaye jinsi Ng'ombe zinavyopandana, mzee akamwambia "Mwanangu unaona hao Ng'ombe wawili wanachokifanya?" Kijana akajibu "ndiyo"

Mzee akafungua darasa kwa mwanaye huyo (Bwana harusi mpya)... "Tumekuozesha mke, usimuogope, hata mimi nilimuoa Mama yako tukaishi pamoja, tukafanya tendo la ndoa mara nyingi zaidi ndiyo ukapatikana wewe, hivyo mwanangu ukifika chumbani, msogelee mwenzako, mvue nguo zote, mshike shike 'Ndutu, Mabhele' mshike na huku chini kuona kama pamekuwa laini, tayari ufanye kama hao Ng'ombe na mke wako atakupenda sana.

Usiku wa siku hiyo kijana alifuata maelekezo ya Mzee hatua kwa hatua, mpaka nakuletea story hii ya kweli familia ya bwana harusi mpya ina watoto watatu na wanaishi kwa furaha tele.

FUNZO.

Wazazi wa kiume tuwafundishe watoto wetu wa kiume kuishi kiume hata kabla ya ndoa zao.

Mwandishi wako nayeyuka mpaka wakati ujao
 
Back
Top Bottom