Uingizaji wa mabaki ya kitimoto nchini Cameroon. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uingizaji wa mabaki ya kitimoto nchini Cameroon.

Discussion in 'International Forum' started by Darwin, Sep 2, 2008.

 1. D

  Darwin JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuna sehemu nimesoma kuhusu hii title.

  Wafugaji wengi wa Cameroon wamefilisika kwa kuingizwa kwa wingi nyama ya nguruwe kutoka nchi za Ulaya.

  Nyama zenyewe ni mikia ya nguruwe, masikio, vichwa, utumbo na vitu vingi vya ndani ambavyo watu wa Ulaya hawali bali waafrika.

  Wanavileta Cameroon matani kwa matani nakuuza kwa bei ya chini kabisa kiasi kwamba wafugaji wa Cameroon wanashindwa na ushindani wa nje hadi kufilisika kwani hawana wanakuwauzia nguruwe zao.

  Uingizaji huo wa mabaki ya nguruwe yenye bei nafuu umesababisha kuwakosesha vijana wengi waliokua wanapata ajira kwa wafugaji wa ndani kwa kiasi cha asilimia 67% na wafugaji wengi wa ndani kufilisika.

  Haikushia hapo, nchi za Ulaya sasa zinaingiza pia kuku wa bei rahisi ili kuwamaliza kabisa wafugaji wa ndani.

  Haya wana forum mnalionaje hili?
   
 2. P

  Prince Member

  #2
  Sep 2, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  it is terrible! talk about vicious cycle of poverty ...
   
 3. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Ahhaaaa! nasikitika sana maana najua hata hapa kwetu yatakuja tu. Nimeona nchi za Scandinavia wanazalisha kuku kwa wingi na kwa muda mfupi (wiki moja mpaka mbili) na ukimuona ni kuku mkubwa utadhani ana umri wa miaka saba. Sasa hawa wakimwagwa hapa Bpngo wafugaji wetu si watakwisha kabisa Eeeeee Mungu pitisha mbali hii dhahama.

  Kuhusu k'moto hapa sijui kama tunahitaji kula masazo maana bado tunazalisha wakutosha na bei bado poa. Kwa mwezi huu Mtukufu ndio bei zitashuka maana walaji wengi wamefunga hahhaaaaaaaaaaaaa
   
 4. M

  Mkora JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu hata hapo Bongo ipo sasa hivi yaani mataahira wamerushusu ma apple kutoka south Africa wakati ya lushoto yanaoza bure
   
 5. D

  Darwin JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kama sio masazo yanauzwa kwenye maelfu ya pesa utanunua na uache sijui mikia, utumbo, maini yanayouzwa kwa shilingi mia tu?
  Kumbuka pia wa Cameroon pia japo yakula ambayo sio masazo lakini walikua wanakula nyama bora.
  Kitu ambacho pengine hujakielewa vizuri ni kwamba watu wa ulaya kuna vitu hawali na kwa waafrika wao wanaona ni delikatese.

  Ukimkaribisha mtu wa Ulaya maini basi atakuona umemdharau lakini mtu wa afrika ukimkaribisha anaona umemheshimu.

  Yaani vile wanavyoona havina thamani kwao ndio wanakuja kuwauzia waafrika kwasababu waafrika wanavithamini

  Hio ndio tofauti
   
 6. D

  Darwin JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Yaani huu ni ujinga kabisa.

  Kwa maana hio watu wa Lushoto nao sio muda watakuja filisika kwa kwa utaahira huu.

  Taifa lenyewe linategemea kilimo kwa asilimia kubwa, sasa wale wauzaji wa mazao yakawa na ushindani na wakakosa kuuza si ndio hapo hali za maisha zitazidi kudidimia.

  Kumbuka kwamba
  Mkulima wa Lushoto kama hapati faida basi hata mpa ajira mtoto wa jirani aje kuchuma ma apple. ma jobbless ndio watazidi kuongezeka.
  Watu wa malori nao watakosa kazi kwani hawataenda kuchukua matunda Lushoto.

  Uchumi wa nchi utaendeleaje hapo? waliosoma uchumi wanifafafanulie
   
 7. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2008
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160

  Jana nimemskia Bw. Luhanjo alipotemebelea Mlimani City kati ya mambo ambayo ameyaongelea ni pamoja na kukanusha kwamba wamiliki wa Mlimani City hawajakataa kununua bidhaa (mazao) za ndani, bali wanaagiza kutoka Afrika Kusini baada ya bidhaa za ndani kushindwa kutoshereza mahitaji ya supermarket yao yaani Mlimani City. Wazee hiyo imekaaje? Tunakubaliana na maneno yake hayo?
   
 8. D

  Darwin JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Kuleta bidhaa kutoka nchi za nje sioni kwamba ni tabu kama wana uwiano wa bei.
  Kwa maana hio wazalishaji wa ndani wasipate ushindani mkubwa mpaka kufilisika.

  Kwa maana hio hizo bidhaa za nje zisiwe cheap kushinda za ndani.

  Kila mtu anataka urahisi lakini kama bidhaa zetu tunazozalisha hazinunuliwi kutokana na bidhaa za nje ni rahisi hapo ni dhambi
   
Loading...