Uingereza sio wajinga

Uingereza sio wajinga

dorge

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2025
Posts
235
Reaction score
365
Ndg kwa ufupi niliachaga kitambo mambo ya siasa za nchi hii.
Kwa nini.
1. Siasa ni kwa ajili ya viongozi na familia zao.
2. Siasa ni kwa ajili ya matajiri vs wanasiasa.
3. Maskini kaa sibiri mwisho wa uhai wako.
4. Waliotimkia majuu wanabahati maana wameepuka dhahma.
5. Ahadi nyingi za wanasiasa ni uwongo,
6. Waliokatika nafasi za management wanazuia wananchi wasiwasimbue viongozi. Na ukiongea sana unaondolewa.
7. Wananchi wanaoongea sana wanapotezwa.
8. Wazungu wanahakikisha nchi au taifa lenye mali kama mafuta, madini mfano Kongo wanayachukua.
9. Nimeona nikae niishi maisha haya ya sh 100 kukiko fedheha. Nshio maana maprofesa, wame mute. Madaktari wameamua kuhamia bungeni.
10. Ikiwa msomi bongo ni adhabu Bora machinga na bodaboda maana haelewi mielekeo wa taifa
 
Hata ukae pambeni, kandokando, pembezoni popote utakapokaa siasa zinakuhusu utake usitake upende usipende ujihusishe usijihusishe. Ukisema ufanye umachinga wanasisa watakupangia pa kufanyia umachinga wako utaki virungu kama mbwa koko vitakuhusu mpaka utakapo fuata anavyotaka mwanasiasa, ukienda kwenye ufugaji atakuja huko na alama kwa mifugo hutaki virungu na faini juu.

Kwenye kilimo mwanasiasa anakuja fasta kukupangia namna ya kuuza tumbaku zako korosho, kahawa, ufuta, mahindi anavotaka yeye hutaki unakamatwa kwa utoroshaji mazao.

Kwenye uvuvi atakuja huko kukupangia namna ya kuvua, atafunga ziwa au bahari kwa kipindi fulani hutaki unakamatwa kichapo fine na kifungo juu unafanya uvuvi haramu sasa ndg yangu siasa utazikwepea wapi? Siasa ni maisha yetu kwa ujumla wake. Utake usitake labda ufe, Ukisema ujiue ukikutwa kabla hujafa ukaokolewa mwanasiasa alishatunga sheria ufungwe jela kwa kutaka kujiua wakati maisha ni yakwako wewe. Hapana chezea siasa ni zaidi ya ugali bwana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom