chase amante
JF-Expert Member
- Feb 24, 2018
- 5,553
- 2,074
Naomba niwape pole wakazi wa Dar Es Salaam, Polisi na ndugu wa Polisi waliofariki katika tukio la leo.
Tukio hili la anayeshukiwa kuwa jambazi kufyatua risasi hovyo, limeshtua watu wengi. Niwape hongera Polisi kwa kazi hiyo.
Naomba kwanza niseme kuwa huyu mtu sio mgeni machoni pa vyombo vya usalama. Inaonekana wanamjua, na ndio maana wamemuua moja kwa moja na hawajataka kumkamata. Pia, anaonekana hakuwa na nia ya kuua raia, kwani hakuua yeyote aliyekuwepo kwenye gari au karibu zaidi.
Kuna ujumbe alikuwa analeta kupitia tukio hili. Cha kwanza, nikutaka watu wamuone na aonekane kwenye media kwani kaenda eneo ambalo lina ulinzi mkubwa sana na alijua kuwa atakufa tu. Nadhani alitaka kuonesha kwamba Polisi hawana huruma na weledi, kwa kuwa hawatamkamata.
Uhusiano uliopo na kesi ya Mbowe, ni kuwa huyo jambazi alikuwa anataka kuonesha maana sahihi ya ugaidi wa silaha. Pengine katumwa kujitoa mhanga au alikuwa na madai yake binafsi lakini lazima utakuwa ni mpango wa kikundi cha watu na siyo kwamba huyo jambazi ni kichaa.
Ni mtu timamu, na ndiyo maana hajalenga au piga risasi raia baki yeyote au kitu chochote kwa lengo la kuua.
Wito wangu, ni kwa Polisi wote nchini hasa wa usalama barabarani na watu wa idara ya usalama wa taifa kuongeza umakini ili lisije jirudia tukio kama hili. Pia, ufanyike uchunguzi wa kina zaidi kuhusu tukio hili