Wewe unayesema hakuna kabila la Wachagga kwanza kabisa naamini wewe si Mchagga maana ungekuwa Mchagga usingeongea hivyo
Kwa kukusaidia tu ni kwamba Wachagga wanafanana kwa kila kitu, hiyo tofauti iliyopo ni maeneo tu wanayotoka lakini mambo mengine yote wanaenda sawa
Kwanza mila na desturi za Wachagga wote ni moja yaani kuanzia vyakula vya asili, vinywaji vya asili, majani na miti ya asili, uchumba, ndoa, uongozi, majina ya machifu, imani za kidini kila kitu ni kimoja
Pili Wachagga huwezi kuwatenganisha kwani muingiliano wao ni wa kindugu zaidi hapa namaanisha koo au familia za kichagga zinapatikana maeneo yote ya uchagga, kwa mfano utakuta Massawe anapatikana Rombo, Kilema, Kirua Vunjo, Old Moshi, Uru, Kibosho na Machame
Ukikuta Temba anapatikana KIbosho, Uru, Old Moshi, Marangu
Ukikuta Ngowi anapatikana, Kibosho, Uru, Old Moshi, Marangu, Rombo
Ukikuta Kimaro anapatikana Machame, Kibosho, Uru, Old Moshi, Marangu, Rombo
Sasa kwa akili yako watu hawa unawatofautisha vipi?
Yani unaanzaje kunishawishi kwamba Urassa aliyeko Machame na Urassa aliyeko Rombo sio ndugu, wakati hatujasikia Urassa aliyepo Tanga?
Pia Wachagga wanafahamiana, wanatambuana na wanafahamu kwamba wao ni wachagga na mtu ambaye si mchagga wanajua si mwenzao na wanamuita kyasaka au (mndu o nuka) wakimaanisha mtu wa porini, kwa mfano unaweza kuulizwa huyo mtu ni mchagga?, unasema ee ni mchagga kutoka Rombo au Uru au Sanya Juu, lakini kama si mchagga utasikia tu hapana si mchagga ni kyasaka yaani hatokei sehemu yoyote ya uchagga
Mfumo wa Umangi na lugha zote zinafanana ila kuna kuwepo utofauti mdogo unasababishwa na ule umbali wa kijiografia kutoka sehemu moja mpaka nyingine
Ni kawaida kutokea utofauti kidogo wa lugha pale jamii zinapokuwa zimegawanyika kiuongozi hata kama ni jamii moja
Naamini mpaka hapo nimekusaidia kwa kiasi kama unataka kufahamu zaidi vipo vitabu vingi sana vinavyowahusu Wachagga katika maktaba karibu zote za vyuo vikuu nchini upitie utafahamu zaidi
Kwa maelezo zaidi nifuate inbox
Karibu sana