UINGEREZA: Gari lagonga watu kadhaa London

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,472
2,000
_96543286_76bf2c74-7686-4a2b-a7e2-c5986dd375b5.jpg

Mtu mmoja ameuawa na wengine wanane kujeruhiwa baada ya gari kugonga umati wa watu waliokuwa wakitembea karibu na msikiti kaskazini mwa London.

Mwanamume mmoja wa umri wa miaka 48 alikamatwa kufuati kisa hicho.

Polisi wa kupambana na ugaidi wako eneo hilo. Polisi wamelielezea tukio hilo kama la kigaidi.

Waziri mkuu Theresa May amekitaja kuwa kisa kibaya akisema kuwa fikra zake ziko kwa wale waliojeruhiwa, wapendwa wao na watoa huduma za dharura eneo hilo.

_96543285_4a2d3b73-aff1-4f96-9e58-137d0c622c96.jpg

Idara ya kutoa hudum za dharura mjini Lanodn imesema imetuma huduma kadha eneo hilo.

Video iliyowekwea katika mitandao ya kijamii ilionyesha vurugu huku watu wakiwasaidia wale waliojeruhiwa.

Tayari mtu moja amekamatwa kufuatia shambulio hilo lililotokea katika wilaya ya Finsbury Park.

Baraza Kuu la Waislamu nchini Uingereza limesema kuwa walengwa wa tukio hilo walikuwa ni waumini, huku majeruhi wengi wakiaminika kuwa ni wale waliokuwa wamemaliza tu kuswali swala ya jioni baada ya kuumaliza mfungo wa siku wa Ramadhan.

Video zilizotumwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha watu walio katika taharuki, kuhu wakijaribu kuwasaidia majeruhi.

Chanzo: BBC
 

magis

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
390
1,000
Unajua kufikiri kukifika mwisho utaweza vua nguo hadharani ukadhani pia ni haki yako.
Nashindwa kuelewa ni kwa jinsi gani watu wanaoitwa "MAGAIDI" mnawafungamanisha na UISLAM wakati tayari umeshasema hao ni aina ya watu wasio na huruma/haya.
Uislamu unakataza watu kuwatoa roho wenziwao,hawa ni wauwaji wanakuwaje waislam.
Hebu tuwe na chuki kisha tuseme ukweli.
Kuna madhehebu yanaruhusu ushoga ndio tuwaite wote wanaofuata dhehebu hilo ni watu wa aina hiyo.
Tumuogope Mungu,tusimsingizie asiyoyaagiza ili tukikutana naye tusiwe wa kutafuta pa kuweka nyuso zetu.
Hakuna ktk dunia bali ni mapito tu wapendwa.TUPENDANE,tusiwe wepesi wa kutamka maneno yaumizayo wengine.
 

kipuyo

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
1,605
2,000
Waliogongwa ni waislamu acha chuki
Sio chuki ila ndo uhalisia,kwani wanaouawa Somalia wote sio waislamu
wanaouawa Kaskazini mwa Nigeria wote sio waislamu?
Je wale waliopo Syria,Afghanistan,Iraq na Pakistan wote sio waislamu?
Magaidi mnauana wenyewe kwa wenyewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom