Ujana........!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujana........!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sharo hiphop, Jun 1, 2011.

 1. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nawasalimu wana JF;

  Inapofikia hatua ya ujana wakati mwingine watu wanaweza kuchukulia kuwa ni hatua ya kukutana na changamoto nyingi, hii inawafanya wengi kutofikia malengo mbalimbali waliojiwekea, sasa tujiulize wapendwa, ni kitu gani hasa inawafanya vijana walio wengi kushindwa kukwepa na kuzishinda changamoto hizo?

  Nawasilisha wapendwa.
   
 2. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  ujana maji ya moto, jiangalie utababuka.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Code:
  Inapofikia hatua ya ujana wakati mwingine watu wanaweza kuchukulia kuwa ni hatua ya kukutana na changamoto nyingi, hii inawafanya wengi kutofikia malengo mbalimbali waliojiwekea, sasa tujiulize wapendwa, ni kitu gani hasa inawafanya vijana walio wengi kushindwa kukwepa na kuzishinda changamoto hizo?
   
  Nawasilisha wapendwa.
  Ni umri wenye kulenga kujaribujaribu na kuona ukubwa umewasili kumbe bado kwanza kumepambazuka..............
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Vijana wengi hawafikii malengo sababu hawafatilii yale waliojiwekea tangu awali, utakuta kuna vimpangi miji kibao vinajitokeza katikati wanasahau malengo yao ya awali
   
 5. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwanza hawaweki malengo, na hata wakiweka yanakuwa sio orijino (wanakopi tu kisa wameona fulani nae kafanya). Na kama alivyobandika Ruta, wanajaribu kila kitu (majaribio sio kitu permanent, its temporary), majaribio yanaendelea tu hadi wakigutuka kumeshakuwa jioni wamechelewa na wamesahau kununua mshumaa.

  Kwa kuwa wanafikiri (siku hizi kuna watu wanawafikirisha pia) kuwa wanajua -- ni vijana, ni wa kisasa, hawawezi kueleweka, wana uwezo wa kuamua kwa hiyo waachiwe tu; basi wakubwa pia wamekaa pembeni kumaanisha hakuna mwongozo tena kutoka kwa wazee.
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Mngetoa na ushauri pia namna ya kuuvuka vyema ujana mngekuwa mmesaidia zaidi.
   
 7. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Malengo mengi tunayojiwekea yanakuwa hayafati hali halisi ya maisha, na mfumuko wa mabadiliko ya uchumi pia yanasababisha mtu kubadili malengo yako... unajua unaweza ukawa na malengo yako mara maisha yakabadilika kabisa hapo huna budi ku shift
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Sharo kwa kweli umeuliza swali la msingi sana tena sana,nakupongeza.Sasa ngoja nikumegee.Kwa kuwa unaingia humu JF na kuandika vitu vya maana ina maana wewe sio maimuna,una kaelimu kako na bila shaka una kashughuli ambako kanakuingizia kipato.Sasa nisikilize:
  1.Kama ukijaliwa kupata ajira epuka tamaa.Wako vijana wengi hasa waliopata ajira kwenye mabenki,bandarini na TRA,kwa sababu ya tamaa ya kupata vitu kama blackberry na Nokia torch,toyota markX,kutanua Runaway na kwa JD,jeans za bei mbaya,kununua vidani vya dhahabu na matumizi mengine kama hayo,mara nyingi wamekwapua hela ofisini na matokeo yake wameishia lupango.Kesi kibao za fojare Kisutu zinahusu vijana,watch out,ishi kulingana na kipato chako , epuka tamaa.
  2.Usiwasahau wazazi. Ni rahisi kupata kipato kizuri girlfried mzuri,apartment,gari na mwisho ukajiona umefika.Wazazi wako hata wawe matajiri vipi bado watafurahi ukiwakumbuka mara kwa mara hata kwa zawadi ndogo,baraka zao ni muhimu. Baba,Mama kama unaishi nao karibu siku moja moja watoe for a drink au hata nyama choma,usiwasahau.
  3. Roho yako ikimdondokea msichana usikurupuke kumwoa,take your time maana majuto ni mjukuu na jihadhari usizae kabla hujaoa maana mwisho wake weza kuta una watoto kumi kwa wanawake kumi,tumeyaona haya na wala sio nadharia.
  4. Fanya mazoezi,yatakusaidia uwe na afya nzuri lakini pia huwa yanapunguza muda wa vishawishi.
  5. Jifunze mapema wakati ungali kijana umuhimu wa kutembelea wafiwa,wagonjwa,kuhudhuria harusi za watu etc hii itakusaidia siku za usoni siku yakikukuta.
  6. Kujenga urafiki wa kweli ni kitu kigumu sana,ukimpata rafiki wa kweli mthamini,mtasaidiana kwa mengi huko mbeleni.
  7. Kama wewe ni mkubwa kwenye familia,jitahidi uwe mfano mzuri kwa wadogo zako.
  8. Endapo itatokea ukapata pesa nyingi usiwe na nyodo,maisha ni kupanda na kushuka.
  9.Anza kuweka akiba ungali kijana,itakusaidia siku za usoni.
  10.Wewe ni mtoto wa kiume,hata kama wazazi wako ni matajiri lakini wewe jitahidi ujenge kanyumba kako kwa pesa yako mwenyewe,utajivunia matokeo ya jasho lako.
  Kwa leo naishia hapa ngoja na wana MMU wengine waendelee kukumwagia ushauri.Nakutakia maisha bora yenye fanaka tele!
  Wako,
  Bishanga Abashaija.
   
 9. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,707
  Likes Received: 8,251
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa kabisa ni kumsahau Mungu...! Once you forget your place in ur creator..u r done, uwe mtoto, kijana ama mzee!
  **Speaking from experience!
   
 10. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante sana bishanga, naamini swali hili limekuwa likiwasumbua vijana wengi, kama changamoto naona sasa kwa kufuata huu ushauri na ikitokea kila kijana akaufanyia kazi,
  1. Suala la umasikini halitotajwa tena
  2. Suala la vijana wa mitaani litakuwa kando
  3. Suala la kusema dunia imefika mwisho litasahaulika, kwa sababu tukiangalia ukweli ni kwamba maovu yaliyo mengi husababishwa na vijana. Hii ni changamoto kwetu, na tukubali kwamba kila challenge inakuface ni saizi yako.
  Thanx.
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,673
  Trophy Points: 280
  Asilimia kubwa ya vijana hawana malengo,wapowapo tu!
   
 12. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Afu kwa nini mara nyingi changamoto kubwa wanayokutana nayo na kushimdwa kulishinda hasa ni suala la mapenzi?
   
Loading...