Uingereza yapunguza bajeti Tanzania

andrewmitchell.jpg

Andrew Mitchell
  • YATOA ASILIMIA 30 KWENYE FUNGU LA BAJETI
SERIKALI ya Tanzania imepata pigo kiuchumi baada ya Uingereza kupunguza msaada wake katika fungu la bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/12 kwa asilimia 30, Mwananchi Jumapili limebaini. Hatua hiyo ya Uingereza kupitia Idara ya yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID), imekuja wakati nchi wahisani zinazochangia bajeti ya serikali (GBS), zikisema zitapitia misaada ya fedha wanazotoa ili kujua kama serikali imefikia malengo yaliyokusudiwa. Jumla ya Washirika wa Maendeleo (DPs) 12 wanasaidia bajeti ya Tanzania, ambapo kwa mwaka huu wa fedha, nchi hizo zilitoa kiasi cha Dola 453 milioni.

Hata hivyo, katika mchango wao wa bajeti ya mwaka huu wahisani wamezuia kiasi cha Dola 100 milioni( karibu Sh170bilioni) ambazo zitatolewa iwapo nchi hizo zitaridhishwa na utendaji wa Serikali katika maeneo mbalimbali. Katika mwaka wa fedha 2010/11 nchi hizo zilitoa Dola 534 milioni ( karibu Sh907.8 bilioni) kuchangia bajeti ya serikali.

Hatua ya kuzuiwa kwa kiwango hicho cha msaada wa Uingereza kwenye bajeti inatokana na serikali kushindwa kusimamia vizuri masuala mbalimbali, kubwa ikiwa ni mazingira ya uwekezaji na kupambana na umasikini, kwa mujibu wa Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza, Andrew Mitchell. Mitchell katika barua yake ya Agosti 3, 2011 kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Uchumi ya Bunge la Mabwanyenye la Uingereza (House of Lords), amesema mawaziri wa Uingereza na serikali yake kwa ujumla wamekuwa wakisisitiza Tanzania kuimarisha mazingira ya kufanya biashara kama njia muafaka ya kupunguza umasikini............

zaidi soma gazeti Mwananchi

RAIS wetu anajua misemo, nahau na methali nyingi sana za Kiswahili. Nashindwa kuelewa kwanini methali ya MTEGEMEA CHA NDUGUYE HUFA MASKINI haimo kichwani mwake! Ukizingatia zaidi hawa wahisani WALA SIO NDUGU ZETU(ni jamaa tuu) si tumekuwa sawa na kujikaanga kwa kutegemea asiyetegemeka?

Sasa wacha tuone albakadabra gani Mkulo and Company wataibuka nayo kuokoa jahazi. Ila kwa mtazamo wangu kama tulikuwa tunakula shubili, sasa tujiandae kwa kilichokichungu zaidi katika uchumi wetu na gharama za maisha ya kila siku! TWAFWA!
 
Afadhali af ndio wanaotudumaza wakati nchi inaouwezo na maliasili za kutosha ikiwezekana wasitupe kabisa tufe na njaa ndo tutajifunza khaa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom