Uhusiano wa ardhi na mafanikio

Tanzanite klm

JF-Expert Member
May 7, 2013
453
376
*Uhusiano wa Ardhi na maisha*17*
Asalaam ndugu zangu,Hii ni jumatatu nzuri kubwa.
- Kuna siku moja katika andiko langu na pia katika kitabu changu kipya *Mgodi kati kati ya masikio* nilielezea juu ya miongoni mwa namna za kupunguza na kuondoa madhara ya negative forces katika mwili na nafsi yako, katika njia nilizotoa ilikua ni KUSAFISHA MAZINGIRA.
- Hiyo inaanzia mwanzo2:15, Mungu alipomuumba mtu alimpa amri akaitunze nchi, iyo ni amri ya kwanza ya kutunza mazingira, upo uhusiano wa kutunza mazingira na good karma.
- Lakini pia Ardhi ni lango la kuweka kumbukumbu na kuamia nini ufanye katika maisha yako;
Kuna andiko moja Nabii anasema na Ardhi; Ee nchi nchi sikia neno la Mungu, andika habari juu ya mtu huyu ya kuwa hatafanikiwa, hana watoto, .. mambo meengi, yule jamaa aliiambia, ivyo tunaona basi Ardhi inayo masikio ya kusikia.
-Kaini alipomuua ndugu yake, Damu ilikua inalia kutoka ardhini,
- Mungu mara nyingi alipotaka kuwaadhibu wanadamu Alipiga nchi; Na kunamaali baadae akasema Sitaipiga tena nchi.
- Musa alipokutana na Mungu, kitu cha kwanza alimuambua vua viatu.
- Ipo connection kubwa sana kati ya udongo na unyayo.
- Jaribu kukumbuka kipindi ukiwa mdogo labda primary ulikua unapekua sana na ndio kipindi ulikua na machale na kumbukumbu mnoo;
- Ndio maana inashauriwa sana unapotaka kufanya connection ya maombi nzuri, uwe peku, miguu ikanyage ardhi.
* Usipojua nguvu ya ardhi haitabadili nguvu yake, Waganga wanajua sana nguvu iliyopo katika ardhi, ndio maana waganga lazima wafukie madawa yao pamoja na maneno*
- Wanajua ardhi inatunza kumbukumbu na inafuata amri ya ilichoambiwa.
-Ndio maana kuna ardhi nyingine unaeza ishi hujui ilifanyiwa tambiko gani au ilishapewa order gani.

-Mimi kila ninapoenda na kila asubuhi lazima Niitamkie Ardhi maneno mazuri juu yangu; Ipo hivi wanasayansi hawajagundua kanuni yeyote, ila wamezikuta zipo ku prove tuu; Dunia imeundwa kwa ustadi mkubwa sana; Kila kitu kipo katika kanuni, ndio maana hata kanuni ya malipo hapa hapa duniani the law of karma inafanya kazi uwe unajua au hujui.
Ukipata nakala ya kitabu changu mgodi wa dhahati katikati ya masikio utajifunza kanuni nyingi zilizosaulika zinazotawala mfumo wa maisha ya mtu na namna ya kutumia nguvu yako ya kiroho kupata utakacho ukifuata kanuni.
0752890158-Whatsapp kupata softcopy
 
Aisee namkumbuka bibi Kidude wa Zanzibar (Mola amrehemu huko aliko) moja kati ya maswali niliyowahi kumuuliza ni Nini siri ya kuishi maisha marefu? Alinijibu, yeye havai viatu kwani kuvaa viatu ni chanzo kikubwa sana cha matatizo mengi yanayopelekea kufupisha maisha yetu ikiwemo maradhi. Alisema unapotembea peku unaunganishwa moja kwa moja na nguvu “energy” ya asili ya uumbaji ambayo inakupa faida na kuishi kwingi..
Inasemekana bibi yule aliishi zaidi ya miaka 100 akiwa na nguvu zake mpaka mauti inamkuta
 
Aisee namkumbuka bibi Kidude wa Zanzibar (Mola amrehemu huko aliko) moja kati ya maswali niliyowahi kumuuliza ni Nini siri ya kuishi maisha marefu? Alinijibu, yeye havai viatu kwani kuvaa viatu ni chanzo kikubwa sana cha matatizo mengi yanayopelekea kufupisha maisha yetu ikiwemo maradhi. Alisema unapotembea peku unaunganishwa moja kwa moja na nguvu “energy” ya asili ya uumbaji ambayo inakupa faida na kuishi kwingi..
Inasemekana bibi yule aliishi zaidi ya miaka 100 akiwa na nguvu zake mpaka mauti inamkuta
tutamuuliza mrisho mpoto.
 
Back
Top Bottom