Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Nilifanya kazi kwenye mradi flani katika mradi ule tulikuwa tukilipwa kiinua mgongo kila baada ya miaka mitano na kama unahitajika tena ulichukuliwa kwa mkataba mpya.
Nilipata marafiki wawili wakiume walikuwa marafiki zangu sana. Mara nyingi kiinua mgongo kikilipwa kilisaidia watu katika shida mbali mbali, wengine alipata ada ya kujiendeleza kielimu, wengine walijenga na wengine waliamzisha miradi au kusomeshea watoto.
Marafiki zangu waliamua kuanzisha mradi wa sehemu ya chakula na vinywaji. Walipata nyumba ambayo haijakwisha, waliimalizia kwa makubaliano na mwenye nyumba. Waliajiri supervisor na vijana wengine wa kuhudumia.
Supervisor alikuwa mdada mrembo aliyemaliza form six na kuzungusha. Kumbe bwana wote wawili walikuwa wapenzi wa supervisor na akilalamila kuwa mshahara ni mdogo wote wawili walimuongezea mshahara wakiwa faragha sasa walijikuta wanamlipa mshahara mkubwa kuliko faida wanayoipata
Anguko la biashara lilianzia hapo.