Azimio Jipya
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 3,362
- 1,131
Ujasiri na Uadilifu wa uongozi, Ungempelekea Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Kuawachukulia hatua za dhati kabisa mafisadi waliokuwa wamewekwa hadharani na kufahamika waziwazi. Lakini akawa mnyonge, akasita na mdhaifu hadi sasa ameshindwa kuchukua hatua muafaka na sasa umoja wa kitaifa unayumba.
Jamii ya Watanzania ingehemuheshimu Kikwete na kumuenzi kama angechukua hatua hizo za dhati dhidi ya mafisadi na ingejisikia Upendo, Matumaini, kujaliwa na kuwa wamoja na kundeleza mshikamano wa Taifa jambo ambalo ni Mila na desturi ya watanzania, lakini sasa linahatarishwa na mafisadi na kulindana kwao kwa nguvu zote.
Umoja wa kitaifa ambao ungejijenga kwa Hatua za kuridhisha dhidi ya Ufisadi na suala lote la rushwa dhidi ya rasilimali za Taifa ungepelekea uimara na mshikamano wa kiutu, kibinaadamu ambao ndio Utanzania wenyewe!
Ndani ya Umoja huo, mshikamano huo, uzalendo huo, utanzania na utu wa kitaifa mgawanyiko wa KIDINI na KIKABILA ungetoka wapi?
Kwanini tunaelekeza nguvu zetu kwingine na si kwa mafisadi na mbinu zao chafu za kututenga kama jamii iliyoshikana ya Kitanzania kwa faida yao?
Watanzania tuamke tufumbue macho yetu, tutizame na kuona kinachotakiwa kuona... tuone kuwa UFISADI uliokomaa na kujisokota kwenye uongozi wetu ....Unatuyumbisha unhatarisha amani na kuligawa taifa.
Inabidi kuchukulia hatua jambo hili na wala si lingine. Tufanye hivyo sasa!!!