Uingereza haikumtendea haki Rais Kikwete

Status
Not open for further replies.
David Cameroon anaisupport chadema kwa hiyo hawezi kuisaliti kwa kukutana na mwenyekiti wa CCM.....

Steven O'brien (kwenye picha na rais) unafikiri anatoka chama gani? na anafuata sera gani?

NB: kwenye blogs rais anaonekana anaongea na wakuwa wa British Gas! Kwa hiyo trip ilikuwa na manufaa.
 
Rais wetu mpendwa, Mkuu wa nchi, Amiri Jeshi, Mwenyekiti wa Chama tawala!!!!!!!!!!!!!??????????????
Sijafurahia kabisa the way walivyom-treat rais wetu.
Amekwenda kuitembelea Uingereza, alitakiwa alakiwe na Mwenyeji wake Waziri Mkuu au Malkia! Lakini cha ajabu Rais wetu mpendwa alikwenda kulakiwa/kupokewa na naibu waziri wa maendeleo wa kimataifa! ??????????????
Not fair at all!
Unajua kama wamemchoka rais wetu wasema tu kuliko kumtendea wasivyopenda na wao kutendewa!

uingereza5.jpg

Naibu waziri wa mambo ya kimataifa wa uingereza Stephen O'brien akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu, ndg Jakaya Kikwete.

Mungi,
Nafikiri hujui masuala ya protocol kwa nchi ya Uingereza. PM haendi airport kupokea wageni wake. Nitafutie hata picha moja ambayo rais wa nchi amepokelewa na PM airport. Kiongozi yeyote anapofika hupokelewa na watu wa ubalozi wa nchi yake pamoja na viongozi wa wizara ya mambo ya nchi za nje.

Nchi kama UK muda wote inatembelewa na wageni mbalimbali ambao wanapita wakiwa kwenye safari zao au wanakuwa wamealikwa kwenye mikutano inayofanyika UK au wanakuwa kwenye state visits.

Hizo aina zote tatu zina protocols zake ambazo zinatofautiana. Kwa mfano kama ni state visit basi huyo ni mgeni wa Malkia na mara nyingi airport hupokelewa na watoto wa malkia, kwa mfano Obama anaweza kupokelewa na prince Charles na viongozi wa serikali wanakuwepo lakini sio PM. Marais wengine wanapokewa na watu hata wa chini zaidi.

Kama ni safari ya kikazi tu na kuonana na PM basi hupokelewa airport na viongozi wa ngazi za chini na kisha huenda Downing street no. 10 kwenda kuonana na PM.

Kama ni mikutano hii mingine ya kimataifa sio lazima hata kuonana na PM. kwa mfano huu mkutano wa juzi uliandaliwa na Melinda Gates. Yeye ndiye alikuwa mwenyeji wa huo mkutano. JK na Cameron wameonana kwenye mkutano huo. Ingelikuwa cameron hahudhurii pia huo mkutano wala wasingeonana kabisa.

UK karibu kila siku kuna viongozi wanapita. ingelikuwa kila mmoja anapokewa na PM basi huyo PM asingelifanya kazi kabisa.

Hii safari JK hakualikwa na Uingereza, hivyo kulikuwa hakuna hata haja ya kukutana na viongozi wa serikali ya Uingereza. Mara nyingi viongozi wa kitaifa wakiwa hapa, basi hawa mawaziri wanatumia nafasi hiyo kukutana nao, kuwapa briefings na pia kujadilia mambo mengine ya kimataifa.
 
Anajitakia mwenyewe kila root awepo,mikutano mingine ni ya mawaziri yeye anakwenda,ndio maana amepokelewa na naibu waziri maana haukuandaliwa na kiongozi wa nchi.
 
"Root out the corrupters,the corruption will follow and chaos averted" hii gvnt ya CCM wafuate hii ki2 kupunguza malalamiko ya wananchi! Ss wana ujasiri huo??? Lets pray, 'Our Father......deliver us from ever evil.AMEN!!
 
Mkuu unaumia bure kumtetea JK. Mbona akienda mikoani anapokewa na wanafunzi wa primary za kata tena wanalazimishwa kushinda juani kumsubiri badala ya kusoma.

Thamani yake imeshuka mkuu. Asikiaye na afahamu
 
Sijafurahia kabisa the way walivyom-treat rais wetu.

Unajua kama wamemchoka rais wetu wasema tu kuliko kumtendea wasivyopenda na wao kutendewa!

.
We waona ivo mwenzio anaona kaula,
Yuko mamto,
Inglish Kozi inamtoa mbele ya wazungu!
Cheki tabasamu lake?
 
Rais wetu mpendwa, Mkuu wa nchi, Amiri Jeshi, Mwenyekiti wa Chama tawala!!!!!!!!!!!!!??????????????
Sijafurahia kabisa the way walivyom-treat rais wetu.
Amekwenda kuitembelea Uingereza, alitakiwa alakiwe na Mwenyeji wake Waziri Mkuu au Malkia! Lakini cha ajabu Rais wetu mpendwa alikwenda kulakiwa/kupokewa na naibu waziri wa maendeleo wa kimataifa! ??????????????
Not fair at all!
Unajua kama wamemchoka rais wetu wasema tu kuliko kumtendea wasivyopenda na wao kutendewa!

uingereza5.jpg

Hii siyo official visit! ni lazima ujue kutofautisha. Hajaalikwa na Prime minister bali na shirika kwenye mkutano!

Mkuu, unachosema ni kweli kabisa.
Lakini ki-protokali kiongozi mkuu wa nchi akienda nchi yoyote hata kama hakualikwa hupokelewa kwa heshima zote, refer kama una kumbukumbu bila shaka mwaka fulani (samahani siukumbuki lakini ni 1970s) nduli Iddi Amin alijialika mwenyewe katika mkutano wa Commonwealth, London. Lakini ilibidi apokelewe na kupewa ulinzi stahiki kama kiongozi wa nchi!!!???

Sina uhakika kama Mhe. Rais JK hakupewa heshima hiyo. Kama ndivyo ni bad implication.
 
Watanzania wakati mwingine tujalipu kupunguza majungu.Waswahili wanasema siyo kosa kutokujua jambo lolote lakini ni kosa kwa kudhani unajua kumbe haujui.Kwa msaada kidogo wako kidogo, Kiongozi wa juu wa nchi yoyote anapotembea Uingeleza safari yake inaangukia kwenye kundi moja kati ya makundi matatu. Makundi hayo ni State visit, official visit na personal visit.
Ni viongozi wachache sana ambao wameishapewa state visit na malkia wa Uingeleza kwa sababu visit hii niya kiwango cha juu kabisa nchini.
Wataalamu wa maswala ya siasa wanasema, sababu nyingine kuwa Familia ya malkia kuwa hawapendi kutoa mwaliko ni kuogopa kujishusha kutokana na silka zao za kitemi.
Viongozi wengi huwa wanapewa official visit ambapo mkuu wa nchi(Malkia) hajihusishi kabisa katika visit hata kama kiongozi aliyealikwa atakwenda kuonana na Malkia. Na katika official visit, inategemea kiongozi aliyealikwa anakuja kwa maswala yapi na anaandamana na watu gani.
Kikwete amekuja kwenye London summit on family planning kwa mwaliko wa serikali ya Uingeleza kupitia department for International development na Bill & Mellinda Gates foundation kwa hiyo siyo ajabu mwenyeji wake kuwa ni Andrew Mitchell ambaye ndiye mkuu wa idara na famili ya Bill Gates. Ikumbukwe Raisi ameamua kuja kwa sababu Tanzania ni kati ya nchi chache za Africa zinazonufaika sana na mpango huu. Pia ameamua kuhudhulia kwa sababu Bill Gates ni rafiki yake sana na bila kusahau Kikwete anaangalia maisha yake ya baadaye katika majukwaa ya kisiasa baada ya muda wa Uraisi kuisha.
Kama Kikwete atamua kuja tu kutembea au kuwaona rafiki zake, hiyo itakuwa ni personal visit na hakuna kiongozi wa juu atakaye shughulika kiserikali pamoja na kuwa serikali ya Ungeleza lazima ijue kama kuna kiongozi fulani wa nchi. Tatizo ni kuwa viongozi wetu wakati wote wanaishi kiutawala tawala na hawana muda wa kuwa na maisha ya kama mtu wa kawaida.
 
d3.jpg

AAAaaahhh mbona wazushi nyie. Mheshimiwa peke yake ndio yuko karibu na Waziri Mkuu. Kagame yuko nyumaaaaaaa, Museveni yuko pembeni ya JK mbali na Waziri mkuu. Jamani tuache majungu. Mnashusha hadhi ya hii JF. Badala ya kuwa home of great thinkers inakuwa home of gossipers. shame on you!
 
Kwani picha hii ni mazungumzo au ni makaribisho.
Walikuwepo marais watatu toka Afrika. Kagame katoa hotuba kuu. Museven kaelezea jitihada zake kwenye uzazi wa mpango. Kikwete sijamsikia. Maybe he was busy thinking how much will be his cut in the USD 560m pledge by Melinda Gates
 
Waingereza wengi wanamsema hivi
"Tanzania’s Jakaya Kikwete, re-elected to a second term last year, will step down in four years. Hobbled with the reputation of a lazy, foreign-trip-loving president who is soft on corruption, Kikwete seems to be busy sprucing his image.

Amidst signs that the long-ruling Chama Cha Mapunduzi is in the midst of a shake-up, Kikwete has been pushing some of the more controversial and scandal-tainted politicians off the cliff, or a few of them have saved themselves the humiliation and jumped

Na wengine wanamsema hivi

Tanzanians are tired of their president. A retarded womanizer, brain dead idiot constantly trotting the world leaving his country in the darkness. His people pray for an African version of Arab spring to topple jokers like him.

Wikileaks revealed how cheap Kikwete is; a whole head of state being bribed 5 suits and $1million.

How low? He is accused of being the master of all corruption. Never home attending even the most mediocre meetings his assistants could attend. They have even named him after the explorer "Vasco Dagama".

Africans will never progress as long as the likes of Kikwete keep on leading Africa''.

Wewe ni hayawani kama siyo kichaa. Huwezi kuja na maandiko kama haya juu ya Raisi ama mkuu wa nchi. Huu ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Kupewa uhuru wa habari isiwe kibali cha kumtusi Raisi, sikubaliani na wewe hata kidogo katika hili.

Mnaosema Jakaya Dhaifu mnapenda awe dikiteta kwa muda wake uliobaki madarakani?, mtaweza kuhimili udikiteta ama mnasema tu?. Jakaya ana polisi, ana jeshi, ana TISS, ana mahakama na uwezo wote bado mnasema ni dhaifu?.
 
Mungi,
Nafikiri hujui masuala ya protocol kwa nchi ya Uingereza. PM haendi airport kupokea wageni wake. Nitafutie hata picha moja ambayo rais wa nchi amepokelewa na PM airport. Kiongozi yeyote anapofika hupokelewa na watu wa ubalozi wa nchi yake pamoja na viongozi wa wizara ya mambo ya nchi za nje.

Nchi kama UK muda wote inatembelewa na wageni mbalimbali ambao wanapita wakiwa kwenye safari zao au wanakuwa wamealikwa kwenye mikutano inayofanyika UK au wanakuwa kwenye state visits.

Hizo aina zote tatu zina protocols zake ambazo zinatofautiana. Kwa mfano kama ni state visit basi huyo ni mgeni wa Malkia na mara nyingi airport hupokelewa na watoto wa malkia, kwa mfano Obama anaweza kupokelewa na prince Charles na viongozi wa serikali wanakuwepo lakini sio PM. Marais wengine wanapokewa na watu hata wa chini zaidi.

Kama ni safari ya kikazi tu na kuonana na PM basi hupokelewa airport na viongozi wa ngazi za chini na kisha huenda Downing street no. 10 kwenda kuonana na PM.

Kama ni mikutano hii mingine ya kimataifa sio lazima hata kuonana na PM. kwa mfano huu mkutano wa juzi uliandaliwa na Melinda Gates. Yeye ndiye alikuwa mwenyeji wa huo mkutano. JK na Cameron wameonana kwenye mkutano huo. Ingelikuwa cameron hahudhurii pia huo mkutano wala wasingeonana kabisa.

UK karibu kila siku kuna viongozi wanapita. ingelikuwa kila mmoja anapokewa na PM basi huyo PM asingelifanya kazi kabisa.

Hii safari JK hakualikwa na Uingereza, hivyo kulikuwa hakuna hata haja ya kukutana na viongozi wa serikali ya Uingereza. Mara nyingi viongozi wa kitaifa wakiwa hapa, basi hawa mawaziri wanatumia nafasi hiyo kukutana nao, kuwapa briefings na pia kujadilia mambo mengine ya kimataifa.

Kwahiyo O'brien ambaye ni naibu waziri ndiye aliyestahili kumpokea mkuu wa nchi yetu?
 
Mkuu tunashukuru kwa ufafanuzi wako murua.

Rais Jakaya Mrisho kikwete, Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na mkewe Mama Janet Museveni, Waziri Mdogo wa Uingereza wa Maendeleo ya Kimataifa Bw. Stephen O'Brien (kulia) na Mama Melinda Gates, wakibadilishana mawazo kabla ya kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012.

kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020. PICHA NA IKULU

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani, katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.

mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman (wa pili kulia) na maafisa waandamizi wa kampuni hiyo. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
 
Mungi acha uongo JF sio sehemu ya porojo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mdogo wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Bw. Stephen O'Brien jijini London, ambapo Uingereza iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuendeleza sekta ya nishati hususan utafutaji wa gesi asilia.
 
Rais wetu mpendwa, Mkuu wa nchi, Amiri Jeshi, Mwenyekiti wa Chama tawala!!!!!!!!!!!!!??????????????
Sijafurahia kabisa the way walivyom-treat rais wetu.
Amekwenda kuitembelea Uingereza, alitakiwa alakiwe na Mwenyeji wake Waziri Mkuu au Malkia! Lakini cha ajabu Rais wetu mpendwa alikwenda kulakiwa/kupokewa na naibu waziri wa maendeleo wa kimataifa! ??????????????
Not fair at all!
Unajua kama wamemchoka rais wetu wasema tu kuliko kumtendea wasivyopenda na wao kutendewa!

uingereza5.jpg

Naibu waziri wa mambo ya kimataifa wa uingereza Stephen O'brien akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu, ndg Jakaya Kikwete.

Kuna wimbo juu ya mgeni katika hadithi za zamani; MGENI SIKU YA KWANZA MKARIBISHE KWA MAMBO YOTE MAZURI; IKIFIKA SIKU YA KUMI MTIMUE KWA MATEKE NA MAGUMI.........

Mgeni baadaye ukizidisha UGENI UNAKUWA KERO!!!!!!
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi akiongea na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kimataifa wa Uzazi wa Mpango katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London Julai 11, 2012. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Bi Josephine Mwankusye na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Afya ya Mzazi na Mtoto katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt Neema Rusibamayila.
 
Ni kama Cameruni aje hapa afu anapokelewa na kuwa hosted hadi anaondoka na naibu wa Membe.
Kikwete anakuwa hajui kabisa!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom