Uhusiano wa Franco na Mobutu

Sawa mkuu tuachie sisi tufurahie vitu adimu na midundo adimu. Franco was a genious hana mfano.
 

Kwanz nikupongezee mkuuu kwamb wew nimfuatiliaj na mi napnda xan kujua histria ya huyu jmaaa mobutu vp naeza pata wapi maelezo zaid kuhuc huyu mobutuuuuu mkuuu????
 
Marehemu Thierry Mantuika Kobi huyu ndo alifundishwa ule upigaji gita la Luambo (Mi solo) hivyo nyimbo nyingi Franco alikuwa na hamsini zake kobi akipiga Mi Solo (gitaa chombezi). Mara nyingi alishirikiana na Marehemu Jerry Dialungana Kasi akiwa kwenye solo gitaa. Hawa waliingia OK Jazz kati ya 1976-1978. Wapigaji solo wengine wakati huo walikuwa Franco mwenyewe (Mi solo), Papa Noel (1978), Dizzy Mandjeku (1986 or 88).
 
Sawa mkuu tuachie sisi tufurahie vitu adimu na midundo adimu. Franco was a genious hana mfano.
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, unajua mambo ya music ni ya ajabu sana, ni kama mapenzi tu; demu unaye muona we mkali wenzio wanaona wa kawaida sana, miaka hiyo ya kina Franco ndio kina Michael Jackson nao walikua kwenye pick kimuziki, huwezi amini kaka, sijawahi kupenda nyimbo za kizungu kabisa except ule wa the Londoners baaasi, ila nyimbo za kina Pepe, Nyboma na wale wengine nimewataja hapo ju, aise ilikua lazima ninunue cassette zao, tena kaka uzi hu umenikumbusha ile studio ya kupiga copy ilikua mapipa pale inaitwa BINGO records, ilikua na kauri mbiu yake ya hivi, "muziki husahaulisha dhiki" Noma sana aise.
 
Kuna mwingine pia anaongezeka hapo kwenye solo anaitwa micherino Visi Mavatiku.
 
Baadhi ya wanamuziki nyota wa OK Jazz. Kutoka kulia Simaro Lutumba (1961-1993) Rhythm guitar, Josky Kiambukuta 1973, Ntessa Daliensti (Muzi), Malage de Lugendo(1980's), Madillu (1980), Youlou Mabialla Mwana wa Luambo, Mwana wa OK Jazz (1966) ndo muimbaji peke yake ambaye bendi yake ya kwanza kuimba ni OK jazz wengine wote waliingia wakiwa wametoka kwenye bendi zinazofahamika, Mangwana (1972) Ndombe (1975?) wote hao waimbaji. Hao wa mwisho wawili ni Jerry Dialungana(solo ) na Thierry Mantuika (Mi Solo)
 
Sasa mbona mnatuchanganya.... Jamaa hapo wanasema franco aliambukizwa ukimwi hawara yake .. wewe unakataaaa..
 
Yollou Mabiala ana sauti nzuri ya aina yake akikaa na Wuta Mayi utapenda.
 
Mavatiku alipoingia OK Jazz 1975 ndo Franco alipohamia kupiga Mi Solo na Mavatiku akawa anapiga solo gitaa. Jamaa mahiri sana. bahati mbaya kuna wakati Franco aliwahisi wanampamgo wa chini kwa chini kuanzisha bendi (mavatiku na ndombe) ndo ukawa mwisho wao. ndombe alikuja kurudi baadae. Mavatiku yeye alirudi kwenye project ya Lisanga ya Banganga (Franco, Ley na Mavatiku). Na josky alitupia sana hapo mavocal. Hao niliowataja hapo ukiacha Franco wote ni baada ya Mavatiku. Usimsahau Fan Fan na Bholen huko nyuma.
 
Yule aliyechezea yanga anaitwa Mayaula Mayoni mzee wa Mbongo, namfagilia sana nyimbo zake slow flani hv lkn tamu sana.
 
kama hukuwahi kupenda Mziki wa Franco basi hujawahi penda muziki kabisa ndugu yangu
 
Pepe Ndombe yeye alikuwa mzuri sana kwenye kuimba peke yake.
Uimbaji wa pekee sijui nani alikuwa zaidi fikiria Mangwana (mabele), Djo Mpoyi, malage, Carlyto na Madilu. Ndombe nafikiri aiimba mwimbo wake tu wa Voyage du Bandundu. Ndombe, Josky na Ntessa nafikiri hawa walikuwa ndo wakali wa nyimbo za kuita na kuitikia. Hapo hatujawazungumzia waimbaji wazamani (Vicky, Edo, Boyibanda, Youlou, Kwany, Mujos etc)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…