HoodRich
JF-Expert Member
- Sep 13, 2015
- 208
- 66
Wadau naandika makala juu ya Uhusiano wa Lowasa,kikwete na hatma ya CCM.
Naomba mawazo jinsi ya kuweka kichwa cha habari!
Ni hilo tu!
Andika title " kikulacho kiko nguoni mwako "
Wadau naandika makala juu ya Uhusiano wa Lowasa,kikwete na hatma ya CCM.
Naomba mawazo jinsi ya kuweka kichwa cha habari!
Ni hilo tu!
vipi hao wengine aliowapa madaraka ki uswahiba unelezeaje hilo mkuu
Fisadi Anayejikomba Kwa Rais Wa Watu,
Kichwa cha habari chafaa kiwe UNAFIKI ULIVYOVUNJA URAFIKI WA LOWASSA NA JK.
Sababu Lowassa alimpenda,kumuamini na kujitolea kumsaidia rafiki yake lakini rafiki akamtenda na kumdhalilisha.
Lakini Mungu mkubwa,leo hii Lowassa anaonekana shujaa na mfano wa kuigwa tofauti na mwenzie.
jk hata siku lowasa anajiudhulu alimtetea kuwa hiyo ilikua ajali ya kisiasa tu a hata katika uchaguzi mkuu uliofuata alimnadi lowasa.....
sasa fikiri hata wewe rafiki yako unakuja gundua kuwa kumbe ana plan kukupindua kwenye madaraka kwa kutumia hila,utaendelea kuwa nae karibu?....
lowasa alikosea sana kutaka kuwatumia wajumbe wa mkutano mkuu kumvua kikwete umwenyekiti wa ccm...
hadi hapo jk alikua hajamfanyia kitu kibaya lowasa na alichaguliwa hadi kuwa mwenyekiti kamati ya bunge ya ulinzi bila jk kumwekea mizengwe...
sasa hapo utamlaumu vipi jk.....?
Mkuu unaweza kutusaidia,kuna uhusiano wowote kati ya Richmond na bifu la Lowasa na Jk.
Je,zoezi la mapinduzi kwa kutumia wajumbe lilifanyika lini?
Maana mimi nilisikia zoezi hilo lilikuwa lifanyike kwenye mkutano wa kupitisha majina
mie kila siku hujiuliza,hii manenp kuwa lowasa alimsaidia jk kupata urais huwa inatoka wapi....
nachokumbuka hawa jamaa wawili mwaka 95 walikodi ndege pamoja kwenda kuchukua form za urais....
lowasa akakataliwa na kambarage kuwa hafai.
jk akaambiwa bado umri mdogo asubiri.
jk kasubiri kwa miaka kumi mpaka 2005 ndo kagombea,sikumbuki kama mwaka huo lowasa alichukua form,lakini kama alichukua itakuwa alikatwa mapema.
katika mchuano jk akapita,nakumbuka kipindi hicho kikwete alikua na uungwaji mkono sana tu ,na wala kampeni zake hazikuwa za kulazimisha kwa mapesa,alikua anapambana na kina mbowe,lipumba na mapesa,wote hao alikuwa kawaacha mbali mno.
sasa huwa najiuliza,huo msaada wa lowasa kwa jk ni upi huo,mbona huwa hauwekwi wazi???
kwa ulichokiandika hapa, nimekupuuza, hujuichochotee
Amini Amini nawaambia Jk na El still are friends..El kuja CDM ipo well planned by both..Jk mwenyewe hazipendi figisufigusu za miccm maslai ambayo ndo yaliyompoteza Jk mpaka kasi na hali mpya ikakwama akajiamulia awe anapiga trip za ulaya tu..Jk also need changes..mark my words guyz
Mkuu unaweza kutusaidia,kuna uhusiano wowote kati ya Richmond na bifu la Lowasa na Jk.
Je,zoezi la mapinduzi kwa kutumia wajumbe lilifanyika lini?
Maana mimi nilisikia zoezi hilo lilikuwa lifanyike kwenye mkutano wa kupitisha majina
hakuna uhusiano wa jk na lowasa na bifu la richmond...
richmond ilikua ni irregularity katika kugawa tenda za kampuni ya kufua umeme,na edward lowasa aliwajibika kwa kujiuzulu kama bunge lilivyotaka.
na hata katika maneno ya mwanzo ya lowasa baada ya kujizulu alisema kuwa alichukua UAMZI MGUMU katika kuipa kipaumbele richmond juu wananchi walikua wanahitaji umeme kwa haraka.
kuhusu mapinduzi ya kumng'oa jk umwenyekiti,kila mtu aliona kwenye tv manuva yaliyotokea hadi njama zikajifia,au haukufuatilia,kuna nyuzi humu za kipindi hicho,tuliongelea..
tatizo jf sijui archieve yao iko wapi