Uhusiano wa Chagga na Kikuyu

Uhusiano wa Chagga na Kikuyu

nzalendo

Platinum Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,901
Reaction score
14,611
Kutokana na Ramani ya Afrika ku fitinishwa mwaka 1884-1885,kuna Fitna baridi iliwekwa makusudi ili kukidhi VIU vya maharamia waliohusika katika mambo hayo.

Bila kujijua na kuendelea kuabudu fikra za maharamia hao bado tunaendelea kufuata mipaka waliyotuwekea kwa sababu zao.

Kwa mfano wamakonde wapo Tz na pia wapo Mzqe Je mpaka pale ulitakiwa uwe wapi? Hata hili sakata la Ziwa nyasa chanzo ni kuendelea kuabudu mipaka iliyowekwa na wale wezi zama hizo.

Angalia wamasai wapo Kenya na wapo TZz, kama hiyo haitoshi cheki wajaluo:Wanyambo je? hawasikilizani na wanyarwanda na wabaganda? Pia waha na watu wa fasi ya Kongo kina papaa wanasikilizana bila shaka.Pande za Mkoa wa Rukwa na Zambia huelewana bila taabu.

Wameru wapo kenya na Tanzania na wanasikilizana vizuri sana WaChagga katika maongezi yao kuna vitu husikilizana na vichache hutofautiana kutokana na kwamba wewe ni Mchagga wa wapi,kwa mfanno mRombo au mMachame Vivyo hivyo wa KIkuyu ni jamii hii hii ya wa Chagga,mbali na lugha kuzikilizana hata mambo yao ya kiasili kwa mfano ndoa zao,taratibu za ndoa zao ni zilezile za wa Chagga jaribu kufuatilia Star Tv(kwenye kipindi cha bridal blah blah).

Je ni lini Afrika itaweka tofauti zao pembeni na kuamua kuungana kuwa nchi moja?
Search Results
upload_2016-9-13_12-59-23.jpeg
Bob Marley- Africa Unite (live) - YouTube
 
hapo kwa wameru ni uongo mtupu wameru wa kenya hawasikilizani na hawa watz wameru wa tz wanasikilizana na wamachame

Swali langu kwako, kwa nini Wameru hawaitwi Wachaga kama wanasikilizana na Wamachame ambao wanajiita Wachaga? Au kwa nini Wamachame hawasikilizani na Warombo au Wakibosho wakati wote wanaitwa/wanajiita Wachaga?
 
Hata wachaga na Wakikuyo hawasikilizani hata mila zao ni tofauti na za wachaga
Kwa kukusaidia Wachaga na Wameru wa Tanzania ndiyo wanaosilikizana kwa lugha hadi mila zao ni moja
 
Kuna wakikuyu wengi wameadapt umasai na kuna muingiliano mkubwa baina ya wamasai na wakikuyu huko Kenya.
Kuna wakikuyu wengi ambao wamekuwa wamasai vizazi vingi vilivyopita.
Hata ukiangalia mawaziri maarufu wa kabila la wamasai Kenya unakuta wamechanganya na wakikuyu hivyo ukaribu wa wachaga na wakikuyu sio kama walivyo wamasai na wakikuyu.
Labda kama factor yako ni ujanja ujanja na biashara pekee
 
Hata wachaga na Wakikuyo hawasikilizani hata mila zao ni tofauti na za wachaga
Kwa kukusaidia Wachaga na Wameru wa Tanzania ndiyo wanaosilikizana kwa lugha hadi mila zao ni moja
Swali langu kwako, kwa nini Wameru hawaitwi Wachaga kama wanasikilizana na Wamachame ambao wanajiita Wachaga? Au kwa nini Wamachame hawasikilizani na Warombo au Wakibosho wakati wote wanaitwa/wanajiita Wachaga?
Kabila la Chaga linajumuisha tonation 11 za lugha inawezekana hata wameru nao wangekuwa katika hao kama Mchili au Chifu wao angekubali kujiunga na Chaga Kingdom wakati huo
 
Kabila la Chaga linajumuisha tonation 11 za lugha inawezekana hata wameru nao wangekuwa katika hao kama Mchili au Chifu wao angekubali kujiunga na Chaga Kingdom wakati huo

Kwa hiyo kwa maelezo yako unakubalina na mimi na kile ninachoamini siku zote kwamba HAKUNA kitu kama Kabila la Kichaga Dunia hii? Na badala yake kilichopo ni makundi mbalimbali ya watu yaliounganishwa na Wageni na hapa Wazungu kwa lengo la kututawala Waafrika?
Na hapa ni Tanzania nzima vivyo hivyo kama vile hakuna kitu kama Kabila la Wahaya au sijui Wasukuma au sijui Wanyakyusa wote hawa ni matokeo ya Ukoloni aidha Waarabu au Wazungu!
 
hapo kwa wameru ni uongo mtupu wameru wa kenya hawasikilizani na hawa watz wameru wa tz wanasikilizana na wamachame
Sina hakika saana, kama wana matatizo ya masikio,ila kazi ya masikio ni kusikia.(Unajua nini...Wa Rombo na Wakibosho hawasikilizani lakini wote wanajinasibu kuwa ni wachagga,,,lipi jema?Wote kuitwa Wameru ilhali hamsikilizani au muitwe majina tofauti na huku mwasikilizana?)
 
ni kweli Wameru wa Arusha na Kenya hawasililizani
(Unajua nini...Wa Rombo na Wakibosho hawasikilizani lakini wote wanajinasibu kuwa ni wachagga,,,lipi jema?Wote kuitwa Wameru ilhali hamsikilizani au muitwe majina tofauti na huku mwasikilizana?)
 
Kwa hiyo kwa maelezo yako unakubalina na mimi na kile ninachoamini siku zote kwamba HAKUNA kitu kama Kabila la Kichaga Dunia hii? Na badala yake kilichopo ni makundi mbalimbali ya watu yaliounganishwa na Wageni na hapa Wazungu kwa lengo la kututawala Waafrika?
Na hapa ni Tanzania nzima vivyo hivyo kama vile hakuna kitu kama Kabila la Wahaya au sijui Wasukuma au sijui Wanyakyusa wote hawa ni matokeo ya Ukoloni aidha Waarabu au Wazungu!
We wacha kuanika uhayawani wako. Makabila hayakubuniwa na wageni bali wao walitenganisha makabila kwa mipaka yao bandia ambayo hata hivyo tumeihalalisha.
 
Aliyekwambia akina maringo na waha wanaelewana lugha ni nani? Bora ungesema wafipa
 
Kwahiyo unataka kuniambia Zitto ni Mrundi.
Ngongo ukiondoa "n" ya kwanza imabaki gongo. Bila shaka umepiga hiyo kitu ha ha ha.

Yeye amekwambia waha wanasikilizana na wahutu/watutsi yaani warundi na wanyarwanda.

Wewe unahamisha unauliza eti zito ni murundi. Siyo uchizi huu?
 
Swali langu kwako, kwa nini Wameru hawaitwi Wachaga kama wanasikilizana na Wamachame ambao wanajiita Wachaga? Au kwa nini Wamachame hawasikilizani na Warombo au Wakibosho wakati wote wanaitwa/wanajiita Wachaga?
Nikikutana na wachaga nawaambia live hakuna kabila la wachaga. Ila kuna machame, kibosho, uru, marangu n.k. na hakuna lugha ya kichaga daima
 
Nikikutana na wachaga nawaambia live hakuna kabila la wachaga. Ila kuna machame, kibosho, uru, marangu n.k. na hakuna lugha ya kichaga daima
Ngoja nikueleweshe kwa mfano kiswahili n mkusanyiko wa lahaja 10 na zaidi mfno kipemba,kimtangata wanaweza kufanya mawasiliono kutokana na kushea misamiati, matamshi, sarufi na muundo wa sentesi sasa chukulia kikibosho, kimachame, kimarangu wanashea izo sifa nilizotaja hapo juu na ndio maana wanaesabika kama kundi moja. Ni mtazamo wangu nipo tayari kurekebishwa.
 
Hamna ukweli wowote wa bandiko lako. Wa meru wa kenya na Tz ni tofauti kabisa na wala hakuna uhusiano wa chagga na kikuyu, labda tu ulitaka kuwataja wachagga bila hoja ya msingi.
 
Ngoja nikueleweshe kwa mfano kiswahili n mkusanyiko wa lahaja 10 na zaidi mfno kipemba,kimtangata wanaweza kufanya mawasiliono kutokana na kushea misamiati, matamshi, sarufi na muundo wa sentesi sasa chukulia kikibosho, kimachame, kimarangu wanashea izo sifa nilizotaja hapo juu na ndio maana wanaesabika kama kundi moja. Ni mtazamo wangu nipo tayari kurekebishwa.
Ok. Jibu haya:-
1. Kichaga ni lahaja ipi?
2. Nani aliyesanifisha lahaja hiyo kuwa kichaga?
 
Back
Top Bottom