Uhusiano wa Kifedha Kati ya UK na EU Kuzorota.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
16ab9dd0606532a8a8df102cea870b40.jpg

Rais wa nchi za umoja wa Ulaya wanaotumia sarafu ya Euro, Jeroen Dijsselbloem, amesema sasa taasisi za kifedha za Uingereza zitakuwa na mahusiano machache tu na zile za kifedha za muungano wa Ulaya baada ya taifa hilo kuondoka rasmi kutoka kwa jumuiya hiyo.

Bw. Dijsselbloem amekiambia kituo cha televisheni cha uholanzi kuwa hali hiyo itayalazimu baadhi ya makampuni kuhama mji wa London.

Waziri wa fedha wa uholanzi kwa upande wake amesema anatarajia miji ya Frankfurt na Amsterdam kufaidika kibiashara kutokana na msukumo huo utakaojiri wa biashara kulazimika kuhamia kwengineko ulaya ili kutoroka masharti magumu ya kazi yatakayoikumba uingereza baada kujitoa kutoka EU.

Chanzo: BBC news.
 
Wawe wapooleee
Waje tena Zanzibar wafanye Mikutano ya Uchaguzi uliopita,hahaha.Hao EU wenyewe majanga.
Eu tulieeeni,mlisema Zanzibar kuna blaa blaa,sasa nyie wenyewe mnaanza yale yale tena zaidi ya ya Zanzibar.Watu wameishafanya maamuzi,tulieni sasa na msilazimishe
 
Back
Top Bottom