Uingereza kwanini haikuishambulia Urusi?

Uingereza kwanini haikuishambulia Urusi?

Uingereza na washirika wake USA na Ufaransa wanadai ukitumia silaha za kemikali lazima wakuadabishe kwa mashambulizi ya kijeshi. Kama ni hivyo kwa nini hawajaishambulia urusi kwa kuwa wanadai imetumia silaha za kemikali kujaribu kumwua yule jasusi ndumila kuwili akiwa uingereza kama walivyofanya Syria? Karibuni wadau tudadavue!

Wewe ni mchokozi....hahahahahhaha...jibu lake unalijua...Si Uingereza wala Ufaransa na hata Marekani anayeweza kuingiza pua yake Russia...Uingereza ikithubutu iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi chini ya dakika tani itakuwa majivu..hakuna kiumbe chochote kitakachobaki hai pale kwenye visiwa vya UK...
 
Kumpiga mrusi sawa na kujinyonga mwenyewe,hiyo ni hatari juu ya hatari,ni nchi 2 ambazo hizipigiki,merekani na urusi
 
acheni mambo yenu jamani world cup ipo karibu
 
Ni swali la msingi sana,kama anamshambulia Syria kwa kutumia sumu kwa watu wake,kwanini asimshambulie Russia katika ardhi yake kwa kutumia sumu katika ardhi ya UK?Anaishia kufukuza mabalozi?Kwanini asijaribu kupiga kombora hapo Moscow aone mziki wake?
 
Hakuna nchi yeyote Duniani ....labda Mungu mwenyewe ndiye atakae weza.....kushambulia hizi nchi ( U.S.A.., Russia, ) shambuliz lolote maana yake ni kwamba nusu ya ramani ya dunia itabadilika watachokozana tu na si vita vya moto.....
 
Uingereza na washirika wake USA na Ufaransa wanadai ukitumia silaha za kemikali lazima wakuadabishe kwa mashambulizi ya kijeshi. Kama ni hivyo kwa nini hawajaishambulia urusi kwa kuwa wanadai imetumia silaha za kemikali kujaribu kumwua yule jasusi ndumila kuwili akiwa uingereza kama walivyofanya Syria? Karibuni wadau tudadavue!

Hahahaaa wajaribu waone 😀😀
 
Back
Top Bottom